andate
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 2,651
- 1,006
Kweli usim-count mtu ni msafi kwa sababu tu kasema fulani(mwingine) ni mchafu.Mume wangu nakupenda sana, ujilinde, mimi siwezi kukulinda au kukuchunga kila uendapo, unaweza ukawa kuna mambo unayafanya ambayo mimi hutaki niyajue na wala sitaki nijue, Tafadhali sana lolote lile utakalofanya jua kuna ukimwi, Angalau ukumbuke kutumia kinga, kwakweli sitakusamehe wala kukuhudumia siku ukipatwa na ukimwi. Hayo ni maneno ambayo mke alikuwa anamwambia mumewe. Lakini baada ya miaka kadhaa ya ndoa kama nane hivi mke ikajulikana yeye ndio amepata ukimwi bahati nzuri mume alipoenda kucheki yeye alikuwa bado hajaathirika. Mbaya zaidi jamaa hajawahi kusikia wala kuhisi kama mkewe anatoka nje ya ndoa mpaka alipogundua dalili za ukimwi kwa mkewe.
Kweli ndoa ngumu. Kupata mtu muaminifu ni ndoto.
Hapa ndipo pale utakapogundua kuwa maamuzi ya kuvaa au kutokuvaa condom yapo kwa mwanaume. ndio maana mwanaume akisikia mkewe ametembea nje hasira yake inakuwa mbaya sana, na baada ya hasira kuisha bado kuna hofu itaendelea kutanda, je jamaa alitumia au hakutumia?
Mbaya zaidi mihuni ikishajua huyu ni mke wa mtu ndio huwa haitumii condom.
Na UKIMWI huu sometimes ndoa ni kama risky bussiness.