UKIMWI bado upo mazee, usiuze mechi kijinga!

UKIMWI bado upo mazee, usiuze mechi kijinga!

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,144
C&P
Mhuni Smart nipo kwenye mbishe zangu nini, nakimbiza kama kawa mara paap, nikiwa naperuzi kwenye mamitandao nini, nakutana na ishu moko important kinyama ambayo kama vipi nimeona itakuwa barida nikishea na ma-blood!

First of all nikukumbushe mwanangu kwamba Desemba moko, majumapili hiyo wikiendi hii, ni siku ya ngwengwe duniani! Siku ya ngoma ndiyo, wengine wanaita moto, umeme, gridi na majina kibao, lakini ishu ni kwamba ni siku ya ngoma! Usijisahaulishe wewe!

Sasa ishu niliyogumiana nayo, unaambiwa mtu bati mbili hapa Bongo, zinapata ngoma deile! Usione kama labda nataka kukuyeyusha nini, hayo ni matakwimu ya Tacaids na yametolewa na mshua mwenyewe wa hiyo mambo kipande cha Dom, anaitwa nani yule mshua, Makoba sijui, huyohuyo najua ushamnyaka.

Picha linaanza, kati ya hizo mtu bati mbili zinazopata ngoma deile, fote pasenti (40%) ni machalii wenye chini ya aka 24! Huu si msala mazee? Hapa maana yake waliopo denja zoni ni machalii wa chuo nini, madogo maskuli na kitaani na mamanzi wakaree hawa wanaoanza kujua kuoga ndo wanaongoza kwa kupata ngwengwe deile.

Usifanye masihara, ngoma noma mazee! Unapiga zako chuo nini, unahitimu unakula zako nondo, unaingia kitaani kuanza kukimbizana na laifu, mara paap! Afya inaanza kuleta mgogoro! Unavuta ukiwa na mandoto kibao kichwani, unawaacha washua na huzuni, wana wanakuchimbia futi sita chini, imeisha hiyo!

Ukicheki laifu wanaloishi madenti, machalii wa chuo, mahosteli nini, daah, noma sana mazee! Inaitwa chipsi funga hiyo, wana wanajipigia tu, mwendo wa kitonga, unajiuliza machalii wanakumbuka kwamba kuna ngwengwe?

Manzi akipewa ofa ya kiepe kuku na kyoda nini, jamaa anajilia vyake kiulaini! Wale wanaozibuka nao ndiyo msala zaidi, manaiti klabu huko hakufai mazee! Mikasi njenje, manzi akipigishwa savana mbili tatu, wana wanapita naye, tena wanauza mechi, hakuna cha zana wala nini! Hatari sana mazee.

Namkumbuka mwanangu Ngwea alishatoaga pini lake moko kitambo hicho linaitwa AKA MIMI! Mwana FA na yeye akajaga na ile Alikufa kwa Ngoma, wasanii kibao nini wanaimba, mwanangu Jebby naye akaachia Marehemu Kaacha Orodha lakini dah, Wabongo wanavunga yani, Take care mwanangu.

Wapo washua kibao nao pigo zao siyo kabisa! Yaani anajijua alishaunguaga kitambo, kwa sababu mtonyo upo nini, anapiga mavidonge, mamisosi ya nguvu, basi anaendelea kudunda tu kitaani sasa mbaya zaidi, anawaumiza mamanzi macho juu huko kitaani! Mamanzi nao wanatoa mchezo kwa machalii wenzao huko maskuli na makoleji nini, mwisho cheni inakuwa kubwa kinyama.

Oyaa! Sanuka mwanangu, mbishe za kujifanya kidume au sijui sista duu nini, siyo mpango! Kama upo skuli piga msuli, kama upo chuo fanya yaliyokuleta, bata zipo tu lakini usiingie kiboyaboya! Ngoma ipo na inatesa kinyama na mwisho lazima uvute! Take care, ukiona namna gani basi kuwa na manzi mmoko au msela mmoko na kama vipi uaminifu ndiyo dili tauni hapa!

Piga shule uje kujenga taifa wewe! Acha uboya wa kutembea macho juu, ukiona manzi ana kijungu basi macho yanakutoooka! Ukiona mshua ana mawe, ndinga kali nini mtoto wa kike unajiresi! Utakufa mbwa wewe.

Mazee Desemba moko ndiyo hiyo, pigeni utepe mwekundu wanangu, tunakumbushana tu laifu jinsi lilivyo bovu hili, halafu ujikute na ngwengwe juu, si utavuta kwa mastresi? Take care, ngwengwe ipo na ukiipata imeisha hiyo.
 
Dah, kumbe sina!

Lakini nishawahi kusikia kwamba, unaweza ukawa na virusi vya Ukimwi, lakini usiwe na Ukimwi

Lakini pia unaweza ukawa na Ukimwi bila kuwa na virusi vya Ukimwi!

Hilo limekaaje nduguzanguni!?
 
Ungekuwa ukipima na ukikutwa unao unapewa dawa,ningeenda kupima, ya Nini kujipa presha ya bure, waache wenye viherehere waende

Acha tu mie kuna siku nilipatwa na taharuki sitasahau. story iko hivi, watu wa benki ya damu walikuja kanisani kwetu kuomba damu, mie nikawa kiherehere kuchangia, wakasema anayetaka majibu ya damu yake aje siku ya Jumatano pale ofisini kwao Bugando kuchukua majibu. Mwanamke nikajitosa kwenda kuchukua majibu.

Yule dada mtoa majibu nikamsikia ana sema wewe ni Positive, maneno mengine ya mwanzo siku ya sikia zaidi ya neno "positive", uwiiiiiii pale nikaanza kulia kwa sauti, makamasi yakaanza kutoka mfululizo. Yule dada akawa ananishangaa, mie ndio sauti ya kulia ikazidi. Wenzake wakatoka ofisi zingine kuja kushuhudia kuna nini? Wakamuuliza yule mwenzao "wee Vicky mbona huyu dada analia kuna nini?" akawajibu kuwa "hata mimi ninashangaa nimeona tu ghafla analia, tena kwa sauti kubwa..."

Basi, wakaniuliza ni nini dada mbona unalia? Mie sasa kwa sauti ya kwikwi, nikawajibu kuwa amenipa majibu yangu yameonesha nina ukimwi..." ndipo Vicky akaanza kujitetea kuwa, "mie nime mwambia damu yake ni GROUP O POSITIVE, ghafla akaanza kulia...." hahahahahahahah, basi nikapewa majibu yangu, wakasema, HUNA HOMA YA INI, HUNA UKIMWI, HUNA TATIZO LOLOTE, TUNAOMBA BAADA YA MIEZI MINNE URUDI TENA KUCHANGIA DAMU...."
 
Back
Top Bottom