Ukimpenda Utamjali na Kumlinda

Ukimpenda Utamjali na Kumlinda

Bimkubwa hapo moyoni alikuwa anajisemea kidume nimepata
Mi ni mkimya sana na huwa sipendi ugomvi hata familia yangu inalijua hilo ila siku ile sikutaka kuwa mnyonge bi mkubwa akivunjiwa heshima wakati hata yeye sio mkorofi kabisa. Humu wengi wanamfahamu anajulikana sana ni vile tu tunatumia fake ID.
 
Nimeishia hapo uliposema jinsia ke akikubali vile umempenda, umemjali na kumlinda atakutii,

Hapo inategemea, mwanamke anachojali ni hisia zake kwako, ke hajali kabisa kama umemnunulia gari, umempa Figo kuokoa maisha yake, umemaliza miezi 59 kumtongoza, umemsomesha chuo, ke hajali unampenda kiasi gani, ke hata umpende vipi na kusacrifice vipi kwa ajili yake, kama tangu mwanzo alikuwa anakuona nyani ataendelea kukuona nyani tu, kwanza ke wengi wa sahivi ukiwaambia unawapenda, hata kama ni ukweli, kichwani watakuona wewe ni muongo na mnafiki unaetaka kula papuchi halafu utembee, kumbe kiuhalisia unampenda kweli Kasie


Nimekusoma na nimekuelewa....

Nilisema awali, hii mada ni pana sana....

Watu tunatofautiana kutokana na hulka kila mtu na yake. Sio KE wote wataoelewa huu ulinzi wa ME unamletea faida gani akiamua kuajiri bodyguards wampe ulinzi.

Nilishasema pia hapo mwanzo, ulinzi asili anaoutoa ME kwa KE ni zaidi ya kushika silaha na kupigana vita kwa ajili yake....
Ni kujitoa aka to sacrifice. Its only when you reach a point of no return on pure true love, that's when you can sacrifice yourself for your loved ones.

Nimejaribu kubadili lugha sijui nimeeleweka....!!!

Natambua wako wanawake kwa wanaume waliokwishaumizwa na mahusiano ya nyuma na walijitoa kindakindaki matokeo yake wameapia hawataki kusikia KE wala ME...

Siwalaumu, dunia iko rafu sana, haina kupetipeti na katafunua tupa kule kafie mbele.

ILA, ukibahatika kumpata umpendae nae akakuelewa na kukukubali vile ulivyo.....
Am telling you, you'll die smiling no matter what circumstances you are passing through.

Kasinde Matata.
 
Si unazijua tabia za makonda wengi zilivyo na maneno yao machafu machafu, afadhali hata makonda wa miaka hii wana ustaarabu kidogo, miaka ya nyuma kazi ya ukonda ilikuwa inafanywa na wahuni sana kwahiyo mambo mengi ni uhuni uhuni tu. Nilimjia juu yeye mwenyewe akanywea, mama ananivuta mkono ananiambia twende achana nae asije akakupiga bure, nikamwambia athubutu aone kama hajalala jela, watu wengine wakaingilia kati kumkosoa vikali konda mpaka akamuomba mama samahani.
Wewe ni mbinguni moja kwa moja.

Mimi unitukanie mama yangu au mpenzi wangu mbele yangu...nakuwa mbwa nisiyefaa...utajuta kufungua mdomo.
 
Walindaji ndio wawindaji.. niongeze sauti au nipunguze...?

Kiberenge acha herehere za mapengo yako...

Kwahiyo utamuwinda dada yako wa damu?
Utamuwinda mama yako mzazi?
Utamuwinda binti yako?

Uhalisia uko kwenye makundi yote, sikatai utamuwinda mkeo, ila ulinzi huqnza rasmi baada ya mawindo yako kuwa kwenye milki yako.

Sijui umenielewa......!!!

Usijekuwa wale wanaowinda na kuacha mizoga wavivu kutumia fani ya ulinzi wa asili waliopewa.
 
Bibi wa mahaba, sijui nielezeeje nnavyompenda na kumkubali mama yangu. I wish nije nipate mke mwenye tabia kama zake.

Wooow......!!! Nimepata namna unatamani iwe.....

Iko hivi kuna nguvu za asili kwenye hili tufe tunaloishi. Usiache kufanyiq kazi matamanio yako, fanya matamanio yako kuwa lengo lako ... sijui nielezeeje ila kuna usemi positive poles attracts positive energy.

Weka nguvu hapo kwenyw hayo matamanio, fanya mantra and the like...

Si mtaalamu kwenye hayo ila naaminini kitu kinawezekana hata kama matokeo yake ni asilimia 5 ya 100. Ukiamini bila wasiwqsi wowote huwa.

Nakutakia heri kwenye mema yote uyatakayo.
 
Kuna Kijana Mmoja mtaani kwetu alikua analinda hivihivi kumbe analindia Wenzake Mwaka jana yule Binti kaolewa na Msela Wa Dar Nyie😂😂

Yanatokea, yalishatokea na si ajabu yakaendelea kutokea.

Saa zingine ni vyema kuruhusu aende kama hataki ulinzi wako, usilazimishe haswa kama amekuinesha dalili zote hahitaji your masculine...

Sasa kama binti alifanya uhalifu wa kufurahia ulinzi wa kaka mtaani kisha akaenda olewa na mwingine hilo ni tatizo.
 
Back
Top Bottom