Ukimpenda Utamjali na Kumlinda

Ukimpenda Utamjali na Kumlinda

Habari za muda huu,

Rejea kichwa cha uzi, kinaongea kwa mapana ila yaliyopo kwenye akili yangu yako kwenye nyanja tofauti tofauti.

1. Mwanaume kumjali jinsia ya kike yeyote yule aliyempenda.

Baba mzazi/mlezi kwa binti yake:
Kuna wababa asisikie au kujua binti yake ametendwa isivyo, yuko radhi ache kila kitu ila usalama wa binti yake kwanza.

Mume kwa mkewe:
Mwanaume akisikia au kujua kuna wanaotaka mdhuru mke wake huwa mbogo na hacheki na kima mbele ya mkewe wala kuleta matani. Achana na wivu kuna ile kumlinda bila kuwa na mtutu wa bunduki...

Kaka kwa dada wa damu (sibling):
Kaka wote wanaojielewa hawakotayari kuona dada yake/zake wanapata tabu. Awe mkubwa ama mdogo, atapambana kuhakikisha dada yake/zake wanakuwa salama.

Mtoto wa kiume kwa mama mzazi:
Hapa wanaume wenyewe mtaongea zaidi, ila iko asili sio tuu mapenzi makubwa yako kwa mama mzazi ila hata kuhakikisha mama hapati shuruba, hateseki yaani ile kumkingia kifua kwa namna yeyote ile...

Kiasili mwanaume ana mabavu kumzidi mwanamke, misuli na nguvu za ziada zipo kwa sababu maalum. Ukiacha kupigana na ubabe, kazi kubwa ni kutoa ulinzi.

Hakuna kitu mwanamke anapata tulizo la akili kama akijua ndani yuko ya mtu anaweza mkingia kifua kwenye jambo lolote lile hata kama sio la hatari...

Kale kahisia kuwa kuna sauti nene inakoromea shambulio lolote lile linaloelekezwa kwenye paa lenu bila ugomvi ila kwa hekima na umakini na msisitizo usio wa mchezomchezo.

Si wanawake wote ni wadau wa mambo za kuwa (protected), ila kuna raha yake... ni asili.

Ukiona hajali, hajisumbui nawe, hajihusishi na mambo yako, haimhusu uko salama ama hauko salama...

Tambua tuu kuwa haupo kwenye himaya yake ya anaowapenda.

Ngumu kukubaliana na uhalisia ila bora kuchukua njia mapema utabaki salama hadi pale atapotokea wa kukujali.

Hiyo ni upande mmoja, kurudisha majibu ya kuwa ulinzi wako umekubalika na unatambulika ni kukuheshimu.

Jinsia ya KE akikubali vile umempenda, umemjali na kumlinda, atakuheshimu na ATAKUTII.

Huu mjadala ni mpana sana ila akili yangu ililenga hapo kwa ME kumpenda, kumjali na kumlinda KE.

Wasalaam,

Kasinde Matata.
ni kweli mambo haya yapo, tena sana tu miongoni mwa jamii tunamoishi.

ila kwa kiasi fulani mimi nadhani inachochea ulegevu katika kujitegemea katika kujilinda, na kisha baadae huleta majuto, manung'uniko na laumu nyingi sana endapo huyo mlinzi kipenzi anapokua hayupo mathalan ameitwa na Mungu n.k. Upweke, hofu ya usalama na unyonge hupindukia zaidi kwa mlindwa kipenzi.

Ni vizuri hali hiyo ya protections kwa vipenzi wetu ikaambatana na kuwapa uwezo au kuwajengea uwezo na ujasiri wa kujilinda wao wenyewe wawapo kekeyao.

Tunajifunza kwa miongoni mwa familia bora sana zenye protection sana kwa vipenzi wao mitaani Ila sasa baada ya zile protections kutoweka, tunaona familia na vipenzi vile vinaharibika kabisa, kwa kuwa hawana tena wa kuwaprotect, na wao hawana uwezo wa kujiprotect, walizoea kuwa protected.

Therefore ukimpenda, utamlinda, utamfunza na utampatia nyenzo na mbinu za kumpatia ujasiri wa kujiprotect mwenyewe unapokua haupo...

Thank you madame Kasie
 
Binafsi alishanifundisha jinsi ya kujilinda hata niwapo barabarani.

Akaenda mbali zaidi kwa kunipatia watu wa kuwatafuta endapo nitapata dharura ya haraka ikiwa yeye sitoweza kumpata kwa uharaka.

Mungu amlinde mlinzi wangu!
 
Yes,
thats true love.
wafundishe vema unaowaprotect kwa udi na uvumba wasidhurike wajitegemee kujiprotect wenyewe pia, ni muhimu sana, kwasababu, sisi ni wanadamu, kuna leo na kesho you never know.
 
Japo ulinizuia nisikujibu, nasemea hapa asante sweetheart.

Unachokiongelea hata mimi niko hivyo siku hizi, hadi najiuliza ndio nimekuwa mtu mzima busara zimeongezeka au vipi?

Niko ktk stage sitaki kabisa ugomvi na watu, nafurahia maisha coz yana vingi vya kunipa furaha kuliko ugomvi.
they say, 'don't let a stupid person drags you into his level, he will always beat you with experience'...!!

ndiyo love, Life still has a lot to offer, ni bora tuchague kuwa positive na kuwa na furaha over and over again..!!
 
Kibinadamu ni ngumu 😂😂😂 ilaaa kiimani tukikaza tunaweza na mwisho tutazoea kutokulipa ovu kwa ovu, tutajikaza kutolipiza kisasi na kuacha ghadhabu ya Mungu ifanye kazi yake.
Hakika Sweetheart, kwa akili zetu ni ngumu mno mno, inahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu kuishi na kutembea katika Hekima yake..!!🙏
 
Inawezekana kumbariki na kumwombea aliyekuudhi ikiwa unaye Roho mtakatifu, kibinadamu Si Rahisi, shetani hutumia na kuinua watu waje kutuchokoza na kutuonea, Nia yake umtukane mtu huyo au umjibu Kwa kurudisha matusi Ili achukue matusi Yako na kuyapeleka Kwa Mungu Ili kukushtaki uadhibiwe.

Ukimbariki anayekuudhi na kumuombea unapata faida kubwa moja,

Kumsamehe na kumbariki aliyekuudhi bila Yeye kuja kukuomba msamaha kunaondoa Sumu ya matusi ndani ya moyo wako, AMANI ya moyo wako itakurudia.

Tendo Hilo litarudi kurudisha HATIA na kukosa amani zaidi Kwa aliyekuchokoza, hautapita muda atakuja na kutubu kwako, jambo ambalo, ungerudisha matusi isingewezekana.

Kumsamehe aliyekuonea inakupa wewe Amani na kumwachia Mungu akulipie kisasi, maana imeandikwa kisasi ni Cha Mungu, ukisamehe, Mungu atakwenda kukulipizia kisasi Kwa mtu yule kama hatotubu.

Wezi waliowahi kuibia WATAKATIFU na hawakurudi kutubu, walipata ADHABU ya Mungu bila kujua, na ADHABU ya Mungu ni nzito na ya HAKI.

Amen
Shukrani sana dear Rabbon kwa hili somo zuri, Mungu akubariki mno tafadhali..!!🙏🙏
 
Si unazijua tabia za makonda wengi zilivyo na maneno yao machafu machafu, afadhali hata makonda wa miaka hii wana ustaarabu kidogo, miaka ya nyuma kazi ya ukonda ilikuwa inafanywa na wahuni sana kwahiyo mambo mengi ni uhuni uhuni tu. Nilimjia juu yeye mwenyewe akanywea, mama ananivuta mkono ananiambia twende achana nae asije akakupiga bure, nikamwambia athubutu aone kama hajalala jela, watu wengine wakaingilia kati kumkosoa vikali konda mpaka akamuomba mama samahani.
Bimkubwa hapo moyoni alikuwa anajisemea kidume nimepata
 
Back
Top Bottom