Mzigua90
JF-Expert Member
- Sep 23, 2014
- 38,383
- 88,739
Huu wimbo wa Diamond siupendi hata kidogo,
Siyo kwamba uliimbwa vibaya ama simpendi Diamond, hapana bali unanikumbusha tukio la huzuni.
Nikiwa nausikiliza mida ya saa 9:30 usiku kwenye mgahawa unaotazamana na barabara, kuna Dada mmoja[kama 26-29] aliyekuwa na matatizo ya akili, mjamzito na asiyekuwa na makazi.
Huyo Dada akiwa anavuka barabara aligongwa na pikipiki aka anguka na kupoteza fahamu katikati ya barabara.Kabla ya watu kugundua uwepo wake barabarani fuso ilimpitia na kumkanyaga, nilisikia miguu na mikono ikivunjika kama kuni kavu.Jamaa mmoja aliyetaka kujaribu kumvuta pembeni alirudi mbio alipoona semi imekolezwa ambayo ilimpitia yule Dada kwa mara ya tatu.
Baadae barabara ilifungwa ili kumtoa barabarani[kilichonishangaza tumbo na kichwa havikujeruhiwa],
Wakati hayo yote yakitokea huo wimbo ulikuwa ukipigwa kwenye redio.....nikisikia anaposema ukilala lala salama, picha inanijia anamwimbia yule Dada aliyefariki kwa ajali kwamba akila alale salama.
It was too odious.
Pole sana. Kumbukumbu mbaya sana hiyo