SoC03 Mazingira na changamoto zake

Stories of Change - 2023 Competition

Lvandason Noel

New Member
Feb 10, 2017
1
1
Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyo mzunguka mwanadamu. Hii ni pamoja na miti, bahari, anga hewa. Ili binadamu na viumbe hai wengine waweze kuishi vizuri wanahitaji mazingira yaliyo safi na salama.

Mazingira safina salama ni yale yasiyo athiri afya ya mwanadamu na afya ya viumbe hai wengine na kusababisha magonjwa mbalimbali. Mazingira yanapo kuwa safi na salama upelekea binadamu kufanya shughuli zake za uzalishaji vizuri na kupelekea binadamu huyu kukua kiuchumi na kijamii kama vile kuwa na familia iliyo bora, mahusiano mazuri kati ya wanafamilia, mahusiano mazuri kati kati ya jamii Moja na nyingine.

Shughuli za kila siku za binadamu ndizo zinazo pelekea mazingira kua safi na salama pia ndizo zinazo pelekea uharibifu wa mazingira na kufanya mazingira kuto kua safi na salama. mfano kupanda miti sehemu mbalimbali ya nchi, Kilimo cha kuzingatia kanuni za kitaalamu, uvuvi wa kuzingatia sheria na kanuni zilizo wekwa na wizara ya mifugo na uvuvi ni moja ya shughuli za binadamu zinazopelekea kua na mazingira safi na salama ya kuishi.

Zipo changamoto mbalimbali zinazopelekea mazingira kuto kua safi na salama

1) Uharibifu wa mazingira unaofanywa na shughuli za kibinadamu ni changamoto Moja wapo inayofanya mazingira kuto kua safi na salama, mfano Ukataji wa miti, misitu kwa ajili ya makazi na upatikanaji wa kuni kwa ajili kupikia, matumizi ya Sauti(muziki) kwenye biashara

Matumizi ya kuni kama chanzo cha nishati ya kupikia hupelekea maeneo mbali mbali ya nchi kua jangwa, na kukosekana kwa mvua ambayo pia hupelekea Kilimo kutofanyika vizuri kutokana na ukosefu wa mvua hivyo basi chakula kutopatikana kwa wingi. Pia matumizi ya nishati chafu na uchomaji wa misitu hovyo hupelekea uchafuzi wa anga hewa na kusababisha magonjwa kwa binadamu kama vile kansa ya ngozi na magonjwa mengine yatokanayo na hewa kuwa chafu.

Suruhisho la hii changamoto ni kuwezesha jamii kuweza kupata chanzo cha nishati safi mbadala ambacho ni rafiki wa mazingira, hakiharibu hali ya hewa na pia hakileti magonjwa kwa binadamu.

Chanzo hiko ni matumizi ya Gesi asili(LNG) na gesi ambayo si asilia(LPG). Kwa sasa upatikanaji wa hizi gesi upo lakini si kwa kiwango kikubwa kwa watumiaji wa mwisho hii ni kutokana kuwa bei zake ziko juu na upatikanaji wake kuwa hadimu kwa watu wengi hasa walio vijijini hawawezi kumudu hizi bei. hivyo kuendeleza matumizi ya mkaa na kuni.

Serikali iwajibike katika hili kwa kuhakikisha inapanga na kusimamia bei za gesi watu wengi waweze kumudu kununua. Pia serikali inapaswa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji katika sekta ya gesi ili kila muwekezaji aweze kuvutika kuingia na kuwekekeza katika maeneo mbali mbali ya nchi ili kurahisisha upatikanaji wake hasa vijijini hii pia italeta ushindani mzuri wa kibiashara na kupelekea bei kushuka zenyewe.

Changamoto nyingine inayotokana na shughuli za kibinadamu inayoperekea uharibifu wa mazingira ni matumizi ya sauti mfano kupiga muziki kwa sauti iliypitiliza, matumizi ya honi za magari kupitiliza hupelekea mazingira kuwa si safi na salama. kwani matumizi yake yanapokuwa yamezidi kiwango kilichowekwa na mamlaka husika inayosimamia shughuli zote za mazingira(NEMC) hupelekea kuwa kero kwa watu wanaoishi maeneo jirani na izo shughuli. Pia huweza kusababisha matatizo zaidi mfano matatizo ya kusikia na magongwa ya presha.

Suruhisho, Serikali kupitia taasisi yake ya NEMC na taasisi zingine zitenge maeneo ambayo ni maalumu kwa shughuli zinazohitaji sauti na kutoa vibali vya shughuli iyo inayohitaji sauti kwa wale waliokidhi vigezo hii itasaidia kuondoa kuondoa kero ya kelele na kuepusha magonjwa kwa jamii zinazohishi karibu na maeneo ayo.

2) Changa moto itokanayo na majanga ya asili. Majanga ya asili hayasababishwi na binadamu moja kwa moja hutokea tu yenyewe kutokana na uvutano wa nguvu za dunia, isipokua shughuli hasi za binadamu kama vile kukata miti uongeza maafa pindi yanapotokea. Mfano wa majanga haya ya asili ni tetemeko la ardhi, Kimbunga.

Pindi yanapotokea mazingira yanakua si safi na salama tena kwa binadamu kuishi kwani kunakua na uharibifu mkubwa wa mali na hata vifo kutokea au watu kupata ulemavu wa kudumu.

Suruhisho, Serikali kupitia taasisi zake za mazingira zitambue maeneo hatarishi yanayo weza kupata matetemeko ya mara kwa mara na kuweka marufuku ya watu kuishi na kufanya shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom