Ukiambiwa uchague kimoja kati ya hizi project za Kilimo utachagua ipi? na why?

1. Project ya Ng'ombe wa maziwa
2. Project ya Ng'ombe wa Nyama
3.Project ya Mbuzi wa nyama
4. Project ya Mbuzi wa Maziwa.
5.Project ya Kondoo wa nyama
5. Project ya Kuku wa Mayai
6.Project ya Kuku wa nyama/Kienyeji/Chotara
7.Project ya Ufugaji wa nyuki
8.Project ya kilimo cha uyoga
9.Project ya protein mbadala ya Binadamu au mifugo.
10.Project ya ufugaji Samaki.
11.Project ya uzalishaji wa vyakula vya mifugo
13.Project ya Kilimo cha nafaka
14.Project ya Kilimo cha matunda ya muda mfupi au muda mrefu
15.Project ya Spice na herbals
16.Project ya miti ya Mbao na kuni
17.Project ya Sungura
18.Project ya Kware/ Kanga
19.Projects ya Ducks
20.Project ya Miche ya matunda, mboga na miti mingine.
21.Project ya Petties animals
22.Project ya Nguruwe


Unachagua moja tu na sababu zako tusaidie.
14. Kilimo cha matunda ya muda mfupi!
Why?

1. Ni aina ya mradi unaonivutia sana

2. Inaweza kuwa ajira ya kudumu. Nikiwa na "plots" kadhaa nitakazokuwa nikilima kwa kupokezana, matunda yanaweza kupatikana majira yote ya mwaka na hivyo kutoa ajira ya kudumu kwa watu kadhaa. Hiyo itasaidia "kujitengenezea" wateja wa kudumu.
 
Nachagua ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.
Kwa sababu sinunui chakula, wanakula majani/nyasi ninazolima na ninahifadhi kwa ajili ya kiangazi na ninatumia gharama ndogo.
Ukiwa mzoefu ni mradi rahisi wenye faida kubwa.
Mkuu, umenishawishi kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Nafikiri unaizungumzia "silage". Inaweza ikagharimu kiasi gani kwa mwaka kuandaa chakula cha ng'ombe watano?
 
Chasha farm hapo umepigaje ? Twende layers upande wa pili kiti moto....sababu ....project zote zina soko uhakika mzunguko utakuwa mzuri sana....chakula almost sawa sawa.....ukiweza tengeneza cha kiti koto ...na ukiweza zaidi tafuta formula ya layers....anza kuku 1000...na kitimoto majike 10....utanielewa after 2yrs
 
Ufugaji wa nguruwe unalipa sana, hasa ukipata mbegu nzuri. Maana nguruwe ukimtunza vizuri, akiwa na umri wa kuanzia miezi 8. Siyo chini ya 250,000. Hiyo inategemeana na maeneo uliyopo.
 
Nachagua ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.
Kwa sababu sinunui chakula, wanakula majani/nyasi ninazolima na ninahifadhi kwa ajili ya kiangazi na ninatumia gharama ndogo.
Ukiwa mzoefu ni mradi rahisi wenye faida kubwa.
Mkuu, unatumia mbinu gani kuhifadhi? Una mitambo ya kuchakachia ili iweze kukaa muda mrefu bila kuharibika?
 
Back
Top Bottom