Ukiachwa achika

Ukiachwa achika

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,350
Ni ngumu kuachwa hasa na mtu unaempenda. Wengine wanakuambia tumefika mwisho wa barara, gari yetu ya mapenzi haiendelei na safari. Kuna wanaotoa visingizio, unakuta miezi mitatu hamjaonana wala kuwa na maongezi ya kueleweka. Kila siku atadai yuko busy. Mmh huu u busy mbona unapata muda wa kuoga kula na kulala kama mimi bado ni wa muhimu kwako.

Awe mwanamke au mwanaume. Kama amefikia hatua hiyo, ingawa ni ngumu lakini kubali matokeo. Kumbuka yeye ni mtu mzima ana sababu zake katika maamuzi hayo.

Sasa kuna wale wa binafsi wanaotishia kunywa sumu, kulia, kujiumiza. Mpenzi wewe unafarijika kuwa nae lakini ukumbuke kuwa uwepo wako kwake si faraja tena.
 
Hayo yalikua yananipa shida hapo zamani.. Siku hizi nkiona hivo namtafuta nimuulize kulikoni.
Kama hana jibu la maana tayari naziamini hisia zangu then anakula block maisha yanaendelea
Imagine nakutana na wengi wanaohitaj kuwa nami nawakataa sababu ya huyo boya mmoja..
Nimekomaa kwakweli.. Sjpelekeshwi zama hizi
Kama unampenda kuchinja na kunyonga vyote vinaleta maumivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ngumu kuachwa hasa na mtu unaempenda. Wengine wanakuambia tumefika mwisho wa baraka, gari yetu ya mapenzi haiendelei na safari. Kuna wanaotoa visingizio, unakuta miezi mitatu hamjaonana wala kuwa na maongezi ya kueleweka. Kila siku atadai yuko busy. Mmh huu u busy mbona unapata muda wa kuoga kula na kulala kama mimi bado ni wa muhimu kwako.

Awe mwanamke au mwanaume. Kama amefikia hatua hiyo, ingawa ni ngumu lakini kubali matokeo. Kumbuka yeye ni mtu mzima ana sababu za kuchukua hatua hiyo.

Sasa kuna wale wa binafsi wanaotishia kunywa sumu, kulia, kujiumiza. Mpenzi wewe unafarijika kuwa nae lakini ukumbuke kuwa uwepo wako kwake si faraja tena kwake.
Sky Eclat vip jamaa kaishia au
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom