Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Mtu unayempenda akikuacha inauma.

Hasa pale unapokumbuka jinsi ulivyompenda na mlivyokua na furaha. Usiku huwa ni mrefu sana. Ukiwa bado huamini kama ndo mmeshaachana(umeachika) na unaona huna matumaini tena ya kumpata kama yule uliyempenda sana.
Unachoka zaidi pale unapofikiria kuanza upya.
Unabaki na mawazo na maumivu ya moyo kila siku unaona hali inazidi kuwa mbaya sana.

Au unaweza ukawa kwenye mahusiano lakini unaona unapoelekea mhh, unahisi utaachika na utaumia mno. Lakini tambua kuwa we sio wa kwanza kuachwa, wengi wameachwa na kuyashinda.

Waliyashida kwa kuzingatia haya.

Kubali kwamba umeachwa.
Imeshatokea, Jide alisema maji yakishamwagika hayazoleki.
Kubali kwamba kwa sasa ameona hufai kuwa naye.
Kama utakasirika sawa, kama utaumia kujisikia kulia sawa, nenda kajifungie ulie. Ila usitegemee vilevi kukusaidia kuepuka maumivu. Maumivu yataisha kwa muda huo wa vilevi, alafu baadaye vilevi vikiisha akilini mawazo yanarudi.

Pia usimuwekee gubu, kisasi au kumchukia ex wako, kitendo cha kufanya ivo maana yake unamkumbuka na bado hujakubali kuachwa. Bado unang’angania ulipoachwa.

Jipe muda, jiruhusu kupata muda wa maumivu ili upone haraka. Jipe muda usifanye maamuzi ya haraka.

Jichunguze kwanini uliachwa.
Kabla ya kuanza kumtupia mawe ex wako, jiangalie wewe kwanza.
Hii ni kazi ngumu, ila ina faida sana.
Je, ulitetereka kwenye mahusiano? Au ulianza kuwa mnyonge kwa mpenzi wako na ulikua humpi changamoto?

Je, kuna sehemu mlipishana? Au ulikua na kauli mbovu Kisha na mtu wa kukasirika kila muda?
Je, ulikua unamkwaza mwenzio mara kwa mara? Au ulijitahidi kumridhisha lakini hukufikia anapotaka?
Je, ulipenda kufanya asichotaka mwenzio? Au ulikua humridhishi mwanzako?
Ukipata jibu anza kufanyia kazi hicho kitu.

Kwanini?
Kama umeachwa leo sababu ya kitu fulani una uwezekano mkubwa wa kuachwa tena sababu ya kitu hiko hiko kwenye mahusiano yanayofuata. Unaweza ukapata mtu sahihi kabisa lakini ukampoteza sababu umeshindwa kujirekebisha. Na ukishajua kwanini uliachwa ni vigumu kuachwa tena kwa sababu hizo hizo.
Labda uwe hujatatua hilo tatizo lako.

Jiimarishe sehemu zingine za maisha yako.
Kama ulipanga kuanza kitu fulani anza kufanya. Kama una masomo weka nguvu kwenye masomo. Kama una kazi/ biashara weka nguvu kwenye biashara/ kazi yako. Itakusaidia kupunguza mawazo kuhusu ex wako.
.
Usijaribu kumrudisha ex wako mapema.
Ikiwa ye ndiye aliyevunja mahusiano.
Na ulijaribu kuyaokoa lakini ikashindikana, mwache aende zake.
Sababu kama amefikia hatua ya kukuacha ujue hauna kambi tena kwake kwa muda huo. Hivyo mpe muda kama naye akiona ana uhitaji wa kuwa nawe maishani mwake mtayasuluhisha na kusonga mbele. Hasa baada ya kujua ulipokosea na ukajirekebisha.

Lakini usimlazimishe mrudiane, hata kama ulimpenda vipi. Ukisema ulazimishe utaishia;
kuumizwa zaidi mana mwenzako atakua anakuchukulia poa,
utachunwa na
kutumiwa tu, ndo maana ni muhimu kujipa muda na kuanza upya ku

Tafuta mpenzi mwingine.
Usitafute mpenzi mpya ili kuepuka upweke.
Usitafute mpenzi mpya ili umringishie ex wako.
Usitafute mpenzi mpya sababu umeshindwa kuwa peke yako.
Usitafute mpenzi mpya kulipiza machungu ya kuachwa.
Usipeleke mabaya yako ya nyuma kwa mpenzi wako mpya. Huyo mpenzi mpya maana yake ni nafasi nyingine Mungu amekupatia ili kujielewa zaidi na kukua ili kufikia malengo yako ya kimahusiano.

Kumbuka mahusiano uliyokua nayo tayari yameisha, rekebisha ulipokosea na wekeza nguvu zako kwenye mahusiano mapya. Na ikitokea mmerudiana, msiishi kama zamani, bali fanyeni kama mnaanza upya na kumpa nafasi ajitetee mana yeye ndiye aliyekuacha kwanza.

Hata kama uliumizwa huko nyuma kisiwe kizuizi cha wewe kufurahia na kujitoa kwa 100% kwenye mahusiano mapya. Kama ikitokea uliyenaye hawezi kuhimili kujitoa kwako mwache aende mana atakua amepoteza dhahabu, lakini isiwe sababu ya wewe kujinyima kufurahia mahusiano.

Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 
Tatizo wengi wetu tuna wapenzi zaidi ya mmoja. Wala haiwi tatizo.
 
Mtu unayempenda akikuacha inauma.

Hasa pale unapokumbuka jinsi ulivyompenda na mlivyokua na furaha. Usiku huwa ni mrefu sana. Ukiwa bado huamini kama ndo mmeshaachana(umeachika) na unaona huna matumaini tena ya kumpata kama yule uliyempenda sana.
........umenena vyema mkuu, sasa ikitokea umeshaachwa na umekubali kusonga mbele sijui ndo kumuvu oni wanasema, then ukapata mtu mpya na mkamatch...after sometimes ex anarudi akitambaaa na machozi juu akiomba msamaha na kuhitaji kile kinachoitwa second chance, hapo tunafanyaje tunasamehe au, na vipi kuhusu mpenzi mpya tunamuachaje.....mind you ex bado unampenda kiasi cha kuweza kumsamehe......
 
Back
Top Bottom