UKAWA Wazuiwa kufanya mkutano Kigoma Mjini

Ni baada ya mkutano walioufanya Uvinza ambapo inadaiwa Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi Bw. Nyambabe kuwatukana viongozi wa kitaifa!

Nyambabe ambaye aliwekwa rumande yuko nje kwa dhamana!

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma amesema mikutano hiyo imepigwa marufuku kwa usalama wa viongozi wa Ukawa!

Source: Radio One Stereo.

Tatizo kubwa la serikali ni kuziba masikio na kujidai wao wanajua kila kitu. Katika siku za mwanzo kabisa Hayati Mwalimu aliwahi kuwapa ushauri wa msingi. Kama wangeuzingatia wala wasingekuwa kwenye shida kama hii ya leo.

Mwalimu aliwaambia "Msitumie nguvu kuwadhibiti wapinzani, waacheni tu, watakufa kifo cha kawaida tu....." Wao wakadhani sijui Mwalimu amechanganyikiwa. Ila kimsingi Mwalimu alimaanisha kadri mnavyowapa misukosuko, ndivyo wanavyokuwa maarufu zaidi. Hata kujifunza kwa watu kama Mandela hawataki!

Kama kuna mtu anajidanganya kuwa upinzani utaisha kwa kufunga mtu, hajajua bado anafanya nini, unapofunga mmoja wanazaliwa wengi kama huyo uliyemfunga. Unapomwua mmoja wanazaliwa wengi zaidi. Unapokazana kuwaambia watu wasiangalie sehemu, watu ndivyo wanavyotafuta kila upenyo kuangalia hapo! hivyo ndivyo ukweli ulivyo.

Kuna jambo moja mimi nna uhakika nalo. Kwamba Watanzania hawatakiwi kuihitaji CCM kwa sababu imefeli malengo na imewaangusha Watanzania. Na kuwa hiki kinachotokea ni sauti ya wananchi kusema hivyo! Sasa kitu ambacho sikielewi ni upuuzi wa hawa watu. Kwamba wao wanadhani kupiga mikutano marufuku kutawanusuru! Ukweli ni kuwa mabadiliko ya kweli hayako viwanjani, yako mioyoni mwa hawa walioonewa kwa muda wa kutosha! Na sidhani kama serikali inaweza kuingia mioyoni mwa wananchi kukataza wao kuichukia CCM na serikali yake!
 
Watanzania wameshaelewa nini wanahitaji, waache wazuie Mikutano, Walisema watapambana na UKAWA huko kwa Wananchi, mbona sasa wanawazuia kufanya Mikutano.?
CCM haina Dira wala muelekeo, Serikali 3 ndio inaingizwa Kaburini. RIP CCM.
 
Kiufupi naifananisha ccm na kinyesi cha mbwa vilevile mwenyekiti wa ccm ni Chief M.A Nanga aka Minus Opportunity.
 
Nape akiwa katika uwanja wa people's power huko Singida amesema Ukawa wamekwisha kufa kwa kukosa wasikilizaji katika mikutano yao!
 
Hawawezi kupambana na nguvu ya Mungu,UKAWA ni sauti ya wengi na ndiyo sauti ya Mungu

Umevurugwa wewe Sauti ya Mungu waijua????
Yani watu wengine wanaropokwa utadhani wamekatwa vichwa vile.
 
Hii habari imenifurahisha. UKAWA wanachafua hali ya hewa na utulivu wa raia.

Yaani wewe unajiona umetulia? Ni kutojua tu nakuona unaelekea kufa wewe unadhani umetulia. Una faida gani unayopata wakati wenzako wanajichotea pesa?
 
Ujamaa syndrome. Hebu define lugha ya matusi ni kitu gani ?

Ni muhimu maana kuna watu wanaamini kumwita kiongozi mwizi au fisadi wakati nikweli ni Lugha ya MATUSI dhidi ya Viongozi, hayo ni madhara yanayotokana na sera za enzi za Zidumu Fikra za Fulani...
 
Back
Top Bottom