UKAWA Wazuiwa kufanya mkutano Kigoma Mjini

Sultan_mdosse

Senior Member
Nov 24, 2013
138
195
Habari nilizopata toka kwa mmoja wa watu wangu wa nguvu kutoka mkoani Kigoma ni kwamba,Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) Wamezuiwa kufanya mkutano ambao ulipangwa kufanyika ktk kiwanja cha Mwanga Center Mkoani Kigoma,Na inasemekana ktk kiwanja hicho kulikuwa na Mapira ya Polisi kuhakikisha hakuna mkutano utaofanyika.

Ikumbukwe kwamba katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alitiwa mbaroni na jeshi la polisi ktk kijiji cha Nguruka wilaya ya Uvinza kwa tuhuma ya kumdhalilisha Raisi Jakaya Kikwete na kuachiwa huru kwa dhamana.

Nawasilisha
 
Shukrani A. Ngonyani

Verified Member
Feb 23, 2014
1,115
2,000
Nimeiona hii habari startv, nikaona kama utani vile.

Eti mkuu wa mkoa tu kwa udhaifu wa moyo wake tu kazuia mikutano ya UKAWA mkoani Tabora.

Najiuliza ni "mkono wa mtu" au nini?

Tuna safari ndefu kuelekea demokrasia ya kweli.
 
Muwazi

JF-Expert Member
May 16, 2014
355
225
Waache vurugu zao na lugha za matusi wakitaka kufanya mikutano yao sio kuendeleza fujo na matusi. Kwa hali hii hawatashinda 2015 na badala yake CCM itashinda kwa kishindo. Wao hata kama wameungana lakini hawataweza kuongoza nchi hii maana wananchi hawataki vurugu bali wanataka amani na hawawezi kuongozwa na watu wenye uchu wa madarakani.
 
kirikuu10

JF-Expert Member
May 4, 2014
249
0
Hana jeuri hiyo ukawa watafanya mkutano hapo kama kawaida hivyo visa vimekuwepo sehemu mikoa mingi na ukawa ikafanya mikutano yake.
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Sasa inakuwaje aliwaruhusu Nape na Kinana wahutubie huko Tabora?Au ndiyo ile halali la kwa CCM kwa UPINZANI haramu?Kazi tunayo.Joyce Banda uzalendo umemshinda kafuta uchaguzi na huku yaja.
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,865
1,500
Huyo Mkuu wa Mkoa anaitwa nani? Inakuwaje hawezi kusoma alama za nyakati? au ni msaka posho aina ya akina Lukuvi ...?... I wish wasaidizi wake wangemwambia ukweli tu kuwa haiwezekani kuwazuia wasifanye hiyo mikutano!!!
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
anajivunia kuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya mkoa na mkuu wa serikali mkoani. anaweza akiamua

Kisheria na kikatiba bila kujali yeye ni mwenyekiti wa nini na nini, mkuu wa mkoa hana uwezo wala mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa katika eneo lake. Mamlaka pekee ya kufanya hivyo anayo OCD wa eneo ambalo mkutano unatakiwa kufanyika, na anapaswa kutoa agizo hilo kwa maandishi siyo Runinga au Magazeti.

Kwa hiyo bado UKAWA wakitaka wanaweza kufanya mikutano yao, mpaka pale taratibu za kisheria zitakapofuatwa!
 
Sultan_mdosse

Senior Member
Nov 24, 2013
138
195
Waache vurugu zao na lugha za matusi wakitaka kufanya mikutano yao sio kuendeleza fujo na matusi. Kwa hali hii hawatashinda 2015 na badala yake CCM itashinda kwa kishindo. Wao hata kama wameungana lakini hawataweza kuongoza nchi hii maana wananchi hawataki vurugu bali wanataka amani na hawawezi kuongozwa na watu wenye uchu wa madarakani.
kweli kabisa mkuu,kinachowapunguzia credit wapinzani ni kutumia lugha zisizo na staa hasa kwa viongozi wetu.Hata walipofanya mkutano wao hapa shy mjini ktk viwanja vya shelkom lugha zisizo na staa zilitumika ambazo kwa kiasi fulani zina arouse animosity.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,408
2,000
Sasa Ni Lugha Gani Zilitamkwa Na MOSENA NYAMBABE Wakati hata Mkutano Hawajafanya !!!
 
kirikuu10

JF-Expert Member
May 4, 2014
249
0
kweli kabisa mkuu,kinachowapunguzia credit wapinzani ni kutumia lugha zisizo na staa hasa kwa viongozi wetu.Hata walipofanya mkutano wao hapa shy mjini ktk viwanja vya shelkom lugha zisizo na staa zilitumika ambazo kwa kiasi fulani zina arouse animosity.
Hahahaaaaaaa! Mh! Kazi mnayo ccm.tena sio ndogo.
 
Muwazi

JF-Expert Member
May 16, 2014
355
225
kweli kabisa mkuu,kinachowapunguzia credit wapinzani ni kutumia lugha zisizo na staa hasa kwa viongozi wetu.Hata walipofanya mkutano wao hapa shy mjini ktk viwanja vya shelkom lugha zisizo na staa zilitumika ambazo kwa kiasi fulani zina arouse animosity.

2015 wataikubali CCM kuwa ndo baba lao. Wao matusi yao na lugha za kejeli hazitawasaidia. Hawana adabu maana hata hawamthamini hata rais wa nchi hii. Matusi mpaka kwa Rais ni sawa na mtoto kumtukana baba yake. Wamuulize Lyatonga Mrema alipomuomba Marehemu Nyerere ushauri kuhusu kugombea urais mwaka 1995 na kumwambia aache na badala yake akamwambia aende agombee ubunge na akakataa. Kilichofuata ni kwamba alipigwa chini hadi leo hana sauti tena wala ndoto za urais.
 
MPANDA Jr

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,298
1,195
Mkuu wa mkoa wa Dodoma alishawah kuzuia pia mikutano ya CHADEMA wakati bunge linaendelea kwa maelezo kwamba polis hawatoshi, lakin tulipiga mikutano kama kawaida... Tabora amkeni
 
aye

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
2,094
2,000
mkuu ni tabora au kigoma naona heading na habari inachanganya hasa tusiyoiona hiyo habari startv
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom