UKAWA Wavunjika Rasmi

UKAWA Wavunjika Rasmi

mkuu lizaboni jahazi la ukawa lilianza kuzama baada ya kukalibsha hili dubwana
m2mbwi wa ukawa.jpg
 
Nilikuwa najiuliza sana kwa nini Madelu ana wafyatua sana makada wa chama na wake wa makada wenzie sasa nimepata jibu. Lizaboni jumapili kama hii SAA 7.20am tayari kesha amka na kupost Uzi mrefu wa kutunga,majungu na uzàndiki alioufikiri usiku mzima unadhani ana muda kweli wa kumpa mama yeyoo hi kitu hii?
Hapo mama wa watu ni full kiu na inabidi watu wamsaidie. Ukuda una gharama zake, yeye acha ajifanye anatumikia chama na wenzake watumikie mamlaka ya nyumbani kwake
Mkuu ni kweli madelu anawamaliza vijana wote wa lumumba, kuanzia kina shonza na familia za hao kina lizaboni
 
Umeishia hadmawazo wegamba yawezekana hunaata mwelekeo wamaisha yako ,UKAWA itabaki imala tu daima.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni umoja ulioasisiwa na vyama vinne wakati wa Bunge Maalum la Katiba. Vyama hivyo ni CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na NLD. Baadaye vyama hivi viliwekeana makubaliano ya kushirikiana kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo walikubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia nafasi ya Urais hadi Udiwani.

Hata hivyo, figisu figisu zilianza wakati wa uteuzi wa wagombea. Kwa upande wa wagombea Udiwani, vyama hivyo vilishindwa kuafikiana kusimamisha mgombea mmoja kwenye kata nyingi. Mwisho wa siku wakajikuta vyama vyote vinasimamisha wagombea hali ambayo ilichangia anguko lao. Hali hiyo pia iliendelea kwenye nafasi ya Ubunge. Majimbo kadhaa walishindwa kuafikiana. Mfano wa majimbo hayo ni Segerea ambapo CHADEMA na CUF walisimamisha wagombea. Hata hivyo, kura walizopata wagombea hao wawili zilizidi kura ambazo alipata mgombea wa CCM ambaye alitangazwa mshindi. Kule Masasi, Mwenyekiti wa NLD, Emmanuel Makaidi, Mungu amrehemu, alishindwa kupewa hadhi yake ambapo CUF pia walisimamisha mgombea. Maskini ya Rabbi, mzee Makaidi akapata kiharusi na shinikizo la damu na kupelekea kifo chake. Baada ya uchaguzi mdogo, UKAWA wakaangukia pua tena.

Kwa upande wa mgombea Urais, hapo ndipo majanga na kifo cha UKAWA kilipoanzia. Vyama vyote vilikubaliana kuteua mgombea Urais. Baada ya hapo, wagombea hao walipaswa kushindanishwa ili kumpata mgombea mmoja. Waliopaswa kuwa Wagombea Urais wa vyama vya CHADEMA, NCCR na CUF ambao ni Dr Slaa, Dr Kahangwa na Prof Lipumba wakafanya kikao cha falagha ambapo walikubaliana kumuachia mmojawapo kwenye nafasi hiyo. Taarifa za awali zilidai kuwa ni Dr Slaa ndiye aliyependekezwa na wenzake.

Hata hivyo, uroho, tamaa na ulafi wa Freeman Mbowe ulisababisha makubaliano hayo yavunjike. Baada ya kununuliwa kwa shilingi bilioni 10 na Fisadi Lowasa, hatimaye kwa nguvu CHADEMA wakamteua Lowasa kuwa mgombea Urais ambaye pia aliwakilisha UKAWA. Ni kutokana na maamuzi hayo ya kilafi ndipo Lipumba na Dr Slaa walipoamua kubwaga manyanga.

Uchaguzi Mkuu umefanyika na UKAWA wameangukia pua tofauti na matarajio yao ingawa wanajinasibu kuwa wameongeza idadi ya wabunge na madiwani. Wamesahau kuwa lengo la vyama vya siasa ni kushika dola.

Ni zaidi ya miezi minne sasa tangu vikao vya kawaida vya UKAWA vifanyike licha ya mambo mengi kutokea ambayo yangelazimu kufanyika kwa vikao hivyo. Hata baada ya Uchaguzi, hawajafanya vikao vya Tathmini kubaini wapi waliteleza na nini kifanyike. Badala yake tunasikia fisadi Lowasa anatangaza kugombea tena 2020 as if yeye ndo CHADEMA na yeye ndo UKAWA. Hata jitihada za kisiasa kule visiwani wameachiwa CUF pekee na hakuna kikao hata kimoja cha UKAWA kimefanyika kujadili nini cha kufanya. Badala yake tumeshuhudia maamuzi yakifanywa na CUF pekee ingawa awali walituaminisha kuwa Maalim Seif anawakilisha UKAWA kwa upande wa Zanzibar. Vyama vya NLD na NCCR tayari vimejitoa kwenye umoja huo baada ya kukosa mawasiliano na vyama vingine.

James Mbatia ameshaandika barua rasmi ya kujitoa kwenye umoja huo. Maalim Seif naye ameshamueleza Lowasa kuwa haoni faida ya kujiita mwana UKAWA ilhali umoja huo haupo Zanzibar. Kwa hali hiyo, Maalim Seif amewaambia CHADEMA kuwa WALIPO SASA NI SAWA NA WALIPOKUWA KABLA YA BUNGE MAALUM LA KATIBA. Tafsiri ya kauli hii ya Maalim ni kwamba hakuna cha UKAWA tena.

Ilishatabiriwa kuwa UKAWA itakufa kifo cha mende. Ndivyo ilivyotokea. Kifo cha UKAWA kimekosa kilio.
Mkuu nakubaliana nawe kwani kwetu chadema taendelea kumlau mbowe
 
mwenzao aliona kiama mapema akasepa fasta
lipUMBA NA UKAWA.jpg
 
baada ya kufukuzwa ccm kwa kosa la kucheza rafu nyng, ikiwemo ufisadi, ukawa wao wakamsajili huyohuyo MCHEZA RAFU
lowasa mcheza rafu.jpg
 
Wanafunzi Shule ya
msingi Bumira,
Dodoma hatarini
kupatwa na magonjwa
ya mlipuko kutokana na
kujisaidia vichakani kwa
kukosa vyoo
#HabariLEO





Wanafunzi zaidi ya elfu
2 shule ya msingi
Nyakanazi, Kagera
wanasomea chini ya
miti kwa kukosa
vyumba vya madarasa
#GazetiMWANANCHI
#Feb21






Hapa Kazi Tu
 
mi nadhani kunapokuwepo na upinzani imara ni jambo jema kwa maendeleo ya nchi...cha kushangaza ni pale mtu anapofurahia upinzani legelege...kwa faida ya nani!!!
 
Teuzi za maDCs wapya zikishafanyika, cjui kama humu ndani habari za umbea khs UKAWA zitakuwepo tena....???
 
Uhusiano wako na aliyekutuma utavufunjika, lakin siyo Ukawa
 
Ukawa uliwaumiza sana ccm. Hawakutarajia. Walikuwa wakitabiri kila diku eti ukawa hawafika uchaguxi mkuu. Leo ukawa imekufa. Ukawa itakufaje wakati wanaunda kambi moja ya upinzani bungeni? Au kila chsmsvsasa kina kambi yake?
Umesema Mbatia kaandika barua ya kujitoa ukawa bila hsta udhibitisho?
Stori yako hata haishikani vixuri.
Hata hivyo tunajua hii ndiyo kazi inayokuweka mjini! Bila kuposti prooaganda hapa watoto wako hawaendi choo! So keep it up!
 
Bila siasa safi na upinzani imara inakuwa ngumu...japo angalau JPM ameonyesha njia tumuunge mkono.

Hilo ndio tatizo kubwa la watanzania, hatujui siasa ni nini hatimayake tuna shangilia siasa kama tunavyo shangilia yanga na simba. Unaona mtu kaleta mada ndefu ya kisiasa lakini watu badala ya kujibu kisiasa wanaanza kushambuliana kwa matusi.
Bila upinzani hakuna maendeleo, tunarudi tena nyuma enzi za Marhemu Nyerere.
Kinachotakiwa tuwe na wapinzani imara, wanasiasa imara lakini mwaafrika anacho angalia kwanza ni maslaha yake na tumbo lake.
Mh. Raisi amefanya mambo makubwa sana ambayo hayajawahi kufanyika na hata hivyo kuna mapungufu na kuna changa moto. Ndio hapo tunahitaji kujadili kisiasa badala ya matusi na ukejeli.
 
Teuzi za maDCs wapya zikishafanyika, cjui kama humu ndani habari za umbea khs UKAWA zitakuwepo tena....???
Kwani kuna uhusiano gani baina ya teuzi na mada za jamiiforums?
 
Uhai na uimara wa chama cha siasa ni ofisi ya katibu mkuu. CCM ya Y.Makamba ni tofauti Sana na ya Kinana. Mbowe alishindwa kuelewa umuhimu wa Dr Slaa kama GS wa chama,alifikiri CDM ni kama danguro,linajiendea tu. Dr Slaa alikuwa ndo CDM,think tank ya chama,msimamizi wa shughuli na nidhamu ya chama. Leo hii hakuna nidhamu,kila mtu boss,hakuna ratiba ya vikao,mpango kazi,hakuna operesheni yoyote iliyobuniwa. Enzi ya Dr Slaa ilikuwa patashika....
 
Back
Top Bottom