UKAWA Wavunjika Rasmi

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni umoja ulioasisiwa na vyama vinne wakati wa Bunge Maalum la Katiba. Vyama hivyo ni CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na NLD. Baadaye vyama hivi viliwekeana makubaliano ya kushirikiana kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo walikubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia nafasi ya Urais hadi Udiwani.

Hata hivyo, figisu figisu zilianza wakati wa uteuzi wa wagombea. Kwa upande wa wagombea Udiwani, vyama hivyo vilishindwa kuafikiana kusimamisha mgombea mmoja kwenye kata nyingi. Mwisho wa siku wakajikuta vyama vyote vinasimamisha wagombea hali ambayo ilichangia anguko lao. Hali hiyo pia iliendelea kwenye nafasi ya Ubunge. Majimbo kadhaa walishindwa kuafikiana. Mfano wa majimbo hayo ni Segerea ambapo CHADEMA na CUF walisimamisha wagombea. Hata hivyo, kura walizopata wagombea hao wawili zilizidi kura ambazo alipata mgombea wa CCM ambaye alitangazwa mshindi. Kule Masasi, Mwenyekiti wa NLD, Emmanuel Makaidi, Mungu amrehemu, alishindwa kupewa hadhi yake ambapo CUF pia walisimamisha mgombea. Maskini ya Rabbi, mzee Makaidi akapata kiharusi na shinikizo la damu na kupelekea kifo chake. Baada ya uchaguzi mdogo, UKAWA wakaangukia pua tena.

Kwa upande wa mgombea Urais, hapo ndipo majanga na kifo cha UKAWA kilipoanzia. Vyama vyote vilikubaliana kuteua mgombea Urais. Baada ya hapo, wagombea hao walipaswa kushindanishwa ili kumpata mgombea mmoja. Waliopaswa kuwa Wagombea Urais wa vyama vya CHADEMA, NCCR na CUF ambao ni Dr Slaa, Dr Kahangwa na Prof Lipumba wakafanya kikao cha falagha ambapo walikubaliana kumuachia mmojawapo kwenye nafasi hiyo. Taarifa za awali zilidai kuwa ni Dr Slaa ndiye aliyependekezwa na wenzake.

Hata hivyo, uroho, tamaa na ulafi wa Freeman Mbowe ulisababisha makubaliano hayo yavunjike. Baada ya kununuliwa kwa shilingi bilioni 10 na Fisadi Lowasa, hatimaye kwa nguvu CHADEMA wakamteua Lowasa kuwa mgombea Urais ambaye pia aliwakilisha UKAWA. Ni kutokana na maamuzi hayo ya kilafi ndipo Lipumba na Dr Slaa walipoamua kubwaga manyanga.

Uchaguzi Mkuu umefanyika na UKAWA wameangukia pua tofauti na matarajio yao ingawa wanajinasibu kuwa wameongeza idadi ya wabunge na madiwani. Wamesahau kuwa lengo la vyama vya siasa ni kushika dola.

Ni zaidi ya miezi minne sasa tangu vikao vya kawaida vya UKAWA vifanyike licha ya mambo mengi kutokea ambayo yangelazimu kufanyika kwa vikao hivyo. Hata baada ya Uchaguzi, hawajafanya vikao vya Tathmini kubaini wapi waliteleza na nini kifanyike. Badala yake tunasikia fisadi Lowasa anatangaza kugombea tena 2020 as if yeye ndo CHADEMA na yeye ndo UKAWA. Hata jitihada za kisiasa kule visiwani wameachiwa CUF pekee na hakuna kikao hata kimoja cha UKAWA kimefanyika kujadili nini cha kufanya. Badala yake tumeshuhudia maamuzi yakifanywa na CUF pekee ingawa awali walituaminisha kuwa Maalim Seif anawakilisha UKAWA kwa upande wa Zanzibar. Vyama vya NLD na NCCR tayari vimejitoa kwenye umoja huo baada ya kukosa mawasiliano na vyama vingine.

James Mbatia ameshaandika barua rasmi ya kujitoa kwenye umoja huo. Maalim Seif naye ameshamueleza Lowasa kuwa haoni faida ya kujiita mwana UKAWA ilhali umoja huo haupo Zanzibar. Kwa hali hiyo, Maalim Seif amewaambia CHADEMA kuwa WALIPO SASA NI SAWA NA WALIPOKUWA KABLA YA BUNGE MAALUM LA KATIBA. Tafsiri ya kauli hii ya Maalim ni kwamba hakuna cha UKAWA tena.

Ilishatabiriwa kuwa UKAWA itakufa kifo cha mende. Ndivyo ilivyotokea. Kifo cha UKAWA kimekosa kilio.
 
Ni hakika Babu Duni pia anazidi kukoleza moto kwani chadema na Lowassa hawajamlipa baki ya 150 m...na Siif keshavuta 350 m anaenda matibabu India na Oman vijana Cuf wamenuna kwanini Seif anashiri mikutano na CCM pekeyake bila timu.Hakika kwa sasa ushirika uliyobaki ni kati ya Seif na Lowassa binafsi na kitaasisi kama ukawa kwa makusudi maalum.....ama kweli "ajizi nyumba ya njaa"
 
Niliwahi kuuliza humu kama kuna umuhimu wowote wa kuendelea kuwa na UKAWA hasa ikisingatiwa muundo na malengo ya Awali ya UKAWA yaliwekwa pembeni ??
 
CCM ni Mpango wa Mungu na Magufuli ni mpango wa Mungu. UKAWA wamekuwa kama wajenzi wa Mnara wa Babeli
 
Ukawa ni genge la matapeli tu,wametapeliana ruzuku yote imekwenda chadema
Nccr na cuf bara vimekufa,Nld imefutika kabisa
 
cuf ni wajinga duniani pamoja na wafuasi wao kujiunga na chama cha wajinga wenzao chadema
Kuna msemo unasema muunganiko wa wajinga huwapeleka njia isiyo sahihi au ukatengeneza sumu kali dhidi yao....hakika CUF na Chadema wametengeneza anguko lao wenyewe.
 
We mngoni ushavimbiwa pitiku na maboga unakuja kubwabwaja huku .

Biashara yako ya kuendesha boda boda imedoda na hii mvua umebaki kuiwaza ukawa.
 
Back
Top Bottom