UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

CCM ni chama changu na ni chama bora Tanzania. Si haya mavyama ya kiliberali ambayo viongozi wake karibu wote ni maliberali
Hakika mkuu ukawa ni wahuni wa kawaida kabisa kama ccm wangekuwa kama ukawa tusingekuwa na kitu kinaitwa taifa.
 
Sure mkuu tena laana hii ya kutukana waasisi nayo imewaandama kweli hawatabaki salama hata iweje huwezi kumtukana matusi yote yale nyerer halafu ukabaki salama kamwe haitokei ukawa hawana pakutokea.
Dah! Sijui Lissu na Jusa wataficha wapi nyuso zao. Natabiri kuwa Lissu atarudi tena Milembe
 
Hakika mkuu ukawa ni wahuni wa kawaida kabisa kama ccm wangekuwa kama ukawa tusingekuwa na kitu kinaitwa taifa.
Hakika Mkuu. CCM imejaaliwa kuwa na waru wenye hekima na busara
 
Inatisha sana na inauma kweli. Sasa si bora warudi tu kwa wake na waume zao. Tatizo kubwa la wana UKAWA ni kuwa wengi wao hawajaoa wala kuolewa. Ndo maana wengi wamebaki huko Dom wanahangaika
Okeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Sasa naipata mnyiki ya wao kutoka bungeni na kushinwa kurudi makwao pamoja na ukata walionao kumbe hilo nalo ni jambo jingine kweli ukawa ni janga sugu la wazawa.
 
... UKAWA walipoondoka Bungeni, walitarajia kuwa, Bunge hilo litavunjwa kutokana na wao kutokuwepo. Matarajio yao ni kuwa, Bunge likiahirishwa, azma yao ya kukwamisha mchakato huo yatakuwa yametimia. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Wabunge waliobaki wengi wao wakiwa ni wa CCM wanaendelea na mjadala na kwa takriban wiki mbili sasa,...
Mkuu, kwani haujui kwamba mjadala ukiendelea tu bila kupitishwa kunakuwa hakuna katiba hapo? Au ukiona wabunge wanachangia wewe unadhani mambo yanakwenda? Unadhani Sitta ni mjinga hadi aende kumbembeleza Maalim Seif? Au unadhani amekuwa mjinga kuacha kuhitimisha mjadala? Nadhani kuna vitu hauvijui, ndio maana unadhani mambo yanaenda shwari. Mjadala kuendelea sio tatizo, tatizo lipo kwenye kupitisha hayo waliyokuwa 'wanaendelea' kuyajadili !!! Ungejua hayo, usingeanzisha thread hii
 
Okeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Sasa naipata mnyiki ya wao kutoka bungeni na kushinwa kurudi makwao pamoja na ukata walionao kumbe hilo nalo ni jambo jingine kweli ukawa ni janga sugu la wazawa.
Hakika Mkuu. Na kwa huo ukata walionao, kuna wabunge wataendeleza uliberali wao
 
Dah! Sijui Lissu na Jusa wataficha wapi nyuso zao. Natabiri kuwa Lissu atarudi tena Milembe
Lakini hawa watu mishipa ya aibu hawana Lisu sote tunajua hayuko sawa na huyo jusa mengine aliyofanya anajua yeye na mungu wake lakini ni matendo ya aibu sana lakini vyovyote itakavyokuwa wamejikaanga tena watukome kukaa wanakwenda kupotosha watu.
 
Mkuu, kwani haujui kwamba mjadala ukiendelea tu bila kupitishwa kunakuwa hakuna katiba hapo? Au ukiona wabunge wanachangia wewe unadhani mambo yanakwenda? Unadhani Sitta ni mjinga hadi aende kumbembeleza Maalim Seif? Au unadhani amekuwa mjinga kuacha kuhitimisha mjadala? Nadhani kuna vitu hauvijui, ndio maana unadhani mambo yanaenda shwari. Mjadala kuendelea sio tatizo, tatizo lipo kwenye kupitisha hayo waliyokuwa 'wanaendelea' kuyajadili !!! Ungejua hayo, usingeanzisha thread hii
Mkuu, hilo nalijua fika na kumbuka kuwa maamuzi ya kujadili tu bila ya kufanya maamuzi yalitolewa tarehe 3 Aprili 2014 yaani siku 13 kabla UKAWA hawajaondola. Hivyo ni utaratibu tu wa bunge maalum na si kwa sababu ya UKAWA.
 
Utafanikiwa kuwadanganya watu kwa muda mfupi, lakini si muda wote, kama unahisi kikwete anaaminika na taifa hili kuliko UKAWA, subiri elimu ianze kutolewa, hapo ndipo utakapojua UKAWA ni nani, kikwete ni nani na wananchi wanataka nini. Unajitahidi kupiga propanda, kazana, watakuelewa wajinga wasio na uelewa.
 
Hakika Mkuu. Na kwa huo ukata walionao, kuna wabunge wataendeleza uliberali wao
Kabisa kabisa,
Namhurumia sana mjumbe mmoja kutoka chuo kikuu mzumbe ambaye ni mdogo kuliko wajumbe wote lakini matendo anayofanya nikiyasema ntapigwa ban bure lakini hasara kabisa ukawa wanaharibu watoto wa watu.
 
Lakini hawa watu mishipa ya aibu hawana Lisu sote tunajua hayuko sawa na huyo jusa mengine aliyofanya anajua yeye na mungu wake lakini ni matendo ya aibu sana lakini vyovyote itakavyokuwa wamejikaanga tena watukome kukaa wanakwenda kupotosha watu.
Hakika Mkuu, kuna mbunge alihoji sana kwa nini Jussa hajaoa. Kuna siri nzito juu ya hilo
 
CCM ni chama changu na ni chama bora Tanzania. Si haya mavyama ya kiliberali ambayo viongozi wake karibu wote ni maliberali

Kwenye uliberali hata mabwana zako ccm ndo vinara na uteja pia kuangamiza taifa wanaongoza. Rejea matukio ya hko China na wafadhili ni maccm. 2nata serikali MOJA na c hii sera ya sasa. Punguza kujam.. kila mara. Pa mdidi hapo.
 
Kabisa kabisa,
Namhurumia sana mjumbe mmoja kutoka chuo kikuu mzumbe ambaye ni mdogo kuliko wajumbe wote lakini matendo anayofanya nikiyasema ntapigwa ban bure lakini hasara kabisa ukawa wanaharibu watoto wa watu.
Ni kweli Mkuu. Si yule mtoto wa marehemu? Hakika matendo anayofanya mpaka anatia aibu. Alianza na Mwenyekiti wa chama fulani na sasa nasikia anadandia watu hovyo baada ya kutelekezwa na Mwenyekiti huyo. Hakika ni aibu kuona kijana mdogo kama yule tena ni mwanafunzi wa chuo kikuu anajiingiza mwenye mambo yasiyorandana na haiba yake
 
Utafanikiwa kuwadanganya watu kwa muda mfupi, lakini si muda wote, kama unahisi kikwete anaaminika na taifa hili kuliko UKAWA, subiri elimu ianze kutolewa, hapo ndipo utakapojua UKAWA ni nani, kikwete ni nani na wananchi wanataka nini. Unajitahidi kupiga propanda, kazana, watakuelewa wajinga wasio na uelewa.
Hujitambui wewe elimu zimeanza kutolewa tangu nchi hii haijapata uhuru watu wako shule za msingi,sekondari na vyuo mbalimbali wewe unalenga elimu gani.

Kwanza ukawa nani wa kutoa elimu pengine useme chuki lakini kama katibu wa ukawa ndiyo huyu bure kabisa.
 
Kwenye uliberali hata mabwana zako ccm ndo vinara na uteja pia kuangamiza taifa wanaongoza. Rejea matukio ya hko China na wafadhili ni maccm. 2nata serikali MOJA na c hii sera ya sasa. Punguza kujam.. kila mara. Pa mdidi hapo.
He! Naona umebadili goal post. Umehama kwenye serikali tatu sasa unakuja kwenye serikali moja. Taratibu utaanza kuimba wimbo wa CCM. hakika utaipenda tu CCM
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa tarehe 17 Aprili 2014, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanaojiita kwa jina la UKAWA, walitoka Bungeni Mjini Dodoma wakati wa mjadala wa Rasimu ya Katiba katika sura ya Kwanza na ya Sita kwa madai kuwa wamechoshwa na CCM kutumia uwingi wao kushinikiza muundo wa serikali mbili na kuhamasisha makundi ya kijamii wakiwemo waumini kususia muundo wa muungano wa serikali tatu. Wakati wanatoka, walisema kuwa wanaenda kuishtaki CCM kwa wananchi.

Wadau, wakati UKAWA wanapanga kwenda kuishtaki CCM kwa wananchi, CCM tayari ipo kwa wananchi ikiwaeleza bayana wananchi sababu za chama kupendeke
za muundo wa muungano wa serikali mbili huku ikipinga kwa nguvu muungano wa serikali tatu. Tumemuona Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akifanya ziara za kichama huko Kigoma na mikoa ya kanda ya Ziwa. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umeratibu na kuendesha matembezi ya bodaboda katika mikoa kadhaa nchini na ujumbe katika matembezi hayo ni kuuenzi muungano ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume. Katika ziara zote hizo, wananchi wameonekana kuelewa na kuwashangaa wale wanaotaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu.

Wadau, UKAWA walipoondoka Bungeni, walitarajia kuwa, Bunge hilo litavunjwa kutokana na wao kutokuwepo. Matarajio yao ni kuwa, Bunge likiahirishwa, azma yao ya kukwamisha mchakato huo yatakuwa yametimia. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Wabunge waliobaki wengi wao wakiwa ni wa CCM wanaendelea na mjadala na kwa takriban wiki mbili sasa, CCM wamepata muda wa kutosha wa kusema yale yaliyo dhihiri huku wananchi wengi wakisikiliza kupitia Runinga, Radio na kusoma kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao huu pendwa wa JF. Hakika wabunge wengi waliopata nafasi ya kuongea wamemwaga nondo za uhakika zilizowashawishi wananchi huku wakiendeleza vijembe vile vile vilivyowakimbiza UKAWA. Nina hakika kuwa wanavipata vijembe hivyo huko huko waliko. Hakika kwa hili, UKAWA wamepigwa bao la kisigino na wananchi wanaendelea kuwalaani katika kona zote za nchi.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, zilisikika taarifa kuwa wamechukua posho zote na kujongomea. Hakika kashfa hii imewachafua sana na hawatakuja kusafishika katu. Watanzania wana hasira nao sana na hakika wasitarajie kuungwa mkono na wananchi wengi. Ingawa jitihada zimefanyika za kuwasafisha na kashfa hiyo kupitia Gazeti la Mwananchi, ukweli ni kwamba wananchi wengi wameamini kuwa wabunge hao wamechukua posho na kutokomea. Hilo ni doa kuu ambalo haliwezi kuondolewa kwa Omo wala Aerial.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataanzisha maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia siku ya pili baada ya kuondoka kwao. Hata hivyo, walipigwa stop hadi tarehe 30 Aprili ndipo watakapoanza kufanya mikutano ya hadhara na si maandamano tena. Tunajua kuwa wakati huo Bunge Maalum litakuwa limesitishwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi watakuwa wanajiandaa na vikao vya Bunge la Bajeti. Hawa UKAWA wataendelea vipi kuwa na mshikamano ilhali wabunge watakuwa busy na bunge la bajeti? Hakika hili ni bao jingine la kisigino. Kwa sasa wamekalishwa chini kama bondia aliyepigwa na mpinzani wake huku akihema asijue la kufanya. Wakati wao wataanza mikutano ya katiba, wananchi watakuwa wameshahamishia mawazo yao kwenye Bunge la Bajeti huku wakisubiri kwa hamu kusikia ni nini serikali itafanya juu yao. Hakika kati ya bajeti na Katiba, ni wazi kuwa suala la bajeti ndilo hugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na hivyo ni vigumu kwa UKAWA kupata watu wa kuwaunga mkono.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataungwa Mkono na wabunge wengi wa kundi la 201. Hata hivyo siku moja tu baada ya kuondoka kwao, baadhi ya wabunge ambao waliondoka pamoja nao akiwemo Mwalimu Ezekiel Oluoch, walirejea Bungeni huku wakiwakana na kuwananga UKAWA. Hakika hili ni pigo jingine. Imekuwa ni fedheha kwao na sasa wamekuwa mabubu kwa vile hawana avenue ya kusemea.

Wadau, baada tu ya UKAWA kuondoka, kuna shirika moja limejifanya kuendesha utafiti ili kujua mtizamo wa wananchi juu ya mijadala bungeni. Eti katika utafiti huo, kwamba Wazanzibari wengi wanaunga mkono muundo wa serikali tatu kama ilivyo kwa bara. Mbaya zaidi, wakamuita mzee Warioba ili atetee hoja hiyo. Hakika hii ni fedheha kubwa na imedhihirisha ni kwa namna gani UKAWA wametepeta. Badala ya kumuacha mzee wa watu augulie madongo anayopewa bungeni, wao wanazidi kumdhalilisha. Mbaya zaidi, Warioba akajifanya kukemea lugha zinazotolewa bungeni asi if yeye ni Presidaa.

Wadau, Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa Nchi anatarajia kuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Mei Mosi yaani siku moja tu baada ya UKAWA kuanza mikutano yao. Ingawa suala la katiba si moja ya ajenda ya sherehe hizo, ni wazi kuwa Mheshimiwa Rais anatumia japo muda kidogo kuelezea juu ya mchakato huo. Hakika nitamshangaa sana kama hatagusia hilo. Katika hotuma hiyo, ni wazi kuwa Rais Kikwete atasimamia msimamo wake ule ule alioutoa Bungeni tarehe 21 Machi 2014 wakati akilizindua bunge maalum. Hotuba hiyo ya JK itazidi kuwatokomeza kabisa UKAWA na kwa vile wananchi wengi watasikiliza hotuba hiyo, ni wazi kuwa hata UKAWA watazunguka nchi nzima, hawatabadili fikra za wananchi. Hili ni pigo jingine kwa UKAWA.

Wadau, yapo mengi ila kwa hayo niliyoyasema, ni wazi kuwa UKAWA wamelikoroga na lazima walinywe. Hakika wamepigwa bao la kisigino huku wakibaki hawana cha kufanya.

Kwanza kabisa nikupe pole sana kwa kuwadanganya wananchi kwamba ukawa walichukua posho zote na hapo hapo unasema walirudi tena kuchukua posho sasa unajichanganya mwenyewe.kama walichukua posho zote walikuja kufanya nini tena bungeni?

Swala la kuzuia mikutano yao hilo liko wazi kwamba ukawa wako sahihi kwa kile wanachokisimamia ndio maana ccm inaogopa na kulitumia vibaya jeshi la police wakizani watanzania ni vibofu kumbe mlango wa nyuma mnajimaliza wenyewe pole pole.

Kumbuka kwa sasa kila mtu anafanya maombi maoni ya tume yapite ya serikali tatu.wewe kwa ushabiki unafanya kinyume na maombi hayo adhabu yako utaipata hapahapa duniani wala hilo halina ubishi.

Sasa nakwambia mlivyowazuia ukawa ndo mnawapa nguvu zaidi kujipanga huku wakisubiri sherehe za muungano zipite wamjibu rais kwa hoja juu ya maoni ya tume.hamtaweza kuzuia huu mchakato labda dunia ife.

Tarehe 30 April ni kesho kutwa tu.mikutano itafanyika na hoja kama zilivyotolewa na warioba zitatolewa hivyo basi usione kama wamenyamazishwa bali sauti kuu itatokea na wananchi tumeamua tutawachangia pesa ili mchakato ufike maeneo yote nchi nzima.

Mwisho nawapongeza ukawa kwa kusimamia maoni ya wananchi na kutoka nje ya bunge ili kutokuwa sehemu ya interahamwe ambao kazi yao ni kupora pesa za walipa kodi kwa kisingizio cha kuandika katiba mpya wakati wanaandika katiba ya ccm.

Mungu mbariki warioba, wabariki ukawa, msamehe Lizaboni kwa kuwa anatetea ufisadi alio nao asiumbuke, ibariki Tanzania.
 
Kwenye uliberali hata mabwana zako ccm ndo vinara na uteja pia kuangamiza taifa wanaongoza. Rejea matukio ya hko China na wafadhili ni maccm. 2nata serikali MOJA na c hii sera ya sasa. Punguza kujam.. kila mara. Pa mdidi hapo.
Hapa unalenga mabwana zako wepi waliokuacha au wale ambao bado unaishi nao nyoosha maelezo kwanza tukuelewe! Jipambanue vema.
 
Hujitambui wewe elimu zimeanza kutolewa tangu nchi hii haijapata uhuru watu wako shule za msingi,sekondari na vyuo mbalimbali wewe unalenga elimu gani.

Kwanza ukawa nani wa kutoa elimu pengine useme chuki lakini kama katibu wa ukawa ndiyo huyu bure kabisa.
Huyu naye awe katibu wa UKAWA? Kanisa limemshinda, familia imemshinda, chama kimemshinda na sasa UKAWA utamshinda
 
Kwanza kabisa nikupe pole sana kwa kuwadanganya wananchi kwamba ukawa walichukua posho zote na hapo hapo unasema walirudi tena kuchukua posho sasa unajichanganya mwenyewe.kama walichukua posho zote walikuja kufanya nini tena bungeni?

Swala la kuzuia mikutano yao hilo liko wazi kwamba ukawa wako sahihi kwa kile wanachokisimamia ndio maana ccm inaogopa na kulitumia vibaya jeshi la police wakizani watanzania ni vibofu kumbe mlango wa nyuma mnajimaliza wenyewe pole pole.

Kumbuka kwa sasa kila mtu anafanya maombi maoni ya tume yapite ya serikali tatu.wewe kwa ushabiki unafanya kinyume na maombi hayo adhabu yako utaipata hapahapa duniani wala hilo halina ubishi.

Sasa nakwambia mlivyowazuia ukawa ndo mnawapa nguvu zaidi kujipanga huku wakisubiri sherehe za muungano zipite wamjibu rais kwa hoja juu ya maoni ya tume.hamtaweza kuzuia huu mchakato labda dunia ife.

Tarehe 30 April ni kesho kutwa tu.mikutano itafanyika na hoja kama zilivyotolewa na warioba zitatolewa hivyo basi usione kama wamenyamazishwa bali sauti kuu itatokea na wananchi tumeamua tutawachangia pesa ili mchakato ufike maeneo yote nchi nzima.

Mwisho nawapongeza ukawa kwa kusimamia maoni ya wananchi na kutoka nje ya bunge ili kutokuwa sehemu ya interahamwe ambao kazi yao ni kupora pesa za walipa kodi kwa kisingizio cha kuandika katiba mpya wakati wanaandika katiba ya ccm.

Mungu mbariki warioba, wabariki ukawa, msamehe Lizaboni kwa kuwa anatetea ufisadi alio nao asiumbuke, ibariki Tanzania.
Lengo la ukawa walitaka kuchukua pesa bila kufanya kazi tena walitaka kuchukua mara mbili mwigulu kawastukia sasa wanahangaika kama ndege juu ya mti uhuni huu tulijua utakuwa na mwisho ,mwisho wenyewe ndiyo huu watakoma.
 
No no no no no no no! Kwa sasa bunge linaendeshwa kwa hoja za ushawishi wakati ukawa walipokuwepo bunge lilikuwa linaendeshwa kwa matusi na kejeli yaliyokuwa yanasababishwa na Lisu pamoja na wenzake.

Usiwe mtumwa kiasi hicho. Komba kasema nini bungeni! Bulembo kasema nini bungeni! Ni kelele tupu hakuna hoja.kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake.ccm leo haipo kesho chama kingine chukua hatua.
 
Back
Top Bottom