UKAWA wamjibu Magufuli kuhusu kutofanya siasa, wasema wataendelea kwa kuwa katiba inawaruhusu

Hahahahahah jamaa zetu awa waoza meno, hawaamini kama watanzania hawawataki. Waongeaji wakuu wote wawili wanywa mbege
Yaani ni wale wale. Mimi nasema waache kutoa maneno tu waje wa vitendo. Waanzishe maandamano moshi maana wote wanatoka huko. Halafu kipondo kinaanzia huko. Hapa hakuna kumchekea mnywa mbege.
 
Mlizoea kupiga blabla sasa hivi magogoni yupo mwanaume anaunguluma, siasa ni 2020 mkileta fyoko hizo ni porojo na siasa zisizo na faida
 
Mbowe anasema atafanya vitendo vya kigaidi tunasubiri aoneshe hivyo vitendo vya kigaidi!
 
JK aliitwa dhaifu tena ndani ya bunge,JPM atawanyoosha tena watanyoka kama rula.
Mbowe ukitangaza maandamano tafadhali wewe na wenzako mnaopeana viti maalum na unaokula nao ruzuku muwe viongozi wa hayo maandamano.
Mimi nasubiri watakapo andamana!
 
Ukiona hivyo ujue watu wameanza kukata tama na wanaweza kufanya lolote kumaliza hasira zao bila kujali nini kitawatokea.
Mbowe amesema atafanya vitendo vya kigaidi nasubiri kuona jinsi atakavyo fanya vitendo vya kigaidi!
 

Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni amepinga vikali kitendo cha Magufuli kuzuia watu kusema amesema unapozuia watu kusema unasababisha watu kusema kwa vitendo na wakisema kwa vitendo vitendo hivyo vinakuwa vya uvunjifu wa amani, Amesema nchi ziizojaa magaidi ni nchi ambazo marais wake walikuwa wanajifanya wababe na watawala kujifanya wana mamlaka zote

Ameshangaa pia kiongozi huyo aliposema kuwa atawalinda marais wastaafu kwani marais wastaafu wanalindwa na katiba wala sio kauli zake, amemtaka wasaidizi wake wamsaide aache kuropoka kwani kauli zake zinalifarakanisha taifa.

Naye mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia amesema Magufuli amewekwa na katiba ya Tanzania hivyo anshangaa yeye mwenyewe anapoipinga katiba na marais wengine wasingefuata katiba kama yeye anavyofanya leo hii asingekuwa rais wa Tanzania na kwamba hawezi kukataza siasa kwa kuwa ipo kikatiba na vyama vipo kisheria.
Ameongezea bila mgongano wa mawazo na demokrasia hakuna maendeleo hivyo.

Naye Peter Msigwa amesema Magufuli anaonekana anapata ushauri wa kijeshi kuliko wa kisiasa, amemtaka kutumia ushauri wa kisasa kwani vyama vya upinzani vina wafuasi wengi na haitakiwi kutumia nguvu kama anajua maana ya siasa.

Amesma ni kweli nchi ilikuwa na ufisadi na ukosefu wa nidhamu nchini kutokana na utawala wa Kikwete kuwa dhaifu lakini pamoja na kuwa na nia nzuri ya kuondoa vitu hivyo vyote havimpi uhalali wa kufanya mambo bila kutumia sheria na taratibu zilizowekwa na wanamtaka avifanye kwa kutumia sheria.

My Take
Nimemuona Mbowe yupo smarter na wiser kuliko Magufuli japokuwa yeye hana Phd, achukue ushauri hawezi kutawala kwa namna hii, 2020 mbali sana na ameshaanza kujutia urais ndani ya miezi 8

Kwa mawazo yake mazuri labda ana DhP
 
Mbowe is a big failure. Mtu anabadili gia angani na kuleta mafisadi aliotuaminisha miaka mia. Pathetic kabisa, Magu fanya kazi achana na hawa wapiga domo.
Amesema kuhusu mambo ya kigaidi kutokea nasubiri tuone! Halafu Mch aliyenyoa kiduku amesema wazi Magufuli alishinda kwa kura 8Million!
 
Mbowe beba silaa mkononi maneno kidogo...mwenzako cku nyingi anaweka maneno mawili vitendo 10000...wew endelea kukusanya media tuu
 
chinchilla coat hiyo Phd inaanza kuleta utata, haiwezekani Marais wa nyuma ambao hawana Phd hawakusoma kwa miaka mingi kama yeye waweze kujieleza vizuri kwa kimombo lakini yeye hakipandi. Na kupanga hoja hata kwa Kiswahili ni shida ni mwendo wa kukurupuka tu. Inatia shaka.
 
Na amesema mwenyewe kuwa anaweza kufanya vitendo vya kigaidi!
Hivyo Mbowe ni gaidi!
Mambo yote ya mauaji yaliyokuwa yanatokea mwanza na tanga anayehusika ni yeye. Tumesikia kwa masikio yetu. Mbowe ni muuaji.
 
Back
Top Bottom