Bungeni pako hygienic ! Genge la CHASO huwezi kulinganisha na BUNGE!Nasikia wengine wanaruhusiwa wawe na mahafali lakini kama kule dodoma kuna ugonjwa ambao ulikuwa unahatarisha mkusanyiko wa CHASO lakini siyo BUNGE!!!!
Bungeni pako hygienic ! Genge la CHASO huwezi kulinganisha na BUNGE!Nasikia wengine wanaruhusiwa wawe na mahafali lakini kama kule dodoma kuna ugonjwa ambao ulikuwa unahatarisha mkusanyiko wa CHASO lakini siyo BUNGE!!!!
Sioni mantiki ya ulichoandika zaidi ya kujifurahisha tu kama wale waliopiga marufuku mkutano kwa sababu zisizo na mashiko .Bungeni pako hygienic ! Genge la CHASO huwezi kulinganisha na BUNGE!
Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni amepinga vikali kitendo cha Magufuli kuzuia watu kusema amesema unapozuia watu kusema unasababisha watu kusema kwa vitendo na wakisema kwa vitendo vitendo hivyo vinakuwa vya uvunjifu wa amani, Amesema nchi ziizojaa vurugu ni nchi ambazo marais wake walikuwa wanajifanya wababe na watawala kujifanya wana mamlaka zote
Ameshangaa pia kiongozi huyo aliposema kuwa atawalinda marais wastaafu kwani marais wastaafu wanalindwa na katiba wala sio kauli zake, amemtaka wasaidizi wake wamsaide aache kuropoka kwani kauli zake zinalifarakanisha taifa.
Naye mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia amesema Magufuli amewekwa na katiba ya Tanzania hivyo anshangaa yeye mwenyewe anapoipinga katiba na marais wengine wasingefuata katiba kama yeye anavyofanya leo hii asingekuwa rais wa Tanzania na kwamba hawezi kukataza siasa kwa kuwa ipo kikatiba na vyama vipo kisheria.
Ameongezea bila mgongano wa mawazo na demokrasia hakuna maendeleo hivyo.
Naye Peter Msigwa amesema Magufuli anaonekana anapata ushauri wa kijeshi kuliko wa kisiasa, amemtaka kutumia ushauri wa kisasa kwani vyama vya upinzani vina wafuasi wengi na haitakiwi kutumia nguvu kama anajua maana ya siasa.
Amesma ni kweli nchi ilikuwa na ufisadi na ukosefu wa nidhamu nchini kutokana na utawala wa Kikwete kuwa dhaifu lakini pamoja na kuwa na nia nzuri ya kuondoa vitu hivyo vyote havimpi uhalali wa kufanya mambo bila kutumia sheria na taratibu zilizowekwa na wanamtaka avifanye kwa kutumia sheria.
My Take
Nimemuona Mbowe yupo smarter na wiser kuliko Magufuli japokuwa yeye hana Phd, achukue ushauri hawezi kutawala kwa namna hii, 2020 mbali sana na ameshaanza kujutia urais ndani ya miezi 8
Naendesha maisha yangu sio kwa cheti bali kilichopo kichwani mwangu, we kumbe ulienda kufuata cheti shule ndio maana bongo lala.Kafeli kwa lipi au kwa sababu amekutumbua? Na bado waliokuwa wanakula hela za watumishi hewa wanasubiri kushitakiwa. Na nyinyi mliofoji vyeti. Chuki yenu itaongezeka maradufu