Dkt. Slaa: Ni wapumbavu pekee ndio wanaweza kubinafsisha Maeneo muhimu ya Nchi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Wakuu, Balozi mstaafu Dkt. Willbrod Peter Slaa anazungumza live kwenye Medani za Siasa Star TV.

Sababu ya kuondoka CHADEMA ilikuwa ni kumpokea Edward Lowassa kuwa mgombea Urais wa chama hicho. Dkt. Slaa amesema alizunguka nchi nzima akiutangazia umma kuwa Lowassa ni fisadi, na alimtangaza Mwembeyanga kwenye orodha ya mafisadi nchini (The list of shame). Asingeweza tena kumsafisha kwa namna yoyote ile.

Amesema Hayati Magufuli aliwahi pia kuwa na makosa ya ufisadi wakati wa kuuza nyumba za serikali, na miongoni mwake ni makosa mwili ambayo yeye Dkt. Slaa anayafahamu ikiwemo kugawa nyumba ya Serikali kwa “girlfriend wake”.

Anasema Balozi ana njia za kuwasiliana na Raisi Moja kwa moja ili kupeleka ushauri wake, ivyo hawezi kusema ni kitu gani alikuwa akiishauri serikali na Hayati Magufuli wakati akiwa balozi, pia amesema hata Mawaziri wana njia zao za kupeleka mawazo na ushauri wao huwezi kuwasikia wakipiga kelele kama wabunge maana wao wana njia zao.

Pia si kila kitu kipingwe hadharani, balozi ana njia zake na ivyo kama vipo alivyompinga Rais Magufuli basi alimpinga kwa kutumia njia hizo.

Pia amesema Magufuli hakupiga marufuku vyama vya siasa kwa kuwa ili Rais aseme inabidi aandike kama hakuandika ivyo hakusema na vyama vya upinzani viliogopa kwa kuwa na woga na yeye aliona udhaifu huo na ili kuotoka mtegeni ndio maana alitamka na si kuandika.

Amesema Rostam, hana hadhi ya kujibiwa na mtu wa hadhi yake, ameshampunguza kama punge ya shanga au haradali, hana hoja hivyo amempuuza. Amesema Rostam anaweza kutamka upuuzi tu wa anachotaka.

Dkt. Slaa Amesema Mwalimu Nyerere aliwahi kusema tusibinafsishe maendeo muhimu ya nchi yetu ambayo ni Bandari, Uwanja wa ndege, na mengine jumla yalikuwa 5, amesema ni nchi ya wapumbavu pekee ndio wanaweza kubinafsisha maeneo muhimu ya nchi.

Anasema bandari ni sehemu muhimu, ni kama geti kwenye nyumba na bandari ndio geti la nchi, sasa unachukua geti unamkabidhi mtu hapo utakuwa huru kweli?

Aliweka swali kidogo kimaanisha hakuta kuwa na uhuru. Anasema hayo yanayosemwa na Serikali juu ya mkataba kuwa si mkataba bali ni makubaliano ni propaganda za Serikali ili kuwafanya watu wakubali na hajui kwa nini wanafanya ivyo.

Anasema waandishi Mnaambiwa huo si mkataba ni makubaliano na nyie mnakubali, ina maana waandishi hamkusoma, kiingereza hamjui au hata kama hamjui hamna kamusi, mkataba umeandikwa agreement maana yake mkataba, sasa kwanini mnaambiwa na Msigwa nanyi mnakubali, mnamsikiliza Msigwa ambaye yupo kufanya propaganda tu na si kueleza kisheria.
 
Asante wadhamini
Kule Zanzibar, Ali Karume kasema wazi CCM haijawahi shinda uchaguzi tangu 1995 na sasa huku Bara kwa mujibu yule aliyehongwa ubalozi na CCM (Kwa mujibu wa mtunza fedha wa ccm mstaafu Rostam Aziz) ni kwamba 2015 Lowasa wa CHADEMA alishinda urais.

Ukimwaga mafuta ya taa kwenye shimo la nyoka wote wanatoka nje, ndiyo hiki kinachotokea
 
Tufanyeje sasa Lowasa kama alishinda!

Naunga mkono DP kutimliwa nchini hata kwa mtutu
 
Anasema waandishi Mnaambiwa huo si mkataba ni makubaliano na nyie mnakubali, ina maana waandishi hamkusoma, kiingereza hamjui au hata kama hamjui hamna kamusi, mkataba umeandikwa agreement maana yake mkataba, sasa kwa nini mnaambiwa na Msigwa nanyi mnakubali, mnamsikiliza Msigwa ambaye yupo kufanya propaganda tu na si kueleza kisheria.
Hata FaizaFoxy amekiri kuwa ule sio mkataba ni Makubaliano! Dah
 
kwa kuwa ili Rais aseme inabidi aandike kama hakuandika ivyo hakusema na vyama vya upinzani viliogopa kwa kuwa na woga na yeye aliona udhaifu huo na ili kuotoka mtegeni ndio maana alitamka na si kuandika.
Hapa anazingua, kauli ya rais ni sheria. Ni nani ambaye rais akitoa kauli badala ya kuitekeleza ataanza kudai maandishi?
Kinana tu aliwahi kutoa kauli ya kuwataka matrafiki kupungua barabarani na ilifuatwa bila siku iliyofuata tu, ndiyo iyakua kauli ya rais?
 
Samia kwa ujinga wake bado yupo kimya licha ya hizi kelele zote zinazoendelea akiamini iko siku zitapoa, huyu ndie aina ya kiongozi tuliyenaye, asiyetaka kusikiliza maoni ya wale anaowaongoza, na kujoamulia kufuata anachotaka yeye kwa maslahi ya wajomba zake walioko arabuni.

Aache kufuata ushauri wa kijinga anaopewa na huyo anayemuamini, atambue huyo anayempa huo ushauri sio malaika, ni mwanadamu, asiyejua hali halisi ikoje zaidi ya kuishi kwa kukariri, akiamini watanganyika wa jana ndio wa leo, waache kujidanganya.

Kama anajielewa atazame muda ambao hizi kelele zimekuwa zikipigwa bila kukoma, ajiulize kama ameshawahi kushuhudia hali hii hapo kabla, ajue huu ukimya wake ndio unazidi kupandisha hasira za wengi, zinazowafanya kuongeza sauti zao kulaani ule mkataba wa hovyo walioingia usiomthamini mtanganyika, na kumtukuza mwarabu ndani ya ardhi ya Tanganyika, uvunjwe.
 
Nonsense.

Dr. Slaa anapewa jeuri na katiba ya nchi inayompa haki ya kutoa maoni yake, huu ujinga wenu wa kuhusisha kila jambo na dini umepitwa na wakati, msijipotezee muda, hadanganyiki mtu waambie na wenzako.
Dkt. Slaa njaa tu inamsumbua, akirushiwa fupa leo kauli zitabadilika, yeye anaangalia tumbo lake tu.
 
Hapa anazingua, kauli ya rais ni sheria. Ni nani ambaye rais akitoa kauli badala ya kuitekeleza ataanza kudai maandishi?
Kinana tu aliwahi kutoa kauli ya kuwataka matrafiki kupungua barabarani na ilifuatwa bila siku iliyofuata tu, ndiyo iyakua kauli ya rais?
Wapi imetamkwa kuwa kauli ya Rais ni sheria?
 
Hapa anazingua, kauli ya rais ni sheria. Ni nani ambaye rais akitoa kauli badala ya kuitekeleza ataanza kudai maandishi?
Kinana tu aliwahi kutoa kauli ya kuwataka matrafiki kupungua barabarani na ilifuatwa bila siku iliyofuata tu, ndiyo iyakua kauli ya rais?
Hili hutokea kwenye nchi ya mazombi kama Tanzania
 
Wakuu, Balozi mstaafu Dkt. Willbrod Peter Slaa anazungumza live kwenye Medani za Siasa Star TV.

Sababu ya kuondoka CHADEMA ilikuwa ni kumpokea Edward Lowassa kuwa mgombea Urais wa chama hicho. Dkt. Slaa amesema alizunguka nchi nzima akiutangazia umma kuwa Lowassa ni fisadi, na alimtangaza Mwembeyanga kwenye orodha ya mafisadi nchini (The list of shame). Asingeweza tena kumsafisha kwa namna yoyote ile.

Amesema Hayati Magufuli aliwahi pia kuwa na makosa ya ufisadi wakati wa kuuza nyumba za serikali, na miongoni mwake ni makosa mwili ambayo yeye Dkt. Slaa anayafahamu ikiwemo kugawa nyumba ya Serikali kwa “girlfriend wake”.

Anasema Balozi ana njia za kuwasiliana na Raisi Moja kwa moja ili kupeleka ushauri wake, ivyo hawezi kusema ni kitu gani alikuwa akiishauri serikali na Hayati Magufuli wakati akiwa balozi, pia amesema hata Mawaziri wana njia zao za kupeleka mawazo na ushauri wao huwezi kuwasikia wakipiga kelele kama wabunge maana wao wana njia zao.

Pia si kila kitu kipingwe hadharani, balozi ana njia zake na ivyo kama vipo alivyompinga Rais Magufuli basi alimpinga kwa kutumia njia hizo.

Pia amesema Magufuli hakupiga marufuku vyama vya siasa kwa kuwa ili Rais aseme inabidi aandike kama hakuandika ivyo hakusema na vyama vya upinzani viliogopa kwa kuwa na woga na yeye aliona udhaifu huo na ili kuotoka mtegeni ndio maana alitamka na si kuandika.

Amesema Rostam, hana hadhi ya kujibiwa na mtu wa hadhi yake, ameshampunguza kama punge ya shanga au haradali, hana hoja hivyo amempuuza. Amesema Rostam anaweza kutamka upuuzi tu wa anachotaka.

Dkt. Slaa Amesema Mwalimu Nyerere aliwahi kusema tusibinafsishe maendeo muhimu ya nchi yetu ambayo ni Bandari, Uwanja wa ndege, na mengine jumla yalikuwa 5, amesema ni nchi ya wapumbavu pekee ndio wanaweza kubinafsisha maeneo muhimu ya nchi.

Anasema bandari ni sehemu muhimu, ni kama geti kwenye nyumba na bandari ndio geti la nchi, sasa unachukua geti unamkabidhi mtu hapo utakuwa huru kweli?

Aliweka swali kidogo kimaanisha hakuta kuwa na uhuru. Anasema hayo yanayosemwa na Serikali juu ya mkataba kuwa si mkataba bali ni makubaliano ni propaganda za Serikali ili kuwafanya watu wakubali na hajui kwa nini wanafanya ivyo.

Anasema waandishi Mnaambiwa huo si mkataba ni makubaliano na nyie mnakubali, ina maana waandishi hamkusoma, kiingereza hamjui au hata kama hamjui hamna kamusi, mkataba umeandikwa agreement maana yake mkataba, sasa kwanini mnaambiwa na Msigwa nanyi mnakubali, mnamsikiliza Msigwa ambaye yupo kufanya propaganda tu na si kueleza kisheria.

If privatisation gas economic sense let it be upumbavu
20230702_071619.jpg
 
Back
Top Bottom