UKAWA waeleza sababu za kuzomea Bungeni

Bado haijaeleweka,kuzomea zomea ni ulimbukeni na haitoi taswira ya watu civillised,afterall sio mara ya kwanza na ndio sababu tendo lenyewe la kuzomea wala halikuwa na punch kwa wananchi kwani waliona hakuna jipya na kwamba UKAWA NI ILE ILE.nilikuwa nimekaa na mwanangu wa miaka minne wa chekechea akawa ananiambia "baba waone wale wanafanya kama sisi shuleni" NIMEMNUKUU.

Hahahahahahah
 
Bado haijaeleweka,kuzomea zomea ni ulimbukeni na haitoi taswira ya watu civillised,afterall sio mara ya kwanza na ndio sababu tendo lenyewe la kuzomea wala halikuwa na punch kwa wananchi kwani waliona hakuna jipya na kwamba UKAWA NI ILE ILE.nilikuwa nimekaa na mwanangu wa miaka minne wa chekechea akawa ananiambia "baba waone wale wanafanya kama sisi shuleni" NIMEMNUKUU.

Shule ipi hiyo nami nimlete mwanangu wenda akawa mwana mabadiriko.
 
Ile Sinema ya UKAWA ya Jana ni watanzania wachache sana ndio wameielewa!

Ukawa lazima watambue uungwaji mkono toka kwa wananchi umeshuka sana, hasa kutokana na siasa zao figisufigisu.

Na kwa mwendo wa Magufuli. Wasipobadili siasa zao za matukio ndio wamejimaliza kabisa!
 
Action ya UBABE inazaa reaction ya UGAIDI kwa wale wanaotawaliwa kibabe! Chunguza mataifa yote yenye magaidi kuwa inaanza vipi!Serikali zilizoko madaraka ndizo zinaziasisi vikundi vya ugaidi bila kujua kwa kuendekeza ubabe badala ya demokrasia ya kweli!!
 
wabunge haswa vijana wa ukawa wakumbukue wakifata msimamo wa pashkuna mbowe basis 2020 kurudi bungeni itakua ni mwiko.
 
Kwani kelele zao zimesaidia nini.amiri jeshi mkuu na raisi alitoa hotuba yake ambayo ni mwaka na kuipa dira uongozi wake wakiwemo hao ukawa ambao kwa hotuba yake amewamaliza ukawa.watanzani tumuunge mkono raisi wetu kupasua majipu
 
Ha ha ha,kumbe fidfosi waliingia mpaka ndani?,ndo maana nilishangaa wameondokaje kirahisi mle
 
wamefanya kosa kubwa, hata kama ccm wana mpango wa kuwaachia madaraka "kwa hisani" nadhani waufute tu, wayatafute kwa haki
 
Wabunge wa Ukawa wameelezea sababu zilizowafanya kuchukua uamuzi wa kupiga kelele baada ya Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein kuingia Bungeni hali iliyopelekea kutolewa nje ya Bunge hilo.

Mbunge wa jimbo la Hai ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe alieleza kuwa walishindwa kuvumilia kuona ujio wa Dkt Shein akiingia Bungeni hapo pamoja na msheshimiwa Pandu Kificho ambaye alidai hivi sasa sio Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuwa Baraza hilo lilikwisha vunjwa.

Tumeshangaa kuona Pandu Kificho anaingia kama Spika wa Baraza la Wawakilishi wakati Baraza limeshavunjwa, tulishangaa kuona Dkt Shein anaingia kama Rais wa Zanzibar wakati huo kipindi chake cha kukaa madarakani miaka mitano kimekwisha kikatiba, alisema Mbowe.

Naye mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alisisitiza kuwa wataendelea kuonesha msimamo wao huku akimlalamikia Spika wa Bunge hilo kuwa anaendesha Bunge kibabe.

Leo hii askari wenye uniform, mae-FFU askari wa fujo wameingia ndani ya ukumbi wa Bunge. Sasa kwa wasiofahamu, ukumbi wa Bunge katika nchi kama za kwetu na nchi zinazofuata utaratibu kama wa kwetu, ukumbi wa Bunge huwa haingii mtu yoyote asiyekuwa Mbunge. Ndio maana ili Makamo wa rais na wale wakubwawakubwa tuliokuwa tunawapigia kelele? waingie, ilibidi tutengue kanuni ili kuwaruhusu waingie, alisema Tundu Lissu.

Mwenyekiti wa wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Hamad Omary alimtaja Maalim Seif Sharif Hamad kuwa kiongozi anayepaswa kuigwa kwa kuwa aliwahi kukubali kushindwa mara kadhaa licha ya mapungufu kuonekana na kwamba hata alipokuwa Makamu wa Kwanza wa rais na kisha wawakilishi wa CCM kukataa asuhudhurie kwenye sherehe za kufunga Baraza la Wawakilishi, aliamua kutohudhuria.

Chanzo: Dar 24


...mara kadhaa nimeshuhudia "kivumbi na jasho" katika bunge la Ukraine kupitia kwenye luninga....na kwa hali ninayoiona, bunge lingeanza kwa kurekebisha sheria kuruhusu "wanausalama" kuingia ndani ya bunge kwa dharura...vinginevyo, nahofia...!
 
Vipi aligusia kitendo cha maalim kujitangaza mshindi kabla tume haijamaliza kutangaza matokeo?

(Ccm tayari tushashinda zaidi ya majimbo 174 mpaka sasa) january marope. Hapo bado hata jimbo moja kuhesabiwa kura. Nyani haoni nani h...ii lake.
 
Ile Sinema ya UKAWA ya Jana ni watanzania wachache sana ndio wameielewa!

Ukawa lazima watambue uungwaji mkono toka kwa wananchi umeshuka sana, hasa kutokana na siasa zao figisufigisu.

Na kwa mwendo wa Magufuli. Wasipobadili siasa zao za matukio ndio wamejimaliza kabisa!

kwani ndiyo kwanza unaona au ndiyo kwanza inatokea?
 
Wabunge wa CUF na UKAWA tz kama waliingia Bungeni, basi hawana msimamo thabiti wa kumsaidia Maalim. Kama Maalim ameminywa haki yake, wabunge wote wa UKAWA na CUF Z'bar wangesusia Bunge ili kumpa sapoti.Kwa maana nyingine, hawana mshikamano wanajali maslahi ya posho yao binafsi!
 
Back
Top Bottom