UKAWA vs CCM katika urais, piga Kura hapa

UKAWA vs CCM katika urais, piga Kura hapa

UKAWA VS CCM KATIKA URAIS

  • UKAWA

    Votes: 757 85.2%
  • CCM

    Votes: 118 13.3%
  • NONE OF THE ABOVE

    Votes: 13 1.5%

  • Total voters
    888
Status
Not open for further replies.
Heshima sana wanajamvi,

Mwezi October waTanzania tutafanya uchaguzi wa madiwani,wabunge, Rais wa nchi ya Zanzibar na Rais wa JMT.Nafasi zote hizo ni muhimu kuanzia udiwani,ubunge na rais wa JMT.Kila mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura natumaini atapiga kura na atafanya uchaguzi wa mtu au chama anachoona kinaweza kumvusha kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

Uchaguzi wa mwaka huu (2015) ni kati ya CCM chama tawala na UKAWA muungano wa vyama vya CDM,CUF,NCCR Mageuzi na NLD.Ni wazi uchaguzi wa mwaka huu utakuwa moto moto haswa si katika nafasi ya uras tu bali ubunge na udiwani pia.

Kwa mara ya kwanza katika siasa za Tanzania tumeshuhudia wapinzani wakiunganisha nguvu dhidi ya CCM chama tawala,hichi kimekuwa kilio cha watanzania wengi ambao wamekuwa wakiwapigia kelele wapinzani juu ya umuhimu wa kuunganisha nguvu kwakuwa hawana rasilimali ukilinganisha na chama tawala.Pia kuondoa uwezekano wa kugawa kura zao.
WaTanzania tuna nafasi ya kuchagua either UKAWA au CCM.Ni wazi uchaguzi huu hatuna uwanja mpana sana,tumenyimwa fursa pana tumefungwa kwenye nafasi mbili UKAWA ama CCM.

Kwakuwa tumepewa uwanja mdogo (CCM v/s UKAWA) hakuna utitiri wa vyama ukilinganisha na hali ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita ni busara sasa kuwaunga mkono wapinzani si kwamba naamini watakuja na sera bora,si kwamba watakuja utekelezaji mzuri sana, si kwamba watakuja kubadili maisha yetu ndani ya muda mfupi hapana.Tuwapigie kura UKAWA kwasababu mbili muhimu.

Mosi ni kuondoa kiburi,ghilba,sera mbovu,kujisahau kwa chama tawala CCM.
CCM iliyoanzishwa na waasisi wake Mwl J K Nyerere imeacha kutetea wanyonge,imeacha kuwasemea wakulima na wafanyakazi,imeacha misingi ya kuanzishwa kwake.

CCM kimekuwa chama cha madalali wa kuuza rasilima za nchi,imekuwa kinara wa kuingia mikataba mibovu isiyokuwa na faida kwa taifa na wananchi wake.

Kuipigia kura UKAWA maana yake ni kukataa kiburi cha CCM,maana yake ni kukataa mikataba mibovu,maana yake ni kuwakumbusha wajibu wao (kimejisahau).Maana yake ni kuandaa uwanja wenye usawa katika chaguzi zitakazofuata na hili ndilo jambo kubwa sana yapo mazoea mabaya kwamba CCM lazima ishinde hata kama hakitutendei mema wananchi lazima kishinde.Tukiwaweka bench siku chaguzo zijazo hawatakubali kumlinda mla rushwa,mzembe na nk.Wajifunza kwamba sisi wananchi ndio maboss wao na si watu wa kupuuzwa kama ilivo desturi yao.

Ngongo wa JF ameshafanya uamuzi mwezi October siendi kubahatisha,nitawapigia kura UKAWA kwasababu kwa mara ya kwanza wametambua umuhimu na kuheshimu umoja.

Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.
 
1. Si mtu wakutafuta sifa kwenye media.

2. Hashirikiani na wafanyabiashara maana wengi ndiyo mafisadi na wahujumu uchumi wa nchi.

3. Nimtendaji na muwajibikaji kwahiyo ni kiongozi anayehitajika.

NB: Mimi siyumbishwa na makundi, sitafuata mkumbo, sitarubuniwa kwa hela na maneno yote ya ushawishi.

Nilizaliwa peke yangu nitakufa peke yangu nasema NO kwa wasaka tonge kura yangu itabaki kwa Magufuli.
 
Ujielewi ndio mana..... Hakuna hoja hapo zaidi ya upumba.vu na uji.nga wako.... Utampa kura wewe na Mama Salama
 
Kupiga kura na kumchagua umpendae wa kumpa kura ni gali yako haijalishi jiwe au magufuli
 
Ujielewi ndio mana..... Hakuna hoja hapo zaidi ya upumba.vu na uji.nga wako.... Utampa kura wewe na Mama Salama

Wewe ndiyo huna hoja. Matudi ya nini leta hoha zenye nguvu. Rais wetu ni Magufuli. Nina imani naye. Hivyo matusi yako hayaninyimi fursa ya kupiga kura. Cyberbulling has no room here!
 
Lizaboni,Lowasa hatafuti sifa kwenye media mkuu,ila media zinaangalia ni nani popular halafu zinampa airtime ili kulinda maslahi na matakwa ya wananchi!!
 
Last edited by a moderator:
Lizaboni,Lowasa hatafuti sifa kwenye media mkuu,ila media zinaangalia ni nani popular halafu zinampa airtime ili kulinda maslahi na matakwa ya wananchi!!
Kwa hiyo ni maslahi gani ya wananchi yanalindwa kwa kumpa air time ya kutosha Lowasa?
 
1.Fedha za uuzaji wa nyumba za Serikali alizipeleka wapi?
2. Wale samaki aliowakamata walilinufaisha Taifa au walulitia hasara Taifa?
3. Vipi zile billion 252 za Wizara ya Ujenzi zilizopotea bila Maelezo ya kina kutoka kwa Magufuli unazizungumiaje?
4. Hapo alipo Magufuli ameweza Kuhenga nyumba za gorofa kama NNE hivi katika viwanja tofauti tena kwa kipindi kifupi je tukikuuliza hizo fedha katoa wapi utaweza kutujibu?
 
Hiyo sifa namba 1 "kutotafuta sifa kwenye media" Naamini unaongea kinyume!
Huyo unayempigia debe ndiye mwenyewe kwa kutafuta misifa kwa kutumia media. Hakuna anayemzidi!
 
Kwa hiyo ni maslahi gani ya wananchi yanalindwa kwa kumpa air time ya kutosha Lowasa?

Maslahi ya wananchi ni kuwa wananchi wanahitaji mabadiliko nje ya CCM na Lowasa yupo nje ya CCM kwa hiyo kwa kulipa air time ya kutosha jina la Lowasa in kulinda maslahi ya wananchi
 
Urais wa bahati nasibu....huyu jamaa naona atakuwa puppet wa wakubwa tu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom