meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,349
- 4,674
- Thread starter
- #41
Unapotaka nilinganishe uhalifu wa tanzania na south africa, nikishalinganisha inasaidia nini..? Nani kakwambia kwamba kipimo cha uhalifu wa tanzania ni south africa kwa nini isiwe congo, rwanda, uganda nk..!? Au kwani south kukiwa na uhalifu mkubwa inakuwa ni haki tanzania kuwa na uhalifu..?
vijana wa ccm mjifunze kusoma makala na vitu mbali mbali, mnazorotesha nchi kuwa na vijana wenye ufahamu mdogo
kipindu pindu ni kati ya magonjwa yanayoonesha ni kiasi gani nchi ina umaskini, kwasababu mara nyingi husababishwa na huduma mbovu za jamii ikiwepo
1.makazi
2.upatikanaji wa maji safi na salama
3.usafi wa mazingira(uzoaji wa taka taka)
4.mipango miji mibovu
5.high population density in the cities(watu kukimbilia mjini kusaka maisha bora)
6.huduma mbovu za afya jamii(public health)
Na nchi nyingi duniani zilitokomeza kipindu pindu mda mrefu sana, kama uk, us tangu miaka ya 1800 huko
so ni indicator jinsi huduma za jamii zilivyombovu under ccm na hayo ndo mambo ya kuongea na muache kumsingizia mtu mmoja ndo ksasababisha, maana sasa kila kitu lowasa ndo kasababisha
Tatizo unataka kuingiza utaalamu katika Afya na siasa.
Malaria kama ilivyo kipindupindu ni ugonjwa uliosumbua sana nchi masikini lakini ndani ya miaka mitano iliyopita Malaria imepungua na kupunguza vifo kwa zaidi ya 50%.
Ukimwi vile vile umepungua kutoka 8% ?mpaka 5% katika kipindi hicho hicho.
Magonjwa ya kuhara na vifo vitokanavyo vimeanza kupungua yameanza kupungua katika kipindi hiki cha miaka mitano.
Point yangu hapa ni Unailaumu system hiyo hiyo ambayo imefanya mazuri mengi isipokuwa katika kipindupindu tena kinachotokea Uswahilini tu.
Kuhusu uhalifu ...nilikuwa nakushangaa tu ulivyomention issue ya mtu kuchomwa kisu kwenye basi...na wewe ndio inakuwa ni sababu ya kuikataa ccm na kutaka kuwapa Genge la wahuni.