UKAWA ni Genge hatari kwa amani, utulivu na maslahi mapana ya Tanzania


meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
8,066
Points
2,000
meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
8,066 2,000
Mimi nilikuwa muumini makini wa Chama makini cha upinzani kilichojijenga taratibu mpaka kuonekana kuwa pengine kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

CHADEMA ilikuwa taratibu bila misukosuko mingi mpaka pale kilipoanza kuonekana pengine kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

Wananchi walianza kazi kwa umakini kabisa wa kuipa chadema majimbo ya ubunge kadhaa na serikali za mitaa.

Wananchi walianza kuitambua na kuisaidia chadema kwa michango ya kadiri mbalimbali.

Ni maumivu makali kwa CHADEMA kupoteza focus na kutaka kukimbilia kile ambacho wananchi hawakukiandaa au kukipanga kwa ajili yao.

Hii ina maana Chadema itarudi miaka 20 nyuma na mbaya zaidi kuiacha Tanzania bila mbadala wa Chama bora cha upinzani.

KUHUSU GENGE LA UKAWA:

Itoshe kusema kuwa UKAWA ni genge hatari sana kwa usalama na Ustawi wa Taifa letu kwa sababu au chambuzi zifuatazo:

1 - Edward Lowassa:
Yuko serious katika kuutaka urais na alipenda kwa udi na uvumba kuupata urais kupitia ccm ingawa ilishindikana iwe kwa fitina au kwa kukosa vigezo. Huyu yuko Ukawa kwa lengo la urais tu na anaitumia chadema kama chombo cha kuupata urais. Anaweza akawa na sababu zake lakini sitajadili kwa leo. Lakini haipendi Chadema au UKAWA.

2 - Maalim Seif na CUF:
Huyu naye ni mtaka urais tu lakini anaweza kuwa na ajenda yake ile ile iliyobebwa na CUF Zanzibar yaani kuitaka Zanzibar huru. Alitulizwa baada ya kupewa cheo lakini baada ya vuguvugu la katiba na shinikizo la kichama amejikuta akianza chokochoko upya.

Pia tusisahau CUF inaungwa mkono na makundi kama yale ya uamsho kiasi cha kumfanya mgombea urais wa UKAWA kutamka hadharani kuwa atawaachia huru watuhumiwa wa ugaidi.

3 - CHADEMA Asilia na Maslahi:
Kuna kundi la wanachadema walio serious na kutaka mabadiliko ya kweli.kundi hili limekatishwa tamaa na mambo makubwa mawili yaliyotokea yaani kumpokea lowassa bila maelezo ya kueleweka na kumpa kijiti cha kugombea urais,pili kukatwa kwa Dr Slaa na kutothaminiwa kwa mchango wake ndani ya Chadema.

Chadema maslahi ni kina Mbowe na washkaji kibao kutoka pande za Arusha na Moshi. Hawa wako kimaslahi zaidi, Issue kwao ni chama kinaingizaje fedha au mikutano inaingizaje fedha au nguo na adverts za chama zinaingizaje fedha. Hawa wanaendesha Chadema kama kamati ya harusi za kichaga.

4 - Team Lowassa, Ulipo tupo na 4UMovement:
Hili ni genge ndani ya genge! Katika kundi hili kuna watoto wa kishua wanaosubiri kupiga dili kama za watoto wa vigogo.

Katika kundi hili kuna waliokosa ajira na fursa na hivyo kujishikiza kwa lowassa ili ikitokea kapata na wao watoke(hawajui uhuni wa mwanasiasa)

Katika kundi hili kuna watoto ambao wako tu kwenye age yao ya 'fantancy' na kuburudika na maisha.

5 - WanaCCM viongozi waliomfuata Lowassa:
Hapa kuna mchanganyiko wa waliokatwa kwa kuwa ni makapi haswa. Pia wako walioshtukia dalili za kukosa wakigombea kupitia CCM(Lembeli).

Pia wapo wanaojaribu kuibuka upya kwa mgongo wa Lowassa. Humu pia kuna mashushu kutoka CCM.

6 - NCCR na Mbatia na NLD:
Hili ni kundi lisilojielewa linahitaji nini. Mbatia anaweza kuwa ni mpiga dili flani hivi na pia baada ya kuonja ubunge wa kuteuliwa anatamani angepata ubunge ili aweke mambo sawa.

7 - Wanaharakati na waandishi:
Hawa wako katika kutegemea nafasi za kuteuliwa kama ilivyozoeleka huku wakisahau kuna vijana wengi na wenye weledi. Wengi wao wameumizwa na tendo la CCM kukata na kuvunja makundi na option waliyobakiwa nayo ni kujipendekeza UKAWA.

8 - Wafanyabiashara:
Hawana uhakika kabisa wa EL kushinda nje ya CCM na wamebaki kuuma na kupuliza.
Ingawa kuna wachache bado wanagamble kuendelea kuamini katika EL kuchukua kijiti.

9 - Wachungaji/Maaskofu:
Ni wachache na wanajaribu kutumia karata ya zamu ya mlutheri lakini kimsingi wanataka kutetea matumbo yao tu.


Ukiwa na genge la namna hii na likiwa halina uongozi au miongozo inayoeleweka utakuwa unaongelea nchi iliyoanguka. Ni lazima genge hilo lipate Kiongozi na Muongozo kwanza ndio ufikirie kuwapa nchi.
 
Ryaro wa Ryaro

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
2,661
Points
1,225
Ryaro wa Ryaro

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
2,661 1,225
Ungesema kwa Maslahi Mapana ya MaCCM Watanzania Wangekuelewa. CCM ya Leo No Kirusi Hatari Sana...Hatudanganyiki Tunakwenda Name Mh. Lowassa Hanna Namna Iwayo yoyote.
 
I

IKINGO

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
1,701
Points
2,000
I

IKINGO

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
1,701 2,000
"CCM mkitaka #KURA yangu semeni ukweli nani anahusika na hizi tuhuma? na wahusika wamechukuliwa hatua gani?
-Katiba pendekezwa nani aliyaondoa maoni ya wananchi ambayo yalikuwepo kwenye rasimu ya Warioba?
-Mabehewa feki
-Kiwira
-Richmond
-Epa
-Escrow
-Epa
-Dowans
-IPTL
-NET GROUP SOLUTIONS
-Usafirishaji wa wanyama nje ya nchi mfano twiga alipandaje ndege?
-Biashara ya pembe za ndovu
-Biashara ya madawa ya kulevya
-Meremeta
-Mikataba ya gesi na mafuta
-Uuzwaji wa nyumba za serikali
Nahitaji majibu ya hayo maswali siyo porojo tuuuu za kipumbavu.
 
Fatal5

Fatal5

Senior Member
Joined
Jul 1, 2011
Messages
188
Points
195
Fatal5

Fatal5

Senior Member
Joined Jul 1, 2011
188 195
kwenda kule wewe na post yako ya utumbo....
haya majembe 2 ndio story za mjini sasa hivi

 
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
800
Points
250
Age
29
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
800 250
Hizo ni fulsa ndani ya ukawa.
 
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
800
Points
250
Age
29
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
800 250
"ccm mkitaka #kura yangu semeni ukweli nani anahusika na hizi tuhuma? Na wahusika wamechukuliwa hatua gani?
-katiba pendekezwa nani aliyaondoa maoni ya wananchi ambayo yalikuwepo kwenye rasimu ya warioba?
-mabehewa feki
-kiwira
-richmond
-epa
-escrow
-epa
-dowans
-iptl
-net group solutions
-usafirishaji wa wanyama nje ya nchi mfano twiga alipandaje ndege?
-biashara ya pembe za ndovu
-biashara ya madawa ya kulevya
-meremeta
-mikataba ya gesi na mafuta
-uuzwaji wa nyumba za serikali
nahitaji majibu ya hayo maswali siyo porojo tuuuu za kipumbavu.
majibu yote anayo el,akiwa ccm ndiye mratibuji wa hayo yote.
Kama aliweza kumsaidia rais wa 4 kwa 80% .hawezi kosa majibu.
 
A

ali bugdadi

Member
Joined
Aug 16, 2015
Messages
12
Points
45
A

ali bugdadi

Member
Joined Aug 16, 2015
12 45
Hao ambao wagombea ndo mainjinia wa hayo mambo au hamfaham na ndio mliokua mdawataja kwenye mikutano yenu leo wamekuwa vipusa
 
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Messages
3,880
Points
2,000
Age
28
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2013
3,880 2,000
Naona tim inafanya kaz kwa umakin...... Lkn ni ngumu kubadilisha...
 
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
46,078
Points
2,000
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
46,078 2,000
Mkuu wewe ni mzalendo ...Chadema kamwe hawato weza kupewa nchi hii...
 
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
800
Points
250
Age
29
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
800 250
= fursa

halafu kwenye id yako hiyo "recture" ndiyo nini?

Mnatia kichefuchefu.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
unahitaji maombi yaani unahoji jina la mtu?
Junior=jina la kwanza
recture=jina la pili la baba.
Ndunguru=la ukoo.

Zakupewa changanya na zako.usikurupuke.
 
S

simba wa mara

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2015
Messages
378
Points
0
S

simba wa mara

JF-Expert Member
Joined May 21, 2015
378 0
tulisha wazoea ht slaa mlisema at alifukuzwa upadrii kwa kuchota pesa leo mmehamia kwa edwd na slaa amekuwa teba lafik yenu!
 
S

simba wa mara

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2015
Messages
378
Points
0
S

simba wa mara

JF-Expert Member
Joined May 21, 2015
378 0
katiba mpya imeishia wap?tena walioba akawapa hd wanawake usawa lakn ccm mkaitupa na hawo wanawake walio pewa 50 kwa50 mkawatupa mkakurupuka na yenu iko wap sass?
 
T

Taffman

Senior Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
159
Points
225
T

Taffman

Senior Member
Joined Jul 11, 2015
159 225
Ndg meningitis,kwa taarifa tu ni kuwa lowassa na wafuasi wake wote wapo kila kona hasa kwenye tasnia nzm ya hbr,blogs,forums mbalimbali na vyombo vyote vya hbr vimetekwa na huyu ndg,lengo kuu ni kumsafisha na kupinga kila lisemwalo hasa likiwa nje au linapopingana na ndg lowassa na wengi wao ni hayo makundi uliyoyasema wao wapo tayari kwa lolote alimradi lowassa apate madaraka kivyovyote vile.
Suala la uadilifu ktk uongozi kwao its not an issue anymore,wanataka Mabadiliko no matter what,hivyo kuelezea udhaifu na shortfalls za cdm na ukawa na ni kupoteza muda na utapingwa sana,imani yao ni kuwa lowassa akiingia madarakani maisha yao yatabadilika kwasababu wengi wao wako hoi na wana tamaa ya maisha makubwa,wanaamini lowassa atabadili maisha yao kutoka ktk shida walizo nazo na kuwa matajiri,kiufupi wengi wao wana akili za nyumbu hivyo ht usemaje ni kz bure unapoteza muda wako
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
63,317
Points
2,000
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
63,317 2,000
unahitaji maombi yaani unahoji jina la mtu?
Junior=jina la kwanza
recture=jina la pili la baba.
Ndunguru=la ukoo.

Zakupewa changanya na zako.usikurupuke.

Na "fulsa" mbona hujatolea ufafanuzi?

Dah! unanidhihirishia kuwa ujinga upo kwenye damu yako.
 
meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
8,066
Points
2,000
meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
8,066 2,000
Ndg meningitis,kwa taarifa tu ni kuwa lowassa na wafuasi wake wote wapo kila kona hasa kwenye tasnia nzm ya hbr,blogs,forums mbalimbali na vyombo vyote vya hbr vimetekwa na huyu ndg,lengo kuu ni kumsafisha na kupinga kila lisemwalo hasa likiwa nje au linapopingana na ndg lowassa na wengi wao ni hayo makundi uliyoyasema wao wapo tayari kwa lolote alimradi lowassa apate madaraka kivyovyote vile.
Suala la uadilifu ktk uongozi kwao its not an issue anymore,wanataka Mabadiliko no matter what,hivyo kuelezea udhaifu na shortfalls za cdm na ukawa na ni kupoteza muda na utapingwa sana,imani yao ni kuwa lowassa akiingia madarakani maisha yao yatabadilika kwasababu wengi wao wako hoi na wana tamaa ya maisha makubwa,wanaamini lowassa atabadili maisha yao kutoka ktk shida walizo nazo na kuwa matajiri,kiufupi wengi wao wana akili za nyumbu hivyo ht usemaje ni kz bure unapoteza muda wako
Mkuu ndio maana elimu hii inakuja hapa hapa mtandaoni.

Haijalishi unapendwa au kuungwa mkono lakini ukweli lazima usemwe.
 
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Messages
3,813
Points
1,225
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2012
3,813 1,225
Ivi watu wengine mnaishi wapi"Amani na utulivu"
wakati watu wanapora mchana saa saba kwenye basi lenye abiria.?
vituo vya polisi vinavamiwa mchana kweupe
twiga wanapanda ndege na watu wanaona hivi hivi..
utulivu upi wakati watu uswahilini wanakufa na kipindu pindu karne ya 21, mwaka 2015 bado kuna kipindu pindu.
utulivu wakati kuna mfumuko wa bei watu wanashindwa kumudu maisha mkate sh 1500
nyinyi vijana wa ccm acheni kutukana na kudharau watu kwenye mitandao, mnawaona malofa, kana kwamba hawajui machugu na wanaishi kwa amani na utulivu sana chini ya ccm..!?
 
N

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2013
Messages
22,502
Points
2,000
N

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2013
22,502 2,000
mkuu maneno meeengi lakini hakuna hoja zaidi ya majungu na mipasho. ukawa ni tishio kwa maslahi mapana ya ccm na familia zao. mwaka huu twende na lowasa...
 
meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
8,066
Points
2,000
meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
8,066 2,000
Ivi watu wengine mnaishi wapi"Amani na utulivu"
wakati watu wanapora mchana saa saba kwenye basi lenye abiria.?
vituo vya polisi vinavamiwa mchana kweupe
twiga wanapanda ndege na watu wanaona hivi hivi..
utulivu upi wakati watu uswahilini wanakufa na kipindu pindu karne ya 21, mwaka 2015 bado kuna kipindu pindu.
utulivu wakati kuna mfumuko wa bei watu wanashindwa kumudu maisha mkate sh 1500
nyinyi vijana wa ccm acheni kutukana na kudharau watu kwenye mitandao, mnawaona malofa, kana kwamba hawajui machugu na wanaishi kwa amani na utulivu sana chini ya ccm..!?
Umeshawahi kusikia uhalifu South Africa?

Unaulinganisha vipi na Tanzania?

Unatofautisha vipi kipindupindu,malaria,typhiod,Ukimwi na kisukari??
 

Forum statistics

Threads 1,285,931
Members 494,830
Posts 30,879,334
Top