UKAWA mnaniharibia mwanangu, nakosa raha nyumbani

UKAWA mnaniharibia mwanangu, nakosa raha nyumbani

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,006
Kila nikitaka kwenda nyumbani kwangu,nasitasita. Natafakari namna na kujibu mapigo ya mpigo toka kwa mwanangu. Kijana wangu huyu aliye Chuo Kikuu,akiwa likizoni sasa,ananitambia na kunibeza katika nyumba yangu mwenyewe.

Najuta kumpa uhuru wa kidemokrasia tangu akiwa Shule ya Msingi. Kila akiniona ananitambia kuhusu UKAWA na kukwama kwetu kama CCM.

Nimejaribu kumwambia kuwa mimi sipo tena kwenye kampeni za CCM. Bado ananing'ang'ania. Ananibakisha CCM na kunihusisha moja kwa moja na kampeni za wagombea wetu kuanzia Dr.Magufuli, Mama Samia, wale wa Ubunge na Udiwani.

Nyumba yangu mwenyewe imegeuka uwanja wa tambo na vikumbo vya kikampeni. Yeye amejipambanua kuwa ni mfuasi wa UKAWA kupitia CHADEMA.

Leo, ameshanipigia simu kujiproud kuwa Lowassa anaibomoa ngome ya CCM pale Millenium Towers. Anadai kuwa Lowassa atawateka wanawake wa Tanzania na kuifanya CCM ibaki na wazee tu kama wapigakura wake.

Akajinasibu kuwa wanawake wa Tanzania wanaiacha mkono CCM na inaelekea kuyumba pamoja ya karata yake ya kumsimamisha Mama Samia kama mgombea mwenza.

Leo pia, amenidokeza kuwa watanzania hawa si wale. Amesema kuwa ana tafiti zilizo fiti zikionesha kuwa UKAWA ndiyo dawa. Ananisubiri anioneshe nikifika nyumbani jioni.

Lengo lake nalijua. Ni kuninyanyasa kisiasa lakini kisasa. Kwa hoja za haja bila kubadili lahaja. Najiandaa,kwa kujisomea nyaraka za haraka na baraka,kwenda kupindua tafiti zake. Nikifika nyumbani, kampeni za chumba kwa chumba zitaanza.

UKAWA mmeniharibia mwanangu. Kwasasa hadi ana kibwagizo chake: MAGUFULI APIGE KAMPENI, LOWASSA ATAPIGIWA KURA! Kazi kwelikweli.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Kila nikitaka kwenda nyumbani kwangu,nasitasita. Natafakari namna na kujibu mapigo ya mpigo toka kwa mwanangu. Kijana wangu huyu aliye Chuo Kikuu,akiwa likizoni sasa,ananitambia na kunibeza katika nyumba yangu mwenyewe. Najuta kumpa uhuru wa kidemokrasia tangu akiwa Shule ya Msingi. Kila akiniona ananitambia kuhusu UKAWA na kukwama kwetu kama CCM.

Huyo ni mtoto au mtu mzima mwenzio? Mimi ningemtandika ngumi moja ya uhakika ambayo ingemfanya asiwe mwanachama wa chama chochote milele na ambayo ingemfanya hata akiona watu wanaongelea siasa awakimbie.
 
Yaani watoto wa siku hizi sijui wamepata wapi mwamko wa kisiasa. Mwanangu ana 9years lakini anasema anaichukia CCM na anataka raisi awe LOWASA. Nimefuatilia shuleni kama wanafundishwa siasa za vyama nikaguundua hamna. Nikamdodosa akaniambia wakiwa kwenye mabasi ya shule huwa wanaongea na pia wanapata taarifa kutoka vyombo vya habari yaani luninga. Ila inaniogopesha at that age awe na msukumo kiasi hicho.
 
Mzee Tupatupa,
Nakushauri na wewe twende huko huko ukawa,
mwambie mwanao amwambie mama yake na ndugu
zake na majirani na marafiki wote hasa wale wasomi wa
chuo kikuu ............. kura zao zote kwa UKAWA.

Hata mimi na mama mkubwa kura yangu ni kwa UKAWA.
 
MAGUFULI APIGE KAMPENI, LOWASSA ATAPIGIWA KURA! Kazi kwelikweli.

Hii safi sana maana naona wanazuia sehemu za kampeni lakini wamesahau kura hawawezi zuia!
 
Huyo ni mtoto au mtu mzima mwenzio? Mimi ningemtandika ngumi moja ya uhakika ambayo ingemfanya asiwe mwanachama wa chama chochote milele na ambayo ingemfanya hata akiona watu wanaongelea siasa awakimbie.

Wewe umevurugwa kama wakubwa wako hekima hukaa kwa mtu mwenye busara lakini hasira hulala kifuani kwa mp.umba.vu.
 
Kwa nini usitumie ule mkakati wa kichama kutumia Dola? Tupatupa wewe ni mtu mkubwa hapo Lumumba hivyo sidhani kama Kova hakufahamu. Mwalike dinner kwako leo huku ukiwa umempa agenda za kuzungumza na familia yako baada ya msosi safi atakao andaa mama Yeyoo. Kumbuka Kova anapenda sana Pilau.
Awapige bit wanafamilia yako kuwa;
Kutokana na kukithiri kwa matukio ya uvunjifu wa amani ni mwiko kuzungumzia mambo ya vyama saa za jioni majumbani,
Tishio la alshababu bado lipo hivyo vijana wasiongee na wazee kuhusu CCM,
Kuna uwezekano wa matokeo yake ya chuoni kufutwa kama ataonekana anaendelea kuisifu Ukawa, na mwisho amwambie upo uwezekano kwa wanafunzi wapenzi wa ccm kupewa scholarship kwenda China baada tuu ya uchaguzi na kuwa zile 50 milioni za kila kijiji atapewa mwanafunzi mmoja mmoja badala ya vijiji.
Hapo heshima itarudi tuu.
 
Wewe umevurugwa kama wakubwa wako hekima hukaa kwa mtu mwenye busara lakini hasira hulala kifuani kwa mp.umba.vu.

Acha lisomeke kama ulivyokusudia wewe una hekima halafu unakosa kujiamini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom