UKAWA mnaniharibia mwanangu, nakosa raha nyumbani

UKAWA mnaniharibia mwanangu, nakosa raha nyumbani

Mapadlock piga kampeni, Kura zote ni kwa Lowassa. UKAWAAAAAA ze enddddddddddddddddddddddddddd
 
Huyo ni mtoto au mtu mzima mwenzio? Mimi ningemtandika ngumi moja ya uhakika ambayo ingemfanya asiwe mwanachama wa chama chochote milele na ambayo ingemfanya hata akiona watu wanaongelea siasa awakimbie.

Kijana wa CHADEMA, KAMANDA akiwa CHUO ni komandoo tayari roughly 21 yrs and above... ww unaweza mpigaa...??

Kabla hujarusha ngumi, UKO CHINI...

UNATAKA KUAMKA HUNA MENO...

UNATAKA KUTUKANA TEKE LA MDOMO

UNATAKA KUOKOLEWA ANAKUVUA NGUO NA C.HUPI...

UNATAKA kumwomba msamaha UNAKOSA PUMZI YA KUONGEA KWA KUKANYANGIWA KICHWA SAKAFUNI...

UNAANZA KUTOA MACHO KAMA MJUSI KABNWA NA MLANGO...

Wee unajua ngumi kweli...? Unatania wee...utacha nyumba na kukaa porini au kuhamia kwa ndugu...!!😨😨👊👊👊


Peopleeeeees'...👊👊👊✌✌✌✌
 
kuna utoto mwingi unaendelea humu mpaka nashangaa, hali ya humu na mtaani tofauti kabisa.
 
'Anayemtaka Lowasa akanywe naye chai' by Nyerere 1995. Ikulu si pango la wanyang'anyi.
 
Kila nikitaka kwenda nyumbani kwangu,nasitasita. Natafakari namna na kujibu mapigo ya mpigo toka kwa mwanangu. Kijana wangu huyu aliye Chuo Kikuu,akiwa likizoni sasa,ananitambia na kunibeza katika nyumba yangu mwenyewe.

Najuta kumpa uhuru wa kidemokrasia tangu akiwa Shule ya Msingi. Kila akiniona ananitambia kuhusu UKAWA na kukwama kwetu kama CCM.

Nimejaribu kumwambia kuwa mimi sipo tena kwenye kampeni za CCM. Bado ananing'ang'ania. Ananibakisha CCM na kunihusisha moja kwa moja na kampeni za wagombea wetu kuanzia Dr.Magufuli, Mama Samia, wale wa Ubunge na Udiwani.

Nyumba yangu mwenyewe imegeuka uwanja wa tambo na vikumbo vya kikampeni. Yeye amejipambanua kuwa ni mfuasi wa UKAWA kupitia CHADEMA.

Leo, ameshanipigia simu kujiproud kuwa Lowassa anaibomoa ngome ya CCM pale Millenium Towers. Anadai kuwa Lowassa atawateka wanawake wa Tanzania na kuifanya CCM ibaki na wazee tu kama wapigakura wake.

Akajinasibu kuwa wanawake wa Tanzania wanaiacha mkono CCM na inaelekea kuyumba pamoja ya karata yake ya kumsimamisha Mama Samia kama mgombea mwenza.

Leo pia, amenidokeza kuwa watanzania hawa si wale. Amesema kuwa ana tafiti zilizo fiti zikionesha kuwa UKAWA ndiyo dawa. Ananisubiri anioneshe nikifika nyumbani jioni.

Lengo lake nalijua. Ni kuninyanyasa kisiasa lakini kisasa. Kwa hoja za haja bila kubadili lahaja. Najiandaa,kwa kujisomea nyaraka za haraka na baraka,kwenda kupindua tafiti zake. Nikifika nyumbani, kampeni za chumba kwa chumba zitaanza.

UKAWA mmeniharibia mwanangu. Kwasasa hadi ana kibwagizo chake: MAGUFULI APIGE KAMPENI, LOWASSA ATAPIGIWA KURA! Kazi kwelikweli.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Teh teh teh ...Watoto wa siku hizi watukutu sana, Nimependa hako kamsemo chao!
 
Kwa hiyo mnataka kutujenga kisaikolojia kwamba Lowassa hatapiga kampeni kwa kuwa mna migogoro mbalimbali ikiwemo ya kifedha, kimkakati, kisera na kiafya?
UKAWA itazindua kampeni na mtakoma , hizi kampeni zenu ni za kitoto sana , subiri moto .
 
Huyo ni mtoto au mtu mzima mwenzio? Mimi ningemtandika ngumi moja ya uhakika ambayo ingemfanya asiwe mwanachama wa chama chochote milele na ambayo ingemfanya hata akiona watu wanaongelea siasa awakimbie.

Nahisi haurufu ya uchagonja
 
Lowassa hatapiga kampeni?

Lowassa apige Kampeni, au asipige sio Issue sana, cha muhimu sisi wapiga kura tumeshamuelewa, utumishi wake uliotukuka unajulikana pia lengo kuu ni kuiondoa CCM madarakani ili tuanze kujenga taifa letu upya!
 
Yaani watoto wa siku hizi sijui wamepata wapi mwamko wa kisiasa. Mwanangu ana 9years lakini anasema anaichukia CCM na anataka raisi awe LOWASA. Nimefuatilia shuleni kama wanafundishwa siasa za vyama nikaguundua hamna. Nikamdodosa akaniambia wakiwa kwenye mabasi ya shule huwa wanaongea na pia wanapata taarifa kutoka vyombo vya habari yaani luninga. Ila inaniogopesha at that age awe na msukumo kiasi hicho.

Watoto wa siku hizi wee acha tu! Mwanangu ana miaka 7 jana kaniambia eti wakiwa darasani mchana walisikia ndege zikipita angani (nadhani zile za jeshi), wakashangilia wakisema Lowasa, Lowasa, Lowasaaaa!
 
Huyo ni mtoto au mtu mzima mwenzio? Mimi ningemtandika ngumi moja ya uhakika ambayo ingemfanya asiwe mwanachama wa chama chochote milele na ambayo ingemfanya hata akiona watu wanaongelea siasa awakimbie.

Weee utafungwa kwa kosa la kujeruhi na kusababisha maumivu
 
Huyo ni mtoto au mtu mzima mwenzio? Mimi ningemtandika ngumi moja ya uhakika ambayo ingemfanya asiwe mwanachama wa chama chochote milele na ambayo ingemfanya hata akiona watu wanaongelea siasa awakimbie.

nimeishia kucheka tu...
 
Ukiona mambo ambayo hayajawahi tokea kabla yanatokea ujue kweli mabadiliko hayazuiliwi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom