Ukawa kuanza oparesheni mkoa wa dar 6/8/2014

Ukawa kuanza oparesheni mkoa wa dar 6/8/2014

Kweli kabisa Mkuu. Dar hawana chao UKAWA. Wataaibika bure

Racism is still with us! hata wewe una sapot upumbav, jitaidini kujifunza propaganda safi, sio kuhamasisha chuki, udini, ukabila na ukanda! hata kama porojo ndio ujira wenu bt jitaidi kuwa makini ..
 
Bila Ukawa hakuna Katiba mpya, maoni ya wananchi kwanza ya CCM Lumumba.

Kwani wana CCM sio wananchi?

Hao wananchi hasa ni akina nani? Ni Wajerumani ambao wanawapa hela kuvuruga mchakato? Una hakika kuwa waliohudhuria mikutano ya maoni ni "Wananchi".

Unajua reliability ya research ambayo imefanyika kwa "voluntary response sampling"? Unajua reliability ya research iliyofaniyika kwa sampling methods kama "Convenient sampling" na "Snowballing" Maoni ya katiba yalikusnywa kwa mitindo hiyo hapo juu, hivyo kusema kwamba ni "Wananchi" inaweza ikawa siyo sahihi.

Kuna dhambi gani kujadili ubaya wa serikali tatu sambamba na kujadili mbili au moja? Mbona CCM wamejadili tatu hao "Wananchi" wanaogopa nini?

Rasimu ilipelekwa JMK "kujadiliwa" na "kuboreshwa" Tukiacha kujadili mifumo yote, tutakuwa hatujawatendea haki hata hao "Wananchi"

Ukweli utakuweka huru.Tukijadili mifumo yote, ndipo "wananchi" wa kweli watajulikana.Ni makosa kuamini kuwa "wananchi" ndio wenye haki ya kuteka JM kwa hoja yao ya serikali tatu!!!
 
Wana jamvi kuna taarifa ambayo bado haijathibitishwa kuwa kuanzia tarehe tajwa hapo juu ni kwamba wana ukawa watapiga mikutano ya hadhara kata zote mkoa wa dar kuomba uungwaji mkono mpana wa wananchi dhidi ya wale ccm wanao kataa maoni ya katiba ya wananchi,timu ya wabunge,madiwani,wanaharakati na watu maarufu nchini watagawana kata za mkoa wa dar kupiga mikutano ya hadhara kwa siku 4 mfurulizo na hatimae kuhitimisha mkutano wa hadhara mkubwa jangwani ambao timu nzima ya ukawa bara na znz itakuwepo jangwani,hivyo wananchi jiandaeni na kuwapokea ukawa dar kwa fujo!ccm hawaponi kwa dhambi ya kunyonga maoni ya wananchi

Waende BMK watuache tufanye kazi. Wajadili uzuri na ubaya wa serikali tatu, mbili au moja tuwaunge mkono kwa hoja. Wanaogopa nini kwenda JMK? Kwani baada ya BMK si bado tutarudi kwa "wananchi" wa kweli?

Waache woga na majungu, waende BMK!!! Wasiogope!!! BMK ndio wananchi wote watawasikia, na sio "Wananchi" wao tu.
 
Ndugu yangu Riziki Magembe Nina ujumbe mmoja, jitahidi sana ukiandika thread yako basi iwekee paragraph na capital letters! Pia ujitahidi sana kufanya proof reading kabla hujapost kwani si tu humu JF hata kwa ujumbe wa simu uutumaa basi utakuwa ni ujumbe sahihi.

Muda unao soma vitabu na jinsi ya uandishi Mzuri utakusaidia sana maishani mwako! Leo nimekukumbusha Kama kijana mwenzangu! Asante sana!

Ndugu msahihishaji, nini maana ya maneno "ujumbe wa simu uutumaa" kama ulivyoaandika kwenye aya kwanza??
Kila mtu na udhaifu wake bwana
 
Watu tuko busy na kazi zetu na biashara zetu, usiokuwa na kazi za kufanya nendeni mkatumike kwa manufaa ya wanasiasa uchwala.
 
Kule wanadanganyika ila siyo Dar hapa ni bongo bhana mbululazi wako huko

we ndo mbulula hujitambui kwa kuona walioko nje ya dar wadanganyika..kaa hapo usubiri wenye ubongo wakusaidie kufikiri na kuchukua maamuzi
 
Back
Top Bottom