Ukatili na roho mbaya katika kundi hili la bodaboda vinasababishwa na nini?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,709
36,166
Hili kundi la bodaboda a.k.a Maafisa usafirishaji mostly ni watu wakatili na wenye roho mbaya.

Kijana mwenzao kapata pikipiki ya mkataba akipeleka pua tu kwenye kijiwe wanamtoza laki 2, 3, 4 au aondoke haraka kabla hawajamwitishia mwizi.

Laki 3 kijana ambaye ni jobless ndio kwanza kapata pikipiki ataitoa wapi? Bodaboda huyo anayemtaka mwenzake atoe laki 3 hajawahi kuishika hiyo pesa cash tangu azaliwe.

Hili kundi wakimshika mwizi wanamuua kama kuku, unaona kabisa hakuna utu ndani yao.

Hii hali ni magonjwa ya akili au ni msongo wa mawazo kutokana na maisha magumu?
 
Mimi ni bodaboda mashuhuri mjini Iringa, naomba nijibie hoja yako ya msingi hasa ya kulipisha kiingilio laki 2+.

Vijiwe vimefurika idadi ya pkpk hivyo hujiwekea utaratibu huo ili kupunguza vijana wasiokua siliazi lkn pia inaondoa mlundikano wa pkpk nyingi kijiwen kuliko abiria na saa nyingine utakuta eneo ni dogo linabana wapita njia au magari.

Uzuri vijiwe vingi hasa mjini wana hadi katiba na ndani yake kuna utaratibu wanao kijiwekea kama wanachama na sio huo tu saa nyingine kuchangiana kwenye majanga na heri.

Suala la kupiga mwizi hayo mambo yanategemeana eneo na eneo pia aina ya watu waliopo hapo sio boda tu hata watu wa kawaida hupiga vibaya wezi nafikiri watu wengi wametendewa unyama na hao wezi hivyo akikamatwa ni kama vile hasira zinaishia kwake.
 
Jamaa wakali mno,huu utaratibu nilkuwa siujui sasa kipind nimemaliza chuo nikawa na utaratibu wa kuchukua pikpik jion naenda kupak popote ambapo kuna maboda boda pembeni yao ili niwe napata vihela hela vya matumiz,sasa siku moja nikashangaa wananivamia ghafla wakanipiga mkwala kweli kweli wakataka wanipige cheni au wanipeleke kwenye kituo cha polis bahat nzur ile pikpik ilikuwa ya serikal nilijitetea kwa kukana kuwa mimi sibebi abiria baadae wakaniacha nikasepa
 
Sasa kwanini wasikuelimishe kwanza au ulikua mkaidi?
 
Hili kundi la bodaboda a.k.a Maafisa usafirishaji mostly ni watu wakatili na wenye roho mbaya.
Kijana mwenzao kapata pikipiki ya mkataba akipeleka pua tu kwenye kijiwe wanamtoza laki 2, 3, 4 au aondoke haraka kabla hawajamwitishia mwizi.
Laki 3 kijana ambaye ni jobless ndo kwanza kapata pikipiki ataitoa wapi?
Bodaboda huyo anayemtaka mwenzake atoe laki 3 hajawahi kuishika hiyo pesa cash tangu azaliwe.
Hili kundi wakimshika mwizi wanamuua kama kuku, unaona kabisa hakuna utu ndani yao.
Hii hali ni magonjwa ya akili au ni msongo wa mawazo kutokana na maisha magumu?
Siyo kwamba watu wote wenye boda boda ambao wapo vijiweni kweli ni "boda boda halisi*, walio wengi hapo wapo kama geresha tu, wanazuga huku wakiwa na shughuli zao halisi zinazowaingizia kipato cha halali na haramu. Wezi nao wapo humohumo kwenye kazi za boda boda. Aidha, hata "mumiani" nao wapo humohumo kwenye kundi la boda boda, na ndio hao walitumika sana wakati ule wa mwendazake katika "kuchora ramani" za watu ambao kwao walikuwa ni 'target's' zao. Bodaboda wengi (surveillance agents) walitumika sana ktk kufanikisha mipango yao (mumiani) kwenye misheni za kuteka watu na hata kuwafanyia watu (walengwa wao) vitendo mbalimbali vya hujuma, na ktk wakati huo pikipiki nyingi sana mpya aina ya boxer zilinunuliwa na walipewa watu hao ili waweze kufanikisha mipango yao hiyo ya kidhalimu. Pikipiki hizo nyingi unaweza kuzitambua (endapo kama utakkuwa na macho makali sana ya mwewe ) kwani utaona zimewekwa alama fulanifulani za utambuzi za kificho ili kuwafanya baadhi ya "members" kutambulika kiurahisi na wahusika au members wenyewe kuweza kutambuana wao kwa wao wawapo kwenye missions zao huko kwenye vilinge vya bodaboda. Kwa hiyo usione ukadhani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom