Ukatili huu uliofanywa na Polisi Simiyu kwa Watoto wa shule, ni aina nyingine ya "ukaburu mamboleo"

Sisi waafrika niwapumbavu sanaaa. mbona tunakuwa kama hatujawa civilized au nikukosa elimu ya kibinadamu tunakuwa wanyama kiasi hiki, mwanafunzi mdogo hv unampiga kibano kama mtu mzima, kuna vitu vingine we have to think beyond sio kisa ww ni polisi basi una mamlaka yakupiga tu, Kumbuka kuwa polisi kaz yake kuu nikulinda mwananchi na malizake sasa huku kwenda kupiga watu anapata wap haya mamlka, guys me am just Tired with how african especially Tanzania governed us. We have to make this things hapen KATIBA i think Kidogo Hii Itapunguza Makali now we have Educated Leader Na wengi wao Wapo Opposition Party Naamini They will Make Tanzania A better place. Sio kwa kuonewa huku khaaaaaa...
Hiki ndo nilichomaanisha aabh lakn members wengi walicomment kuhus jinsi askari anavyokimbia...
 
mi naona tatizo ni elimu wanayopata haiendani na wakati tulionao,wapate mafunzo stahiki ya wakati huu tulionao wawe walinzi wa Amani tu wawasindikize na kulinda maandamano na si kushindana na nguvu za wananchi wanavunja Amani ya nchi .
 
Hawajafundishwa namna ya kukabili maandamano ya amani? Hao watoto walikuwa tu wanaprotest kuhusu kuondolewa mwalimu wao na wala hawakuwa hata na mawe.. sasa nguvu zote hizo za polisi zilikuwa za nini.
 
Hivi polisi hawa na mwalimu Frank wanatofautishwaje?
Waziri Mwigulu alifunga hadi safari kwa adhabu aliyopewa na mwalimu.
Lakini utasikia kimya kikuu kwa hawa polisi kwa hiki walichokifanya kwa hawa watoto ni zaidi ya yaliyofanywa na yule mwalimu
 
Tena hao polisi hajafanya nnvyotaka, panya rodi ndo huwa wanaanzia huko huko, hiyo picha dogo anakimbia ilibidi kamanda aonekane anapiga bonge moja la kwanja, yaani kwanja ikibidi hata la kilo 8
Jina unalotumia ni moja kati ya majina niliyokuwa nayaheshimu lakini naanza kutia shaka. Kilichofanyika Simiyu kiko kinyume na haki za watoto na hata namna ya kudeal na rioters watoto ni tofauti na watu wazima na hili polisi wanalijua vizuri sema wanajitoa ufahamu tu. Huu ni udhaifu wa viongozi wa polisi eneo husika wala sio jeshi lote. Kama IGP hatakemea hili tutajua ni kweli lina baraka zake. Tunakumbuka wazee wa Africa mashariki walivyotendewa na FFU Dar, lkn kuna maeneo polisi wamekabili matukio kama haya kwa weledi. Siku moja miaka kadhaa iliyopita nilikuwa mkoa wa Rukwa wilaya Nkasi kwa Kazi ya wiki moja na wanafunzi wa sekondari moja wakaandamana kama hawa kwenda kwa Dc, lakini polisi walitumia busara na kuwasindikiza kwenda uwanja wa mpira badala ya ofisi UA Dc na OCD akamwomba mkuu wa wilaya akaonane nao. Alioonana nao walitoa kero zao kwa amani na wakaondoka kwa amani. Nikibaki kushangaa kumbe kuna polisi wana hekima kiasi hiki!!!?
 
Tunaomba haki za binsdamu na wizara ya Ummy (ina jina refu sana) na hata wizara ya Mwigulu watoe karipio kali kwa Iwe ni Ocd au kiumbe gani, ikiwezekana ashushwe cheo! Namaanisha huyo aliyeamrisha polisi wawapige watoto!
 
Kwanza mimi naona polisi hawajafanyaka kazi niliyotamani mimi.
Huu ni upumbavu wa hali ya juu kucheka cheka na madai ya kijinga kijinga.
Serikali inagharamika mabilioni ya pesa halafu wanafunzi wanakuja kuandamana kwa madai ya kijinga namna hii?...Hiiii.....ningekua mimi ndio DC au RC wa hapo aise wangeisoma namba...
Bora wangeandamana kwa kukosa madawati,vyumba vya madarasa au walimu

Sio ujinga wa namna hii,mkuu barafu naheshimu sana mawazo yako lakini sikubaliani na wewe....kuna mdogo wangu alikuwepo hapo,ndio naelekea Bariadi,atanitambua nikifika labda nikute masomo yake yote ana A
 
Cha kushangaza wafuasi wa Lipumba wakiamua kuandamana kuelekea kwenye ofisi za chama kushinikiza Li-pumba kurudishwa ofisini na ulinzi wanapewa kabisa na hawa polisi maskini ya Mungu..

vitoto vya shule vinavyohitaji mwalimu wao kurudishwa ofisini ndo vinaonekana hatari kwa amani ya nchi kuliko wafuasi wa li-pumba.
No way i think kuna laana somewhere in the corner of our state
 
Utasikia siku yoyote mkuu wa kaya atawasifiwa hao police kwa kipigo walichowapa wanetu, hakyamungu hadi kufika mwaka 2020 tutavunjwa viuno aisee ,,,
 
Siku zote baadhi ya wachunga ng'ombe wanakua na roho za kikatili saana
Mpwa umepotea sana. Hili la Simiyu linanikumbusha yale yaliyotokea Kenya miaka ya karibuni. Watoto walifanya fujo na kubomoa ukuta uliokuwa umejengwa kwenye eneo lao la shule na tajiri mmoja akawa amezuia eneo lao la kuchezea.
Polisi walikuja na kufyatua mabomu tuu ya machozi, kilichofuata ni Makamishna kadhaa wa Polisi walifukuzwa kazi kesho yake tuu. Hakuna cha tume wala nini, umepiga mabomu watoto toka!
Hapa sio ajabu wamewapiga na watapandishwa vyeo
 
Wapuuzi sana hao hasira zao za kutapeliwa kwenye uchaguzi kuwa wataongezwa mishahara ndio wanakuja kumaliza hasira kwa watoto wetu, konyo zao kabisa, walaaniwe wao na watoto na watoto wa watoto wao
Hivi kumbe waliingizwa chaka !
 
Police wanawashwa.hawajapiga watu siku nyingi.siku hizi hatuandamani.tunaandamana kwenye mitandao.mpaka utupate wote ufanye kazi
 
sasa hivi vitoto FFU wa nini, wangevisubiri tu vinarudi shule wanachapa viboko... haya ni matumizi mabaya ya nguvu.
 
Yule aliyesema "i wish i could be IGP", hiki ndicho alichomaanisha!Wala hao Ma RC,DC hawana kosa,walimsikia mkuu vizuri,ukileta fyoko utashughulikiwa!
Au mlitaka Rc aje aulizwe kama alivyoulizwa IGP!
RC anafanya akijiuliza," what would Magufuli do'?
 
Kwanza mimi naona polisi hawajafanyaka kazi niliyotamani mimi.
Huu ni upumbavu wa hali ya juu kucheka cheka na madai ya kijinga kijinga.
Serikali inagharamika mabilioni ya pesa halafu wanafunzi wanakuja kuandamana kwa madai ya kijinga namna hii?...Hiiii.....ningekua mimi ndio DC au RC wa hapo aise wangeisoma namba...
Bora wangeandamana kwa kukosa madawati,vyumba vya madarasa au walimu

Sio ujinga wa namna hii,mkuu barafu naheshimu sana mawazo yako lakini sikubaliani na wewe....kuna mdogo wangu alikuwepo hapo,ndio naelekea Bariadi,atanitambua nikifika labda nikute masomo yake yote ana A
Yaelekea wewe ulipata F zote!!hawa watoto wana akili kuliko wewe ndiyo maana walikuwa wanadai haki yao ya kupewa mwalimu mwenye uwezo!! Na kumgomea mwalimu hovyo mwenye hulka ya kibashiteBashite
 
Back
Top Bottom