Ukatili huu uliofanywa na Polisi Simiyu kwa Watoto wa shule, ni aina nyingine ya "ukaburu mamboleo"

Kweli hili linazidi kudhihirisha UKWELI wa Uislam, moja kati ya mafunzo ya Mtume Mohammad (s.a.w) amesama watakuja watu siku za baadae ambao wawo watakua ni WATU wa MOTONI watu hawa watakua na fimbo mikononi mwao za urefu kama mikia ya nyumbu KAZI zao zitukua ni KUWAPIGA WATU kwa UONEVU pasina kuangalia( mtoto wala mkubwa) basi eleweni ya kuwa makazi ya watu hawa ni JAHANAMA.
 
Na huwezi kunielewa mpaka siku utakapo acha kuchagua viongozi mazuzu ndo utaacha kuona watu wanaonewa na polisi.

Kama viongozi wako ni mazuzu kila siku utaendelea kupigwa na polisi.

Najua ninachosema, katika safari ya kutafuta maisha nimepita kwingi, wengine hata commands za jeshini hamjui wala viapo hamvijui ndio maana mnalaumu polisi.

Fikiria mkoa wenye RC au DC mzuri kama utakuja kusikia kuna mtu kapigwa Bomu na polisi.
Duuhh nimekuelewa
 
Inavyoelekea, kuna maeneo tuna viongozi wa hovyo ambao haijawahi kutokea.

Nilipokuwa shule ya msingi miaka ya 80, darasa letu lilibomoka. Siku 2 tukakosa masomo, tuliandamana. Hatukuguswa na mtu, mpaka tukafika tulikokusudia. Tulipofika tukasoma risala yetu ndogo tuliyoiandika, ikapokelewa. Viongozi tukaitwa ofisini kwa katibu tarafa. Kwanza alitusifu kwa kujali elimu yetu. Baadaye akasema kuwa tulifanya kosa kwa sababu sheria hairuhusu kuandamana.

Tulivyotoka nje Mwalimu Mkuu akasema kwa kuwa tumefanya makosa, itabidi tuomba msamaha, tukakubali. Akutuambia ni kwa namna gani tuombe msamaha. Tukafikiria wenyewe. Tukaandika risala fupi, tukarudi ofisini kwa Katibu Tarafa, tukaomba msamaha. Wakati tunasoma risala, wenzetu walikuwa wamepiga magoti. Katibu Tarafa alitusifu kwa hatua tuliyoichukua ya kuomba msamaha. Kesho yake darasa lilianza kujengwa, kila kiongozi wa eneo lile akiwepo.

Kama hawa viongozi wa kipindi kile walifanya hivyo, ina maana walikuwa na akili, busara na uelewa kuliko hawa tulio nao leo? Hao viongozi walioamrisha au kutenda unyama huo huko Simiyu waliokotwa wapi? Viongozi wa namna hiyo wapo tu huko Simiyu au wapo na kungine?

Viongozi waliotoa amri za kuwapiga watoto wa shule ambao walikuwa hawaandamani kwa vurugu, wafukuzwe kazi na washtakiwe. Pia wapimwe ili kujua kama ni mentally fit maana si rahisi mtu mwenye akili kutenda waliyoyatenda.
 
Inavyoelekea, kuna maeneo tuna viongozi wa hovyo ambao haijawahi kutokea.

Nilipokuwa shule ya msingi miaka ya 80, darasa letu lilibomoka. Siku 2 tukakosa masomo, tuliandamana. Hatukuguswa na mtu, mpaka tukafika tulikokusudia. Tulipofika tukasoma risala yetu ndogo tuliyoiandika, ikapokelewa. Viongozi tukaitwa ofisini kwa katibu tarafa. Kwanza alitusifu kwa kujali elimu yetu. Baadaye akasema kuwa tulifanya kosa kwa sababu sheria hairuhusu kuandamana.

Tulivyotoka nje Mwalimu Mkuu akasema kwa kuwa tumefanya makosa, itabidi tuomba msamaha, tukakubali. Akutuambia ni kwa namna gani tuombe msamaha. Tukafikiria wenyewe. Tukaandika risala fupi, tukarudi ofisini kwa Katibu Tarafa, tukaomba msamaha. Wakati tunasoma risala, wenzetu walikuwa wamepiga magoti. Katibu Tarafa alitusifu kwa hatua tuliyoichukua ya kuomba msamaha. Kesho yake darasa lilianza kujengwa, kila kiongozi wa eneo lile akiwepo.

Kama hawa viongozi wa kipindi kile walifanya hivyo, ina maana walikuwa na akili, busara na uelewa kuliko hawa tulio nao leo? Hao viongozi walioamrisha au kutenda unyama huo huko Simiyu waliokotwa wapi? Viongozi wa namna hiyo wapo tu huko Simiyu au wapo na kungine?

Viongozi waliotoa amri za kuwapiga watoto wa shule ambao walikuwa hawaandamani kwa vurugu, wafukuzwe kazi na washtakiwe. Pia wapimwe ili kujua kama ni mentally fit maana si rahisi mtu mwenye akili kutenda waliyoyatenda.
Mkuu umetoa mifano mizuri, hapa wengi wetu tunalaumu polisi, sawa polisi wametenda unyama ila polisi sio chanzo cha tatizo, polisi kuna mtu kawapa amri, yaani kwa ufupi viongozi ndio wametenda unyama.
Polisi hata aone watu wanaandamana hawezi kuwazuia wala kukataza bila kupewa amri

Tukubali hatuna viongozi wazuri maeneo hayo, huwezi kutumia polisi kuzuia maandamano ya watoto wa shule.
Mwaka mmoja baada ya Mimi kuhitimu kidato cha nne, niliowaacha kidato cha tatu waliandamana mpaka kwa REO wakishinikiza mkuu wa Shule ahamishwe na hakuna aliyewapiga mabomu wala makofi tena walitoka kijijini mpaka katikati ya mji bila tatizo, sasa hapo kiongozi alikua na utu wala hakuona sababu ya kutumia polisi, aliposikia kuna wanafunzi wanakuja mjini kwa maandamano akasema waacheni waje cha msingi lindeni wasiharibu miundombinu na rasilimali za jamii.

Sasa hivi tuna viongozi wanaojiona miungu watu, tatizo sio polisi na kama polisi ni tatizo basi mchango wao juu ya kusababisha tatizo ni kama 0.5% tu 99.5% ni viongozi
 
Nahisi police wakipewa order huwa hawaruhusiwi kufikili ila kuacf tuu

Ni kama marobot tuu
 
Nahisi police wakipewa order huwa hawaruhusiwi kufikili ila kuacf tuu

Ni kama marobot tuu
Ukijua hivi ni heri ukawadharau tu, ukiona wanakuja wewe mapema jiepushe nao.

Maana tutaishia tu kutoa mapovu kama hivi wewe tayari ni kilema.
 
alafu kesho polisi wakiuwawa wanasema eti wananchi tunaficha waharifu,hatutoi ushirikiano kweli kwa tabia hizi kweli mwananchi unaweza kuwa rafiki wa jeshi la polisi??Mwigulu nchemba anakuja humu kupiga watu mikwara eti wote tunaoshangilia kuuwawa kwa polisi tutashughulikiwa kwa namna hii kwanini polisi akiuwawa tusishangilie kw vifijo na nderomo..!!hivi kweli jeshi zima la polisi hakuna aliepita chuo cha psychology kujua jinsi ya kudeal na teens,lakini pia asante kwa awamu hii inayoendelea kujaza sumu kali ya kuichukia hii serikali katika kila tabaka ili next time waje wajipime nguvu zao na nguvu ya umma..Mungu tujalie ujasiri na uvumilivu wanyonge wataifa hili

nashangilia na pilau napika nakula nakunywa na soda
 
Toka jana kumekuwa na picha zinazosambaa zikiwaonyesha polisi wakikabiliana na watoto wa shule (Wanafunzi) huko Bariadi Mkoani Simiyu.

Watoto walioandamana kuelezea hisia zao juu ya kutokukubaliana na kuhamishwa kwa mwalimu wao waliompenda na kumuelewa,hawakumtaka Mwalimu mpya ambaye kwa utashi wao wanaona hakidhi viwango vya aliyemtangulia.

Tunaweza tusikubaliane na hitaji lao,lakini tuna wajibu wa kuheshimu malalamiko yao na kuwasilikiza.Hata kama hatutatimiza haja za mioyo yao,lakini tunapaswa kuwasikiliza watoto hawa kwa kile wanachokileza.

Haikuitajika nguvu kubwa ya kiasi kile kukabiliana na watoto wanaoanza kuelezea hisia zao za kutokukubaliana na uhamisho wa mwalimu wao.

Hii ilikuwa ni haki yao ya msingi,haki ya kuandamana na kukusanyika kuelezea hisia zao.Maandamano ya watoto hawa hayakuwa na fujo wala vurugu,wala hawakuvunja na kuumiza mtu.Waliandamana kwa upole,wakiwa na mabango na kwa kuimba nyimbo za staha kuelezea hisia zao.

Hii ni elimu waliyoipata darasani katika Somo la "Civics".Kidato cha pili na kuendelea wanafundishwa juu ya "Demokrasia na Haki za Binadamu".Kwa uelewa wao,ile ilikuwa ni namna ya kuonyesha walivyoelewa somo la Civics.

Mamlaka husika walipaswa kuwasikiliza,sababu walianza kuelekea ofisi za halmashauri kwa DED walizuiwa,wakaamua kuelekea kwa RC nako wakazuiwa.Huku kote walipita bila kufanya fujo.Viongozi wenye hekima na nuru ya kibaba/mama wangewasikiliza na kuwapa muongozo.

Lakini matokeo yake wamepiga na kuwajeruhi.Kwa miaka ya leo,watoto wengi wa sekondari ni chini ya miaka 20.Hawa ni wa kuwaelekeza na si kuwapiga na mabomu.Hawa ni wa kuwaongoza na kuwashauri na si kuwapiga virungu.Huwezi kumdhibiti mtoto wa chini ya miaka 20 kwa kutumia polisi 4.Huu si uungwana.

Viongozi wa mkoa wa serikali na polisi katika mkoa huu wametia aibu sana.Kwanini wanatengeneza kizazi cha kinafiki?kwanini wasiruhusu watoto wanaohoji?Hivi kunatengenezwa Taifa lipi la kutumia nguvu nyingi kwa jambo dogo??

Halafu polisi hawana uwezo wa kujua huyu ni mtoto?Haki za watoto kama hawa kubebwa juujuu na kudhalilishwa nani anapaswa kuwajibika?Je nguvu zilizotumika zinalingana na madhara waliyosababisha sbb ya maandamano yao?Kwa hatua zile,hatuoni kuwa tunatengeneza kizazi cha kisasi na chuki?

Watoto huongozwa,watoto hulindwa na watoto hutunzwa na kuelekezwa.Tusiwatendee watoto wadogo kama vile ni watu wazima.

Miaka kadhaa iliyopita nilijifunza jinsi nchi za wenzetu wanavyojali watoto na namna ya kuwaadhibu hata kama wamekosa.

Tulikuwa na rafiki yangu katika mji mkuu Rome-Italia,wakati huo kukiwa na wakimbizi wengi kutoka Ulaya Mashariki,wakiwemo watoto wengi wanaouuza miili yao na vijana ambao ni "vibaka"

Tunakatiza katika "Metro" kutoka mjini kati Rome Termini via Ottaviano S Pietro kuelekea St.Peter's Square.Tukiwa ndani ya "Metro" jamaa yangu wa Ghana akachomolewa na "mtoto" ambaye ni kibaka pesa pamoja na saa.

Kijana yule alionekana katika camera na ikaamliwa ashushwe pamoja nasi kuelekea kituo cha polisi.Tukiwa njiani kujongea kituoni,jamaa yangu akawa anamminya minya sana bwana mdogo katika mkono na kiganja,huku amkimvuta kwa nguvu.

Jambo lile lilisababisha matatizo sana kwetu,ilibidi tumlipe tena bwana mdogo kwa kumshika mkono kwa nguvu na kumtendea kinyume na umri wake,japo na yeye alipata "adhabu" iliyotokana na tendo la wizi.

Hili lilikuwa somo kwetu juu ya namna ya kukabili matatizo na tabia za utovu wa nidhamu za watoto.Haiitaji nguvu za jeshi,haiitaji virungu wala mabomu ya machozi.Inahitaji hekima na kuwasikiliza.Huu ndio msingi wa kuwajengea watoto moyo wa kuhoji na kuthubutu.

Mabomu,nguvu,virungu na bakora,ni dalili za Taifa linalotaka kizazi cha kinafiki na cha "ndio mzee".Hizi ni dalili za "ukaburu".Miaka ya 80 tulipokuwa shule tuliambiwa ukaburu sio rangi,bali ni tabia.Tabia ya polisi wa Simiyu inasadifu jina hilo.

Hali ile haina tofauti na kile walichofanyiwa watoto wa Afrika ya Kusini.Watoto wetu walisoma tu ktk vitabu jinsi makaburu walivyouwa na kupiga wanafunzi waliodai haki yao ya msingi ya kupata elimu.Sasa hawasomi tena kati vitabu,bali wanatendewa wao kama walivyotendewa watoto wenzao enzi za "Soweto Massacre".
View attachment 477813 View attachment 477814 View attachment 477815 View attachment 477816 View attachment 477817 View attachment 477818
Unafikiri mbwa aanakili ,ukimwambia shikaaaaa,hata mama yako atamshika na kumng"ata
 
Back
Top Bottom