Ukatili huu uliofanywa na Polisi Simiyu kwa Watoto wa shule, ni aina nyingine ya "ukaburu mamboleo"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Toka jana kumekuwa na picha zinazosambaa zikiwaonyesha polisi wakikabiliana na watoto wa shule (Wanafunzi) huko Bariadi Mkoani Simiyu.

Watoto walioandamana kuelezea hisia zao juu ya kutokukubaliana na kuhamishwa kwa mwalimu wao waliompenda na kumuelewa,hawakumtaka Mwalimu mpya ambaye kwa utashi wao wanaona hakidhi viwango vya aliyemtangulia.

Tunaweza tusikubaliane na hitaji lao,lakini tuna wajibu wa kuheshimu malalamiko yao na kuwasilikiza.Hata kama hatutatimiza haja za mioyo yao,lakini tunapaswa kuwasikiliza watoto hawa kwa kile wanachokileza.

Haikuitajika nguvu kubwa ya kiasi kile kukabiliana na watoto wanaoanza kuelezea hisia zao za kutokukubaliana na uhamisho wa mwalimu wao.

Hii ilikuwa ni haki yao ya msingi,haki ya kuandamana na kukusanyika kuelezea hisia zao.Maandamano ya watoto hawa hayakuwa na fujo wala vurugu,wala hawakuvunja na kuumiza mtu.Waliandamana kwa upole,wakiwa na mabango na kwa kuimba nyimbo za staha kuelezea hisia zao.

Hii ni elimu waliyoipata darasani katika Somo la "Civics".Kidato cha pili na kuendelea wanafundishwa juu ya "Demokrasia na Haki za Binadamu".Kwa uelewa wao,ile ilikuwa ni namna ya kuonyesha walivyoelewa somo la Civics.

Mamlaka husika walipaswa kuwasikiliza,sababu walianza kuelekea ofisi za halmashauri kwa DED walizuiwa,wakaamua kuelekea kwa RC nako wakazuiwa.Huku kote walipita bila kufanya fujo.Viongozi wenye hekima na nuru ya kibaba/mama wangewasikiliza na kuwapa muongozo.

Lakini matokeo yake wamepiga na kuwajeruhi.Kwa miaka ya leo,watoto wengi wa sekondari ni chini ya miaka 20.Hawa ni wa kuwaelekeza na si kuwapiga na mabomu.Hawa ni wa kuwaongoza na kuwashauri na si kuwapiga virungu.Huwezi kumdhibiti mtoto wa chini ya miaka 20 kwa kutumia polisi 4.Huu si uungwana.

Viongozi wa mkoa wa serikali na polisi katika mkoa huu wametia aibu sana.Kwanini wanatengeneza kizazi cha kinafiki?kwanini wasiruhusu watoto wanaohoji?Hivi kunatengenezwa Taifa lipi la kutumia nguvu nyingi kwa jambo dogo??

Halafu polisi hawana uwezo wa kujua huyu ni mtoto?Haki za watoto kama hawa kubebwa juujuu na kudhalilishwa nani anapaswa kuwajibika?Je nguvu zilizotumika zinalingana na madhara waliyosababisha sbb ya maandamano yao?Kwa hatua zile,hatuoni kuwa tunatengeneza kizazi cha kisasi na chuki?

Watoto huongozwa,watoto hulindwa na watoto hutunzwa na kuelekezwa.Tusiwatendee watoto wadogo kama vile ni watu wazima.

Miaka kadhaa iliyopita nilijifunza jinsi nchi za wenzetu wanavyojali watoto na namna ya kuwaadhibu hata kama wamekosa.

Tulikuwa na rafiki yangu katika mji mkuu Rome-Italia,wakati huo kukiwa na wakimbizi wengi kutoka Ulaya Mashariki,wakiwemo watoto wengi wanaouuza miili yao na vijana ambao ni "vibaka"

Tunakatiza katika "Metro" kutoka mjini kati Rome Termini via Ottaviano S Pietro kuelekea St.Peter's Square.Tukiwa ndani ya "Metro" jamaa yangu wa Ghana akachomolewa na "mtoto" ambaye ni kibaka pesa pamoja na saa.

Kijana yule alionekana katika camera na ikaamliwa ashushwe pamoja nasi kuelekea kituo cha polisi.Tukiwa njiani kujongea kituoni,jamaa yangu akawa anamminya minya sana bwana mdogo katika mkono na kiganja,huku amkimvuta kwa nguvu.

Jambo lile lilisababisha matatizo sana kwetu,ilibidi tumlipe tena bwana mdogo kwa kumshika mkono kwa nguvu na kumtendea kinyume na umri wake,japo na yeye alipata "adhabu" iliyotokana na tendo la wizi.

Hili lilikuwa somo kwetu juu ya namna ya kukabili matatizo na tabia za utovu wa nidhamu za watoto.Haiitaji nguvu za jeshi,haiitaji virungu wala mabomu ya machozi.Inahitaji hekima na kuwasikiliza.Huu ndio msingi wa kuwajengea watoto moyo wa kuhoji na kuthubutu.

Mabomu,nguvu,virungu na bakora,ni dalili za Taifa linalotaka kizazi cha kinafiki na cha "ndio mzee".Hizi ni dalili za "ukaburu".Miaka ya 80 tulipokuwa shule tuliambiwa ukaburu sio rangi,bali ni tabia.Tabia ya polisi wa Simiyu inasadifu jina hilo.

Hali ile haina tofauti na kile walichofanyiwa watoto wa Afrika ya Kusini.Watoto wetu walisoma tu ktk vitabu jinsi makaburu walivyouwa na kupiga wanafunzi waliodai haki yao ya msingi ya kupata elimu.Sasa hawasomi tena kati vitabu,bali wanatendewa wao kama walivyotendewa watoto wenzao enzi za "Soweto Massacre".
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
 
Hao askari hawajipeleki wenyewe hua wanaitwa, hapo aliyewaita ni mztu aliyeheshimiwa akagewa cheo kikubwa hivi kama cha ukuu au ukuu msaidizi wa shule au kitengo cha nidhamu.

Wameshindwa kukaa chini na kuwaelewesha, wameshindwa hata kuwadanganya? Basi wangekaa kimya wawaache wazunguke mtaani kwa sababu mwisho wangetulia tu.

Wameshindwa kutumia akili, wameomba back up ya askari, askari nao ni vilaza kama aliyetoka kuwaita, unadhani itakuaje?
 
Toka jana kumekuwa na picha zinazosambaa zikiwaonyesha polisi wakikabiliana na watoto wa shule (Wanafunzi) huko Bariadi Mkoani Simiyu.

Watoto walioandamana kuelezea hisia zao juu ya kutokukubaliana na kuhamishwa kwa mwalimu wao waliompenda na kumuelewa,hawakumtaka Mwalimu mpya ambaye kwa utashi wao wanaona hakidhi viwango vya aliyemtangulia.

Tunaweza tusikubaliane na hitaji lao,lakini tuna wajibu wa kuheshimu malalamiko yao na kuwasilikiza.Hata kama hatutatimiza haja za mioyo yao,lakini tunapaswa kuwasikiliza watoto hawa kwa kile wanachokileza.

Haikuitajika nguvu kubwa ya kiasi kile kukabiliana na watoto wanaoanza kuelezea hisia zao za kutokukubaliana na uhamisho wa mwalimu wao.

Hii ilikuwa ni haki yao ya msingi,haki ya kuandamana na kukusanyika kuelezea hisia zao.Maandamano ya watoto hawa hayakuwa na fujo wala vurugu,wala hawakuvunja na kuumiza mtu.Waliandamana kwa upole,wakiwa na mabango na kwa kuimba nyimbo za staha kuelezea hisia zao.

Hii ni elimu waliyoipata darasani katika Somo la "Civics".Kidato cha pili na kuendelea wanafundishwa juu ya "Demokrasia na Haki za Binadamu".Kwa uelewa wao,ile ilikuwa ni namna ya kuonyesha walivyoelewa somo la Civics.

Mamlaka husika walipaswa kuwasikiliza,sababu walianza kuelekea ofisi za halmashauri kwa DED walizuiwa,wakaamua kuelekea kwa RC nako wakazuiwa.Huku kote walipita bila kufanya fujo.Viongozi wenye hekima na nuru ya kibaba/mama wangewasikiliza na kuwapa muongozo.

Lakini matokeo yake wamepiga na kuwajeruhi.Kwa miaka ya leo,watoto wengi wa sekondari ni chini ya miaka 20.Hawa ni wa kuwaelekeza na si kuwapiga na mabomu.Hawa ni wa kuwaongoza na kuwashauri na si kuwapiga virungu.Huwezi kumdhibiti mtoto wa chini ya miaka 20 kwa kutumia polisi 4.Huu si uungwana.

Viongozi wa mkoa wa serikali na polisi katika mkoa huu wametia aibu sana.Kwanini wanatengeneza kizazi cha kinafiki?kwanini wasiruhusu watoto wanaohoji?Hivi kunatengenezwa Taifa lipi la kutumia nguvu nyingi kwa jambo dogo??

Halafu polisi hawana uwezo wa kujua huyu ni mtoto?Haki za watoto kama hawa kubebwa juujuu na kudhalilishwa nani anapaswa kuwajibika?Je nguvu zilizotumika zinalingana na madhara waliyosababisha sbb ya maandamano yao?Kwa hatua zile,hatuoni kuwa tunatengeneza kizazi cha kisasi na chuki?

Watoto huongozwa,watoto hulindwa na watoto hutunzwa na kuelekezwa.Tusiwatendee watoto wadogo kama vile ni watu wazima.

Miaka kadhaa iliyopita nilijifunza jinsi nchi za wenzetu wanavyojali watoto na namna ya kuwaadhibu hata kama wamekosa.

Tulikuwa na rafiki yangu katika mji mkuu Rome-Italia,wakati huo kukiwa na wakimbizi wengi kutoka Ulaya Mashariki,wakiwemo watoto wengi wanaouuza miili yao na vijana ambao ni "vibaka"

Tunakatiza katika "Metro" kutoka mjini kati Rome Termini via Ottaviano S Pietro kuelekea St.Peter's Square.Tukiwa ndani ya "Metro" jamaa yangu wa Ghana akachomolewa na "mtoto" ambaye ni kibaka pesa pamoja na saa.

Kijana yule alionekana katika camera na ikaamliwa ashushwe pamoja nasi kuelekea kituo cha polisi.Tukiwa njiani kujongea kituoni,jamaa yangu akawa anamminya minya sana bwana mdogo katika mkono na kiganja,huku amkimvuta kwa nguvu.

Jambo lile lilisababisha matatizo sana kwetu,ilibidi tumlipe tena bwana mdogo kwa kumshika mkono kwa nguvu na kumtendea kinyume na umri wake,japo na yeye alipata "adhabu" iliyotokana na tendo la wizi.

Hili lilikuwa somo kwetu juu ya namna ya kukabili matatizo na tabia za utovu wa nidhamu za watoto.Haiitaji nguvu za jeshi,haiitaji virungu wala mabomu ya machozi.Inahitaji hekima na kuwasikiliza.Huu ndio msingi wa kuwajengea watoto moyo wa kuhoji na kuthubutu.

Mabomu,nguvu,virungu na bakora,ni dalili za Taifa linalotaka kizazi cha kinafiki na cha "ndio mzee".Hizi ni dalili za "ukaburu".Miaka ya 80 tulipokuwa shule tuliambiwa ukaburu sio rangi,bali ni tabia.Tabia ya polisi wa Simiyu inasadifu jina hilo.

Hali ile haina tofauti na kile walichofanyiwa watoto wa Afrika ya Kusini.Watoto wetu walisoma tu ktk vitabu jinsi makaburu walivyouwa na kupiga wanafunzi waliodai haki yao ya msingi ya kupata elimu.Sasa hawasomi tena kati vitabu,bali wanatendewa wao kama walivyotendewa watoto wenzao enzi za "Soweto Massacre".
View attachment 477813 View attachment 477814 View attachment 477815 View attachment 477816 View attachment 477817 View attachment 477818
Hicho ndo chama chetu katika uhalisia wake
 
Nadhani mazingira nayo yamechangia , maana taarifa za dunia zinaonyesha kwamba , kanda ya ziwa hasa Simiyu , Geita , Shinyanga na Mwanza ndio eneo linaloongoza kwa ukatili duniani , ikifuatiwa kwa mbali na Mogadishu .

Eneo hili ndio waanzilishi wa mauaji ya Albino africa na ndio sehemu aliuawa mwanasiasa mashuhuri Alphonce Mawazo bila hata polisi kujishughulisha .

Sasa kama na polisi nayo imengia kwenye ukatili basi tunaelekea kuvunja rekodi ya dunia .
 
Siku zote baadhi ya wachunga ng'ombe wanakua na roho za kikatili saana
 
Duh asee watu hawana akili kabisa hata kidogo yani.

Hivi hao ma FFU wanakuwaga maroboti au? Hata kama umepewa ruhusa na mkuu wa kazi kuna mambo mengine ni ufara sana kuyafanya. Mungu awasaidie angalau wapate chembe ya hekima na uwezo wa kufikiri
Tena hao polisi hajafanya nnvyotaka, panya rodi ndo huwa wanaanzia huko huko, hiyo picha dogo anakimbia ilibidi kamanda aonekane anapiga bonge moja la kwanja, yaani kwanja ikibidi hata la kilo 8
 
Na ukute hao ni polisi wenye elimu ya Form four, six, nitashangaa kama Polisi mwenye degree yake aliyoipata kwa kusota darasani atakimbizana na vitoto hivo.

Yaan Polisi wa Tanzania wenyewe wanachojua cha kwanza ni "FORCE" siyo "AKILI Kwanza" mtu badala utumie akili kutatua tatizo, wewe unatumia nguvu moja kwa moja kama mbinu yako ya kwanza, sasa hiyo mbinu ikishindikana ndipo wanatumia akili sasa za kuwaomba wanafunzi wakae wazungumze...

Hii imenikumbusha MBEYA, Mpambano wa POLISI na MACHINGA mwaka juzi, yaan polisi walipofika tu eneo la tukio wao moja kwa moja wakaanza kutumia nguvu, waliposhindwa ndipo wakamuomba Mbunge SUGU aje azungumze na wananchi ili mambo yaishe....hii ndio akili ya POLISI waliofundishwa CCP-MOSHI...

Tunahitaji IGP mpya mwenye weledi wa hali ya juu aje akemee MAKAMANDA wote wa polisi nchini, nguvu itumike kama kuna hatari Fulani, sasa tukio la jana kulikuwa na hatari gani?
 
Back
Top Bottom