Ukatili huu uliofanywa na Polisi Simiyu kwa Watoto wa shule, ni aina nyingine ya "ukaburu mamboleo"

Apo wengine wanataka wapandishe vyeo

Wengine wananjaa

Mwingine kagombana na mke wake kisa kanyimwa papuchi

Alaf eti mwanafunzi wa form two b unagoma......f46ckn kweli unajua haki wewe unakula virungu tuu
 
Kama hawataki kutii sheria bila shuruti,unategemea nn?
Wapigwe tu.
Ndo maana tunapambana na dawa za kulevya kwa nguvu zote.

Watoto wenye maadili hawezi fikia hatua ya kukurupushana na askari.
Ninacho fahamu mimi askari wana mafunzo ya ku deal na uhalifu,tusiwakatishe tamaa.

Tuwakanye watoto wetu.

Tukichukulia kila jambo ni siasa hatutafika
 
Inauma saaaaana ila Wallah mimi nimeshaapa siku ikitokea tena wakanifanyia uonevu basi naanza ktubu kabis akuwa sitaweza kuwa na uvumilivu tena. Nasema sitaweza kuwa na uvumilivu tu
Mkuu, kwani waliwahi kukusulubu?
 
Wakiambiwa wapele vijana angalau wenye degree kwenye mafunzo ya polisi ili angalau kabla hujafanya maamuzi u reason kidogo. Wenyewe wanawajaza kina bashite huko kitu kidogo tu wanatumia nguvu kubwa.Polisi wetu mnatia kitendo kile
 
Ndo maana nilipost kuwa nina wasiwasi na uwezo wa askari mmojawapo akimfukuza mwanafunzi... Uwezo niliomaanisha hapo ni ufikiri wake. Hapakuwa na haja ya kutumia nguvu yote hiyo kwa mtoto kama huyo
 
Sisi waafrika niwapumbavu sanaaa. mbona tunakuwa kama hatujawa civilized au nikukosa elimu ya kibinadamu tunakuwa wanyama kiasi hiki, mwanafunzi mdogo hv unampiga kibano kama mtu mzima, kuna vitu vingine we have to think beyond sio kisa ww ni polisi basi una mamlaka yakupiga tu, Kumbuka kuwa polisi kaz yake kuu nikulinda mwananchi na malizake sasa huku kwenda kupiga watu anapata wap haya mamlka, guys me am just Tired with how african especially Tanzania governed us. We have to make this things hapen KATIBA i think Kidogo Hii Itapunguza Makali now we have Educated Leader Na wengi wao Wapo Opposition Party Naamini They will Make Tanzania A better place. Sio kwa kuonewa huku khaaaaaa...
 
Hiv hao maaskari hao si watoto wao kabisa wa kuwazaa hawana hata huruma na wakat watoto walikua na nie njema kabisa ya kuandamana?
 
Inasikitisha sana ....Wale watoto tuliambiwa Ni taifa la kesho Naona Leo wamekua na wamefikia kupigwa virungu ....Kazi ya upolisi imelaaniwa
 
Ndo maana uwezo wetu inatiliwa mashaka sana popote kwa watu waliostaarabika kuanzia elimu yetu tunayoipata hadi tabia zetu na hii si kwamba elimu yetu ni mbaya bali matendo yetu ndo yanatambulisha kuwa huko vyuoni labda tunasomea degree za ujinga. Na huu ni uthibitisho kuwa tupo hivyo na ndani ya vichwa vyetu kina nazi wazi tu.

Tunadharaulika Africa kutokana na watu wachache wenye roho mbaya, wivu kufikiri na watumwa kifikra.
 
Toka jana kumekuwa na picha zinazosambaa zikiwaonyesha polisi wakikabiliana na watoto wa shule (Wanafunzi) huko Bariadi Mkoani Simiyu.

Watoto walioandamana kuelezea hisia zao juu ya kutokukubaliana na kuhamishwa kwa mwalimu wao waliompenda na kumuelewa,hawakumtaka Mwalimu mpya ambaye kwa utashi wao wanaona hakidhi viwango vya aliyemtangulia.

Tunaweza tusikubaliane na hitaji lao,lakini tuna wajibu wa kuheshimu malalamiko yao na kuwasilikiza.Hata kama hatutatimiza haja za mioyo yao,lakini tunapaswa kuwasikiliza watoto hawa kwa kile wanachokileza.

Haikuitajika nguvu kubwa ya kiasi kile kukabiliana na watoto wanaoanza kuelezea hisia zao za kutokukubaliana na uhamisho wa mwalimu wao.

Hii ilikuwa ni haki yao ya msingi,haki ya kuandamana na kukusanyika kuelezea hisia zao.Maandamano ya watoto hawa hayakuwa na fujo wala vurugu,wala hawakuvunja na kuumiza mtu.Waliandamana kwa upole,wakiwa na mabango na kwa kuimba nyimbo za staha kuelezea hisia zao.

Hii ni elimu waliyoipata darasani katika Somo la "Civics".Kidato cha pili na kuendelea wanafundishwa juu ya "Demokrasia na Haki za Binadamu".Kwa uelewa wao,ile ilikuwa ni namna ya kuonyesha walivyoelewa somo la Civics.

Mamlaka husika walipaswa kuwasikiliza,sababu walianza kuelekea ofisi za halmashauri kwa DED walizuiwa,wakaamua kuelekea kwa RC nako wakazuiwa.Huku kote walipita bila kufanya fujo.Viongozi wenye hekima na nuru ya kibaba/mama wangewasikiliza na kuwapa muongozo.

Lakini matokeo yake wamepiga na kuwajeruhi.Kwa miaka ya leo,watoto wengi wa sekondari ni chini ya miaka 20.Hawa ni wa kuwaelekeza na si kuwapiga na mabomu.Hawa ni wa kuwaongoza na kuwashauri na si kuwapiga virungu.Huwezi kumdhibiti mtoto wa chini ya miaka 20 kwa kutumia polisi 4.Huu si uungwana.

Viongozi wa mkoa wa serikali na polisi katika mkoa huu wametia aibu sana.Kwanini wanatengeneza kizazi cha kinafiki?kwanini wasiruhusu watoto wanaohoji?Hivi kunatengenezwa Taifa lipi la kutumia nguvu nyingi kwa jambo dogo??

Halafu polisi hawana uwezo wa kujua huyu ni mtoto?Haki za watoto kama hawa kubebwa juujuu na kudhalilishwa nani anapaswa kuwajibika?Je nguvu zilizotumika zinalingana na madhara waliyosababisha sbb ya maandamano yao?Kwa hatua zile,hatuoni kuwa tunatengeneza kizazi cha kisasi na chuki?

Watoto huongozwa,watoto hulindwa na watoto hutunzwa na kuelekezwa.Tusiwatendee watoto wadogo kama vile ni watu wazima.

Miaka kadhaa iliyopita nilijifunza jinsi nchi za wenzetu wanavyojali watoto na namna ya kuwaadhibu hata kama wamekosa.

Tulikuwa na rafiki yangu katika mji mkuu Rome-Italia,wakati huo kukiwa na wakimbizi wengi kutoka Ulaya Mashariki,wakiwemo watoto wengi wanaouuza miili yao na vijana ambao ni "vibaka"

Tunakatiza katika "Metro" kutoka mjini kati Rome Termini via Ottaviano S Pietro kuelekea St.Peter's Square.Tukiwa ndani ya "Metro" jamaa yangu wa Ghana akachomolewa na "mtoto" ambaye ni kibaka pesa pamoja na saa.

Kijana yule alionekana katika camera na ikaamliwa ashushwe pamoja nasi kuelekea kituo cha polisi.Tukiwa njiani kujongea kituoni,jamaa yangu akawa anamminya minya sana bwana mdogo katika mkono na kiganja,huku amkimvuta kwa nguvu.

Jambo lile lilisababisha matatizo sana kwetu,ilibidi tumlipe tena bwana mdogo kwa kumshika mkono kwa nguvu na kumtendea kinyume na umri wake,japo na yeye alipata "adhabu" iliyotokana na tendo la wizi.

Hili lilikuwa somo kwetu juu ya namna ya kukabili matatizo na tabia za utovu wa nidhamu za watoto.Haiitaji nguvu za jeshi,haiitaji virungu wala mabomu ya machozi.Inahitaji hekima na kuwasikiliza.Huu ndio msingi wa kuwajengea watoto moyo wa kuhoji na kuthubutu.

Mabomu,nguvu,virungu na bakora,ni dalili za Taifa linalotaka kizazi cha kinafiki na cha "ndio mzee".Hizi ni dalili za "ukaburu".Miaka ya 80 tulipokuwa shule tuliambiwa ukaburu sio rangi,bali ni tabia.Tabia ya polisi wa Simiyu inasadifu jina hilo.

Hali ile haina tofauti na kile walichofanyiwa watoto wa Afrika ya Kusini.Watoto wetu walisoma tu ktk vitabu jinsi makaburu walivyouwa na kupiga wanafunzi waliodai haki yao ya msingi ya kupata elimu.Sasa hawasomi tena kati vitabu,bali wanatendewa wao kama walivyotendewa watoto wenzao enzi za "Soweto Massacre".
View attachment 477813 View attachment 477814 View attachment 477815 View attachment 477816 View attachment 477817 View attachment 477818
sasa tunalalamika kuwa hatun wakimbiaji wazuri wa mbio huyu anaemkimbiza dent c bora aingie kwenye mbio za marathon aiseee
 
Duh asee watu hawana akili kabisa hata kidogo yani.

Hivi hao ma FFU wanakuwaga maroboti au? Hata kama umepewa ruhusa na mkuu wa kazi kuna mambo mengine ni ufara sana kuyafanya. Mungu awasaidie angalau wapate chembe ya hekima na uwezo wa kufikiri
Wengi wao ni Daudi Bashite, form four failier unategemea nini?
 
Huyu Philip Lutema alikuwa Mkuu wa shule hiyo ikamshinda akahamishiwa shule Nyingine. Sasa kinachomrudisha hapo ni nini? Nafikiri uongozi uangalie upya kwa nini alitolewa miaka miwili tu Leo wanamrudisha.
 
Na madawa ya kulevya wanatumia au? maana wananchi wanapenda siku hizi watoto waumizwe tu.
 
Toka jana kumekuwa na picha zinazosambaa zikiwaonyesha polisi wakikabiliana na watoto wa shule (Wanafunzi) huko Bariadi Mkoani Simiyu.

Watoto walioandamana kuelezea hisia zao juu ya kutokukubaliana na kuhamishwa kwa mwalimu wao waliompenda na kumuelewa,hawakumtaka Mwalimu mpya ambaye kwa utashi wao wanaona hakidhi viwango vya aliyemtangulia.

Tunaweza tusikubaliane na hitaji lao,lakini tuna wajibu wa kuheshimu malalamiko yao na kuwasilikiza.Hata kama hatutatimiza haja za mioyo yao,lakini tunapaswa kuwasikiliza watoto hawa kwa kile wanachokileza.

Haikuitajika nguvu kubwa ya kiasi kile kukabiliana na watoto wanaoanza kuelezea hisia zao za kutokukubaliana na uhamisho wa mwalimu wao.

Hii ilikuwa ni haki yao ya msingi,haki ya kuandamana na kukusanyika kuelezea hisia zao.Maandamano ya watoto hawa hayakuwa na fujo wala vurugu,wala hawakuvunja na kuumiza mtu.Waliandamana kwa upole,wakiwa na mabango na kwa kuimba nyimbo za staha kuelezea hisia zao.

Hii ni elimu waliyoipata darasani katika Somo la "Civics".Kidato cha pili na kuendelea wanafundishwa juu ya "Demokrasia na Haki za Binadamu".Kwa uelewa wao,ile ilikuwa ni namna ya kuonyesha walivyoelewa somo la Civics.

Mamlaka husika walipaswa kuwasikiliza,sababu walianza kuelekea ofisi za halmashauri kwa DED walizuiwa,wakaamua kuelekea kwa RC nako wakazuiwa.Huku kote walipita bila kufanya fujo.Viongozi wenye hekima na nuru ya kibaba/mama wangewasikiliza na kuwapa muongozo.

Lakini matokeo yake wamepiga na kuwajeruhi.Kwa miaka ya leo,watoto wengi wa sekondari ni chini ya miaka 20.Hawa ni wa kuwaelekeza na si kuwapiga na mabomu.Hawa ni wa kuwaongoza na kuwashauri na si kuwapiga virungu.Huwezi kumdhibiti mtoto wa chini ya miaka 20 kwa kutumia polisi 4.Huu si uungwana.

Viongozi wa mkoa wa serikali na polisi katika mkoa huu wametia aibu sana.Kwanini wanatengeneza kizazi cha kinafiki?kwanini wasiruhusu watoto wanaohoji?Hivi kunatengenezwa Taifa lipi la kutumia nguvu nyingi kwa jambo dogo??

Halafu polisi hawana uwezo wa kujua huyu ni mtoto?Haki za watoto kama hawa kubebwa juujuu na kudhalilishwa nani anapaswa kuwajibika?Je nguvu zilizotumika zinalingana na madhara waliyosababisha sbb ya maandamano yao?Kwa hatua zile,hatuoni kuwa tunatengeneza kizazi cha kisasi na chuki?

Watoto huongozwa,watoto hulindwa na watoto hutunzwa na kuelekezwa.Tusiwatendee watoto wadogo kama vile ni watu wazima.

Miaka kadhaa iliyopita nilijifunza jinsi nchi za wenzetu wanavyojali watoto na namna ya kuwaadhibu hata kama wamekosa.

Tulikuwa na rafiki yangu katika mji mkuu Rome-Italia,wakati huo kukiwa na wakimbizi wengi kutoka Ulaya Mashariki,wakiwemo watoto wengi wanaouuza miili yao na vijana ambao ni "vibaka"

Tunakatiza katika "Metro" kutoka mjini kati Rome Termini via Ottaviano S Pietro kuelekea St.Peter's Square.Tukiwa ndani ya "Metro" jamaa yangu wa Ghana akachomolewa na "mtoto" ambaye ni kibaka pesa pamoja na saa.

Kijana yule alionekana katika camera na ikaamliwa ashushwe pamoja nasi kuelekea kituo cha polisi.Tukiwa njiani kujongea kituoni,jamaa yangu akawa anamminya minya sana bwana mdogo katika mkono na kiganja,huku amkimvuta kwa nguvu.

Jambo lile lilisababisha matatizo sana kwetu,ilibidi tumlipe tena bwana mdogo kwa kumshika mkono kwa nguvu na kumtendea kinyume na umri wake,japo na yeye alipata "adhabu" iliyotokana na tendo la wizi.

Hili lilikuwa somo kwetu juu ya namna ya kukabili matatizo na tabia za utovu wa nidhamu za watoto.Haiitaji nguvu za jeshi,haiitaji virungu wala mabomu ya machozi.Inahitaji hekima na kuwasikiliza.Huu ndio msingi wa kuwajengea watoto moyo wa kuhoji na kuthubutu.

Mabomu,nguvu,virungu na bakora,ni dalili za Taifa linalotaka kizazi cha kinafiki na cha "ndio mzee".Hizi ni dalili za "ukaburu".Miaka ya 80 tulipokuwa shule tuliambiwa ukaburu sio rangi,bali ni tabia.Tabia ya polisi wa Simiyu inasadifu jina hilo.

Hali ile haina tofauti na kile walichofanyiwa watoto wa Afrika ya Kusini.Watoto wetu walisoma tu ktk vitabu jinsi makaburu walivyouwa na kupiga wanafunzi waliodai haki yao ya msingi ya kupata elimu.Sasa hawasomi tena kati vitabu,bali wanatendewa wao kama walivyotendewa watoto wenzao enzi za "Soweto Massacre".
View attachment 477813 View attachment 477814 View attachment 477815 View attachment 477816 View attachment 477817 View attachment 477818
Ni jambo la kusikitisha sana sikutegemea Tanzania inaweza ikatokea kitu kama hiki. Nawapa pole wanafunzi na wazazi wao.
 
Back
Top Bottom