storyteller
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 1,544
- 1,874
Hii ilikua kwa ajili ya mvua, ila zikiisha biashara itarud pale pale kwenye peak.Wakuu , hii mnaweza kuiona kama Masihara vile , lakini uchunguzi nilioufanya jijini DSM , Jiji linaloaminika kuongoza kwa unywaji wa maji ya chupa ( maji safi ) , unaonyesha kwamba biashara ya maji imeanza kudoda kwa kasi ya kutisha !
Kwanza kwa kipindi cha mwaka mzima maji hayo hayajawahi kuadimika sokoni kama miaka ya nyuma , hali ni mbaya kiasi cha kusababisha magari ya makampuni karibu yote yanayotengeneza maji kupishana na kushinda mitaani yakisaka wateja , mithili ya Wanasiasa wanaoomba kura za ubunge majimboni .
Si kwamba watu hawanywi maji , la hasha ! Ugunduzi wangu umebaini kwamba watu wengi wanabeba maji ya Dawasco yaliyochemshwa ili kupunguza gharama , Hakika hali ni mbaya mno !
Ushauri wangu ni kwamba , maendeleo ya viwanda yaendane na vipato vya wananchi , viwanda vya maji vikifungwa kwa kukosa soko tutapoteza sana chanzo cha ajira ya vijana wengi mno .
Wabongo sio kwamba tunapenda kununua maji ya dukani, ila kwa kuwa maji ya bomba maeneo mengi yana chumvi sana, unakunywa km unameza dawa, so, mtu anaamua anunue tu ya dukani.
Kitonga muhimu mkuu.