Uzushi uliozushwa katikati ya kilele cha maandamano

Uzushi uliozushwa katikati ya kilele cha maandamano

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,042
Reaction score
871,166
Jioni ya tarehe 29. 10. 2025 Bali ilikuwa mbaya sana kwenye miji mingi mikuu Tanganyika.. Maandamano yaliyoambatana na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu yalikuwa yamepamba moto

Mawasiliano yalikuwa ya shida kwakuwa mitandao ilikuwa imezimwa na mamlaka zikakosa kujua athari za ueneaji wa habari ni kubwa kiasi gani ama watu wanawasiliana kwa haraka kiasi gani na kwa njia zipi

Kama mtandao ungekuwepo ilikuwa ni rahisi Ku 'monitor' usambaaji wa habari. Sasa inawezekana kabisa ilikuwa ni lazima kitafutwe kitu cha kuweza kujua bila kutumia mitandao ya data
Kizushwe kitu ama jambo na kuona litawafikia wengi kwa haraka kiasi gani.. Kwa maoni yangu haya mambo mawili ndio yalizushwa na yakaenea kwa kadi kama moto wa kimbunga kwenye msitu mkavu
1. Maji ya DAWASCO/DAWASA kutiwa sumu
2. Kupatikana kwa Balozi
Humphrey Polepole

Ndani ya chini ya saa 24 zaidi ya nusu ya Watanganyika walikuwa wameshapata hizi habari kupitia jumbe fupi na kupigiana simu.. Jibu likapatikana haraka kwamba licha ya kuzima mtandao data lakini bado watu waliweza kuwasiliana kwa haraka
Kilichofuata no TBC kukanusha kwa haraka ishu ya maji kutiwa sumu huku ishu ya kupatikana Polepole wakipiga kimya

Pamoja na kutaka pengine kujua nguvu ya ueneaji wa habari lakini pia pengine lazima ilikuwa kitafutwe kitu cha kufanya distraction kwenye maandanano.. Kwamba badala ya kujadili maandamano basi yajadiliwe mengine

Japo ishu ya maji kutiwa sumu ilikuwa ni uzushi.. Lakini jambo hili hutumika kama silaha mbadala wakati wa vita.. Lakini si kama ilivyozushwa hapa

Wenzetu zamani waliweza kufanya hivyo kwenye visima vya maji ambavyo vinatumiwa na kundi 'specific' la watu.. Hasa kwenye vita vya taifa na taifa, dini na dini ama kabila na kabila

Kwetu ilikuwa ni ngumu kufanya hivyo kwa sababu
1. Hatukuwa vitani
2. Chanzo cha maji hakikuwa kisima
Mto Ruvu ndio chanzo kikubwa cha maji ya Dar na Pwani kinachozalisha lita million 685 za maji safi na salama kwa siku

Kuweza kuyatia sumu maji yanayotiririka na ya ujazo huo inahitaji uwekezaji mkubwa mno wa muda, miundombinu na pesa
Kwa uzalishaji wa lita 685,000 kea siku hata uweke pipa 6 za sumu kali madhara yanaweza yakawa madogo mno!
Kwahiyo kwa tafakuri ya haraka huo uzushi haukukidhi viwango

Kuhusu Pole pole kila mtu alikuwa anaongea lake.. Uzushi mwingine mwingi ulitengenezwa lakini zilizobamba zilikuwa hizi mbili
 
Yule mzee wa 'Gari ni injini sio bodi'eti nasikia alivuliwa nguo kabla ya nyumba yake kutiwa kiberiti ni kweli nyie wana Bunda?
 
-Chura na hawara yake wamekimbia nchi
-Maandamano yanaelekea ikulu kumtoa chura
-domo alimficha abdu
- Polepole katobolewa macho na kung'olewa meno
maridhiano yanafanyika jeshi kuchukua nchi
Kiufupi umbea tulipiga na shangwe lilikuwepo la kutosha
 
-Chura na hawara yake wamekimbia nchi
-Maandamano yanaelekea ikulu kumtoa chura
-domo alimficha abdu
- Polepole katobolewa macho na kung'olewa meno
maridhiano yanafanyika jeshi kuchukua nchi
Kiufupi umbea tulipiga na shangwe lilikuwepo la kutosha
Pole pole katelekezwa Airport
Pole pole kaokotwa kigamboni
Pole pole ksokotwa coco beach hajiwezi
Pole pole kaokotwa ununio hana macho
Nuumbani kwa akina Polepole watu wanalia
Pole pole kafa
 
MaCCM ni mauaji, hilo watanzania hatuwezi samee.

Ni swala la kujipanga kulipa kisasi chetu.

Sio rahisi vile, lakini huu ushe.nzi waliofanya hatuwezi sahau kamwe.

Hatuwezi sahau, wala samehe.

Fucc CCM na yeyote wenye vinasaba na hiko chama.

Ukatili waliofanya kwa uchu wa madaraka watanzania hatuwezi samehe kamwe.?
 
Uzushi mwingine ni jeshi la wananchi linalinda raia
Hii kwa kiasi fulani walifanya pale mwanzoni, vijana wengi wa boda pale Kinyerezi wanasimulia jinsi wenzao walivyoshushwa kutoka kwa gari ya polisi na wanajeshi, wakawaambia waende zao, nadhani hapa ndio Mkunda akaambiwa akome polisi wafanye yao.
 
Uzushi ulikuwa mwingi tu aisee 😅😅
Askari wa Uganda wameiteka Bukoba
Polepole kudanja
Viongozi kukutwa airport wanakimbia nchi
Shilole kudanja kwa presha baada ya kuchomewa mgahawa wake
Ponjoro kula shaba
 
Hii kwa kiasi fulani walifanya pale mwanzoni, vijana wengi wa boda pale Kinyerezi wanasimulia jinsi wenzao walivyoshushwa kutoka kwa gari ya polisi na wanajeshi, wakawaambia waende zao, nadhani hapa ndio Mkunda akaambiwa akome polisi wafanye yao.
Lazima tuanze upya.

CCM aisameheleki kamwe.
 
Imebidi tu nicheke.. Kama sio hii video ningesema ni AI au ni uzushi mwingine
 
Back
Top Bottom