Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 126,599
- 241,418
Wakuu , hii mnaweza kuiona kama Masihara vile , lakini uchunguzi nilioufanya jijini DSM , Jiji linaloaminika kuongoza kwa unywaji wa maji ya chupa ( maji safi ) , unaonyesha kwamba biashara ya maji imeanza kudoda kwa kasi ya kutisha !
Kwanza kwa kipindi cha mwaka mzima maji hayo hayajawahi kuadimika sokoni kama miaka ya nyuma , hali ni mbaya kiasi cha kusababisha magari ya makampuni karibu yote yanayotengeneza maji kupishana na kushinda mitaani yakisaka wateja , mithili ya Wanasiasa wanaoomba kura za ubunge majimboni .
Si kwamba watu hawanywi maji , la hasha ! Ugunduzi wangu umebaini kwamba watu wengi wanabeba maji ya Dawasco yaliyochemshwa ili kupunguza gharama , Hakika hali ni mbaya mno !
Ushauri wangu ni kwamba , maendeleo ya viwanda yaendane na vipato vya wananchi , viwanda vya maji vikifungwa kwa kukosa soko tutapoteza sana chanzo cha ajira ya vijana wengi mno .