Ukarabati wa nyufa za majengo ya UDSM waanza

Ukarabati wa nyufa za majengo ya UDSM waanza

Wanaposema hakuna madhara nin maana yake?
Wamekiri wenyewe kuwa yalifanyika makosa halafu wanajitetea kitu gani...
Wawe straight kwenye point, over!!
 
SIKU chache baada ya kusambaa kwa picha zilizoonesha nyufa katika kuta za majengo ya mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), nyufa hizo zimeanza kukarabatiwa

Ukarabati huo unafanyika na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo Desemba 3, mwaka huu picha za nyufa hizo zilisambaa mitandaoni huku Kumbusho Dawson, Mbunge katika serikali ya wanafunzi UDSM (Daruso) alishikiliwa kuhojiwa na baadaye kuachiwa huru na polisi kitengo cha makosa ya mtandao.

Hata hivyo TBA ilitolea ufafanuzi nyufa hizo kupitia Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga na kueleza kuwa kutokea kwa nyufa hizo ni jambo la kawaida na haina madhara.

Majengo hayo ambayo yalijengwa na TBA ambao wameeleza kuwa bado inaangalia dosari nyingine zilizopo katika majengo hayo.

nyufa.jpg
 
Hivi registration bodi ya wahandisi ilizungumza chochote kuhusu hii issue?
 
Mleta Uzi umepata ruhusa ya TBA kupiga picha za ukarabati huo? Namuona Mambosasa anajipanga kutupatia taarifa kuwa "kijana aliyerusha picha za ukarabati ......"
 
Acha kutupa fake news!!......Tokea lini expansion joint zikafanyiwa ukarabati???![emoji32][emoji32][emoji32]
 
Expansion joints cracks toka lini zikafanyiwa ukarabati?! Nchi hii iko na wasomi wapumbavu kupita kiasi, wakati wanahadaa umma kuwa zile zilikuwa ni expansion joints za kawaida ili hali wakijua wanasema uongo ilikuwa kwa manufaa ya nani?! Awamu hii tutashuhudia mengi sana!
 
Kama aliyejenga angekuwa mkandarasi bonafsi, vibali vyake wangekuwa wamevifreeze
 
Sina Hakika Kama Mleta Thread Kwa Attachments Hii Nadhani Wakuu Watakulaumu
 
Wakae wakijua kuna siku wanafunzi watafukiwa humo. Ubovu/uzembe hauko kwenye kuta tu, inawezekana/kuna uwezekano, tena sana uzembe huo upo hata kwenye msingi , waangalie lisije collapse zima! Tunatoa tahadhali!
 
View attachment 650054

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeanza ukarabati wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yenye ufa.

Taarifa za kuwepo nyufa hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa Desemba 3,2017 na baadaye ufafanuzi ulitolewa na TBA.

Uchunguzi uliofanywa na MCL Digital umebaini ukarabati umeanza, huku ikielezwa kuwa hauwaathiri wanafunzi wanaotumia mabweni hayo.

“Ukarabati umeanza, mafundi wanafanya kazi nje ya jengo kwa kuondoa plasta ili kuangalia tatizo liko wapi,” kimesema chanzo cha habari kilichozungumza na MCL Digital.

TBA iliyojenga majengo hayo ambayo bado yako katika usimamizi wake imeelezwa pia inaangalia dosari nyingine zilizopo.

Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga Desemba 4,2017 akizungumzia nyufa zilizoko kwenye jengo la Block A alisema hazina madhara na walizitarajia.

Alisema nyufa katika jengo hilo la hosteli ambalo ni kati ya sita yaliyopo Block A zimetokea eneo walilotarajia ambalo kitaalamu linajulikana (expansion joint) hivyo hazina madhara.

Mwakalinga alisema kwa kawaida udongo unaobeba jengo hutitia baada ya muda fulani, hivyo wakati wa ujenzi huacha nafasi kuliwezesha jengo kupumua bila kusababisha nyufa.

Mwakalinga alisema kuna makosa yalifanyika ya kuziba nafasi zilizoachwa (expansion joint) kwa kutumia saruji badala ya mbao au plastiki maalumu hivyo kuonyesha nyufa kwenye jengo hilo.

Kutokana na kusambaa kwa picha kuonyesha nyufa katika majengo hayo, mbunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Kumbusho Dawson alishikiliwa na polisi kitengo cha makosa ya mtandao kwa kuhojiwa na baadaye aliachiwa.


Muungwana
Ni Architect (Mbunifu majengo)Elius Mwakalinga and not Mhandisi.

Mnatakiwa kuwa na exposure ya professionals duniani
 
Expansion Joints zisizibwe zote kuna joto sana, tuachiwe kidogo nafasi za kupitisha upepo.
 
Back
Top Bottom