Ukarabati wa nyufa za majengo ya UDSM waanza

Ukarabati wa nyufa za majengo ya UDSM waanza

waliziba expansion joint?

kwa hiyo hakukuwa na expansion joint

sasa unakarabati vipi jengo ambalo halina exp joint, unalichana katikati?
Zilikuwepo ila aliepiga plaster alipiga hadi juu ya hizo joints. Ndio maana walivyokwangua zikaonekana zimenyooka tofauti na nyufa za plaster.
 
Zilikuwepo ila aliepiga plaster alipiga hadi juu ya hizo joints. Ndio maana walivyokwangua zikaonekana zimenyooka tofauti na nyufa za plaster.

kwa nini plaster imepata nyufa za kufa mtu?

Na wanaposema expansion joint zilitakiwa zizibwe na mbao kuna maana gani ya kuacha nafasi ya expansion (kupumua wanaita) halafu unaiziba na mbao? Hiyo expansion itatokea vipi sasa?
 
Sasa Kama hizo ni expansion joints kwa nini wanaziba tena? Nyumba itapumulia wapi sasa?
 
kwa nini plaster imepata nyufa za kufa mtu?

Na wanaposema expansion joint zilitakiwa zizibwe na mbao kuna maana gani ya kuacha nafasi ya expansion halafu unaiziba?
Plaster imepata nyufa around expansion joint area.
Kuhusu kwanini waliziba na plaster ndio kwenye hio taarifa WAMEKIRI EXPANSION JOINTS ZILIZIBWA NA SARUJI KIMAKOSA. Hazitakiwi kuzibwa. Btw mimi sio mhandisi
 
Plaster imepata nyufa around expansion joint area.

nyufa zilikuwa zig zag and L-shaped and what not. Hazikuwa straight.

hotel3-jpg.643167


Expansion joint lililopiga kona kwenye concrete slab tunalieleza vipi?

Mbona sio straight?
 
nyufa zilikuwa zig zag and L-shaped and what not. Hazikuwa straight.

hestel2-jpg.643166


Hilo expansion joint lilipiga kona kwenye concrete slab tunalieleza vipi?

Mbona sio straight?
Nyufa zilikuwa zig zag kwasababu zilikuwa kwenye plaster sehemu fulani juu ya expansion joint, ndio maana walikwangua sehemu kubwa kuzunguka expansion joint.
Mwenye picha ya kuonesha palipokwanguliwa sio palipokuwa na nyufa alete updated image. Hakuna.
 
Nyufa zilikuwa zig zag kwasababu zilikuwa kwenye plaster sehemu fulani juu ya expansion joint, ndio maana walikwangua sehemu kubwa kuzunguka expansion joint.
Mwenye picha ya kuonesha palipokwanguliwa sio palipokuwa na nyufa alete updated image. Hakuna.


Okay, unatetea na ku explain away tatizo, lakini baadae unachomoa unasema mi sio engineer.

Kwa nini concrete slab nayo ina nyufa za kufa mtu? Na yenyewe ilijengwa na expansion joints?

Ndani ya hiyo ledge ya concrete slab ambapo kuna nyufa ipo expansion joint ndani?

hotel3-jpg.643167
 
Kumbe ilikua ni expansion joint tu. wabongo bana kwa kukuza mambo.....
 
View attachment 650054

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeanza ukarabati wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yenye ufa.

Taarifa za kuwepo nyufa hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa Desemba 3,2017 na baadaye ufafanuzi ulitolewa na TBA.

Uchunguzi uliofanywa na MCL Digital umebaini ukarabati umeanza, huku ikielezwa kuwa hauwaathiri wanafunzi wanaotumia mabweni hayo.

“Ukarabati umeanza, mafundi wanafanya kazi nje ya jengo kwa kuondoa plasta ili kuangalia tatizo liko wapi,” kimesema chanzo cha habari kilichozungumza na MCL Digital.

TBA iliyojenga majengo hayo ambayo bado yako katika usimamizi wake imeelezwa pia inaangalia dosari nyingine zilizopo.

Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga Desemba 4,2017 akizungumzia nyufa zilizoko kwenye jengo la Block A alisema hazina madhara na walizitarajia.

Alisema nyufa katika jengo hilo la hosteli ambalo ni kati ya sita yaliyopo Block A zimetokea eneo walilotarajia ambalo kitaalamu linajulikana (expansion joint) hivyo hazina madhara.

Mwakalinga alisema kwa kawaida udongo unaobeba jengo hutitia baada ya muda fulani, hivyo wakati wa ujenzi huacha nafasi kuliwezesha jengo kupumua bila kusababisha nyufa.

Mwakalinga alisema kuna makosa yalifanyika ya kuziba nafasi zilizoachwa (expansion joint) kwa kutumia saruji badala ya mbao au plastiki maalumu hivyo kuonyesha nyufa kwenye jengo hilo.

Kutokana na kusambaa kwa picha kuonyesha nyufa katika majengo hayo, mbunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Kumbusho Dawson alishikiliwa na polisi kitengo cha makosa ya mtandao kwa kuhojiwa na baadaye aliachiwa.


Muungwana
Huyu nae hajui sehemu ya kupeleka taarifa. Kaleta Huku.
 
Expansion joint kumbe unaweza zifanyia repair
 
Back
Top Bottom