Ukarabati wa nyufa za majengo ya UDSM waanza

Ukarabati wa nyufa za majengo ya UDSM waanza

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,309
pic+jengo.gif


Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeanza ukarabati wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yenye ufa.

Taarifa za kuwepo nyufa hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa Desemba 3,2017 na baadaye ufafanuzi ulitolewa na TBA.

Uchunguzi uliofanywa na MCL Digital umebaini ukarabati umeanza, huku ikielezwa kuwa hauwaathiri wanafunzi wanaotumia mabweni hayo.

“Ukarabati umeanza, mafundi wanafanya kazi nje ya jengo kwa kuondoa plasta ili kuangalia tatizo liko wapi,” kimesema chanzo cha habari kilichozungumza na MCL Digital.

TBA iliyojenga majengo hayo ambayo bado yako katika usimamizi wake imeelezwa pia inaangalia dosari nyingine zilizopo.

Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga Desemba 4,2017 akizungumzia nyufa zilizoko kwenye jengo la Block A alisema hazina madhara na walizitarajia.

Alisema nyufa katika jengo hilo la hosteli ambalo ni kati ya sita yaliyopo Block A zimetokea eneo walilotarajia ambalo kitaalamu linajulikana (expansion joint) hivyo hazina madhara.

Mwakalinga alisema kwa kawaida udongo unaobeba jengo hutitia baada ya muda fulani, hivyo wakati wa ujenzi huacha nafasi kuliwezesha jengo kupumua bila kusababisha nyufa.

Mwakalinga alisema kuna makosa yalifanyika ya kuziba nafasi zilizoachwa (expansion joint) kwa kutumia saruji badala ya mbao au plastiki maalumu hivyo kuonyesha nyufa kwenye jengo hilo.

Kutokana na kusambaa kwa picha kuonyesha nyufa katika majengo hayo, mbunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Kumbusho Dawson alishikiliwa na polisi kitengo cha makosa ya mtandao kwa kuhojiwa na baadaye aliachiwa.


Muungwana
 
Hata kama expansion joint za kawaida ukarabati ni lazima, si nyufa huwa tunaziona kubwa kwenye nyumba zetu pindi zikijengwa tunaambiwa imepumua na tunatindua kuta kurekebisha sasa kwanini hizo iwe tofauti au kwa vile wajenzi ni TBA
 
Bora wamemwachia kijana huyo Dawson.

Maana mambo ya TBA kusema ni expansion joints and settling na papo hapo wakamkamata huyo mtoto kimenisababishia changamoto sana hapa kwangu na wanetu wawili .

Nyie acheni tu.
 
so hazikuwa expansion joints kwani ? expansion joints zinakarabatiwa tena? duuuuh yule baba alikuwa anatokwa povu maskini sijui kama alikuwa anaelewa anachoongea TBC.
NIKAPATA MSEMO MWINGINE MPIGA PICHA ALIPIGA KWA HILA.......nitaomba mpiga picha anipige kwa hila nijione naonekanaje
 
Mwakalinga alisema kuna makosa yalifanyika ya kuziba nafasi zilizoachwa (expansion joint) kwa kutumia saruji badala ya mbao au plastiki maalumu hivyo kuonyesha nyufa kwenye jengo hilo.
Daaah hii taaluma imevamiwa sasa.....
Sasa litapumuaje hilo jengo sasa kama wanakarabati tena
so hazikuwa expansion joints kwani ? expansion joints zinakarabatiwa tena? duuuuh yule baba alikuwa anatokwa povu maskini sijui kama alikuwa anaelewa anachoongea TBC.
NIKAPATA MSEMO MWINGINE MPIGA PICHA ALIPIGA KWA HILA.......nitaomba mpiga picha anipige kwa hila nijione naonekanaje
Tundu la pumzi linazibwa?
Kwanini mnaziba expansion joints zetu Bwana?

Wamekiri kosa waliziba expansion joints.
 
Back
Top Bottom