Sasa tatizo liko wapi????
tatizo halipo kama hauamini maandiko ya bibilia.
kama kuna mtu angehitaji mabodigadi wa kwanza alikuwa ni Yesu Kristo maana alikuwa anatafutwa kuuawa kila wakati, lakini maisha yake ni kelelezo kwa kila anayemuamini.
Mfalme daudi alikuwa na mabodigadi kama kiongozi wa kisiasa uzia, shama, na jeili. wakati huo huo watumishi wa Mungu manabii zaidi ya kuwa na wasaidizi wa kazi ndogondogo kama elisha na Gehazi. Hawakuwa na mambo hayo maana wao ni mfano hai jinsi Mungu anavyooperate.
mifano:
vijana watukutu walipomcheka elisha anakipara - Dubu walitokea kwa muujiza wakawala wote.
majeshi ya adui yalipotaka kumuua elisha - Mungu aliwapiga upofu.
Petro alipotaka kujifanya bodigadi na kumkata jamaa sikio - yesu alimkemea na kumkataza.
Jeroboam ailipotaka kupiga nabii wa Mungu Mkono uliganda na kukauka.
Kikosi kizima kilipomsogelea elsha kumdhuru - waliuawa wote hadi kikosi kingine kilipoamua kuja kwa unyenyekevu
Mungu aliporuhusu mabaya yawapate akina stephano - walikufa huku wanafuraha wakimuona Mungu,
Paulo na wenzke wamewahi Kupigwa hadi jamaa wakadhani wamekufa. lakini walisimama na kuendelea na majukumu yao.
Mungu anaposema tusimtegemee mwanadamu anamaanisha ananjia maelfu ya kulinda watumishi wake.
Soma bibilia,
wanachokifanya hawa ndugu ni ubinadamu na kumshushia Mungu hadhi. Mungu ni yule yule jana, leo na kesho