Ujumbe mahsusi kwa Wachungaji wenye Mabodigadi

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,454
Reaction score
166,963
Kuna wachungaji na wahubiri wengi leo wanatembea na mabodigadi, hata wakiwa wanahubiri mabodigadi wanawazunguka.

Biblia inasema kwenye kitabu cha Yeremia 17:5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.

HAYO SIO MANENO YANGU, NI YA MUNGU MWENYEWE
 
Hapo unamsema aliyemtukana Pengo
 
Aisee......!!! Hivi pale inakua anajaribu kuonesha kua nae ni muheshimiwa sio? Sasa kwani mtu wa Mungu anahitaji ulinzi wa mwanadamu?

'....Bwana asipoulinda mji, yeye aulindae akesha bure...' Mwisho wa kunukuu.

'....Watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa..........' wisho wa kunukuu.

'....za kuambiwa changanya na za kwako......' Mwisho wa kunukuu.
 
Mbona wachungaji wetu(KKKT)hawana walinzi???kwanini unafanya kazi ya mungu alafu unahofu??
 
Umesema sahihi sana. Wako watu wengi, hapo huhudhuria ibada, lakini mioyo yao iko mbali na Mungu. Ni jambo zuri kukumbushana, katika kila connection tunazokuwa nazo ambazo tunaona kabisa zinaweza kutumika kama mkono wa Mungu kutuvusha katika hali moja kwenda nyingine, tusije kujisahau na kuhamisha matumani yetu kutoka kwa Mungu.

Ni kweli kumwacha Mungu kwa sababu tunawanadamu wanaotuhudumia ni kutafuta laana kwa Mungu. NI vizuri kukumbushana kwamba pamoja na walinzi hao, tusimwache Mungu akawa nje ya mioyo yetu.

"Bwana asipoulinda mji, walindao wakesha bure. Na Bwana asipoijenga nyumba, wajengao wafanya kazi bure"

Kuna wachungaji na wahubiri wengi leo wanatembea na mabodigadi, hata wakiwa wanahubiri mabodigadi wanawazunguka.
Biblia inasema kwenye kitabu cha Yeremia 17:5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.

HAYO SIO MANENO YANGU, NI YA MUNGU MWENYEWE
 
Magaidi wameshakuwa wengi sana na watumishi wa MUNGU wamekuwa walengwa kwaenye mashambulizi yao mfano huko Zanzibar na kwingineko hivyo lazima kuchukua tahadhali na niwajibu wao kuchukua tahadhali.
 
Sasa hapa kuna angalizo. Kwa kuwa Bwana asipoijenga nyumba wajengao wafanya kazi bure", haina maana kwamba tusijenge nyumba na tumwachie Bwana ajenge.

Bwana sipoulinda mji walindao wakesha bure, haina maana tusichukue tahadhari. Kumbuka kuna andiko limesema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Maarifa!.

Fimbo ya musa haikukausha bahari, lakini ni nyenzo Mungu alimwambia Musa aitumie ili Mungu akaushe maji yale.

"Inuka uangaze", au '"Raise and shine", kuinuka ni jukumu letu, na tunapoinuka, Mungu anatufanya tuangaze.

Aisee......!!! Hivi pale inakua anajaribu kuonesha kua nae ni muheshimiwa sio? Sasa kwani mtu wa Mungu anahitaji ulinzi wa mwanadamu?

'....Bwana asipoulinda mji, yeye aulindae akesha bure...' Mwisho wa kunukuu.

'....Watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa..........' wisho wa kunukuu.

'....za kuambiwa changanya na za kwako......' Mwisho wa kunukuu.
 
Magaidi wameshakuwa wengi sana na watumishi wa MUNGU wamekuwa walengwa kwaenye mashambulizi yao mfano huko Zanzibar na kwingineko hivyo lazima kuchukua tahadhali na niwajibu wao kuchukua tahadhali.

Wafilipi 1:21 unasema
Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.

Ufunuo wa Yohana 14:13 unasema
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Sasa kwanini mtumishi uogope magaidi/ kifo?
Tena Biblia imesema mara 365 usiogope, hii ni sawa kila siku ya mwaka unaambiwa usiogope.
 
😱Lakini mimi.ngoja.nitafsiri tofaut kidogo na wenzangu.. Huo mstari mwshon unatoa sharti la kukwacha Bwana..... Yani una bodigadi halafu unaacha kabisa kumtegemea Mungu... Hapo Biblia yanena UMELAANIWA... lakini kama unamtumia mwanadamu katika kukulinda bila kuacha kutegemea ulinzi wa Bwana.. BasI HUJALAANIWA

hii ni sawa tu na kusafiri na basi linaloendeshwa na mwanadamu bila kumwomba Mungu awaongoze safarini. .. Umelaaniwa

lakini kama unategemea bus likufikishe kule uendako na unamwomba Mungu aiongoze safari yako Na amwongoze dereva kuwafikisha salama basi HAMJALAANIWA

lakin shida ya walimwengu wamemsahau kabisa Mungu

#kutafisiri Biblia kazi ngumu😱
 
Hivi unasimama madhabahuni na kuanza kudhihaki wengine...ni lazima utaweka bodyguards ili kujinisuru.
Dhihaka haitoki kwa Mungu. Kama mhubiri anafanya mambo yasiyompendeza Mungu lazima ajilinde kwa nguvu zake mwenyewe ie kutumia hela kwa ajili ya ulinzi (mishahara ya mabodigadi)
 
Watumishi hawaogopi kifo wala magaidi maana kifo kipo tu kwa njia yoyote lakini Mungu alitupa akili ili tusiwe Easy-target au Soft-target ndiyo maana tunaweka magufuli kwenye milango yetu,hata ukiona nyoka unachukua tahadhali ya kukimbia au kama una uwezo unamuua,

hatuwezi kujiachia achia tu lazima tahadhali ichukuliwe hasa kwenye ulimwengu wa sasa ambao kuna dini na watu wengine wanadai kuwa ni wa AMANI wakati siyo kabisa,watu wanaingia kanisani kwa lengo la kuchafua AMANI, na wengine wanaingia Misikitini hawana lengo jema wao wana uchu wa kumwaga damu isiyo na hatia.
Wafilipi 1:21 unasema
Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.

Ufunuo wa Yohana 14:13 unasema
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Sasa kwanini mtumishi uogope magaidi/ kifo?
Tena Biblia imesema mara 365 usiogope, hii ni sawa kila siku ya mwaka unaambiwa usiogope.
 
Mh haya yote ni mahangaiko ya wanadamu wanalinda nafsi zao huku wakilitangaza jina la Mungu kuwa ni ngome yao huku hawasadiki wakiweka walinzi kuwalinda
 
Back
Top Bottom