Ujumbe mahsusi kwa Wachungaji wenye Mabodigadi

Ujumbe mahsusi kwa Wachungaji wenye Mabodigadi

Wafilipi 1:21 unasema
Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.

Ufunuo wa Yohana 14:13 unasema
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Sasa kwanini mtumishi uogope magaidi/ kifo?
Tena Biblia imesema mara 365 usiogope, hii ni sawa kila siku ya mwaka unaambiwa usiogope.

Hapo umesema ukweli mtupu hawa jamaa Hamna lolote ni USANII MTUPU wanafanya hebu cheki kama huyu anajiwekea ulinzi kama rais wa nchi ni kitu gani hasa anachokiogopa kama si tapeli huyu
 
Kuna nabii hapio....mitapeli tu hiyo...yanapuga hela za waumini wao na kutembea na vogue wakati waumini wanasaga lami kwa lapa....teh!... teh... mm hamnipati ng'o
 
Mkuu umeona mbali....mtumishi wa Mungu..unaenda kadiri ya utumishi wa Mungu,Hauna makandokando, sio mfanya biashara, unaishi kadir ya neno....Walinzi wa nn??kuna.shida.hapa...kuna mambo ya chin chin hatujui kuhusu hawa watu.....mapadre,maaskofu,baadhi ya wahubir wa kubwa na watumishi wengine mbona hawana mabodyguard....hao wenye walinz kama president Magufuli wanalao jambo
 
Hao wahubiri wanajaribu kuwaaminisha watu wasichokiamini wao, utapeli wa wazi kabisa.
 
Wanaitwa Manabii pesa! Hakuna Mungu,wote ndoto zao ni Sadaka, na Mijengo!. Wapo kimwili zaidi!.
 
Kama mtume marehemu analindwa na kupiganiwa kwa nini hawa walio hai wasilindwe na kupewa kinga?
 
Hao jamaa ni wapiga dili tu na very soon watakuwa outdated mana kizazi cha dini kinaanza kusepa
 
Kuna wachungaji na wahubiri wengi leo wanatembea na mabodigadi, hata wakiwa wanahubiri mabodigadi wanawazunguka.

Biblia inasema kwenye kitabu cha Yeremia 17:5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.

Thibitisha kwanza kama hao unaowasema mioyoni mwao wamemwacha Bwana.

Halafu usome Hosea 4:6 " Watu wangu wanaangamiwa kwa kukosa maarifa". Na ufafanue unalielewaje hili andiko.

Kwa nini mnakuwa watu wepesi wa kuhukumu bila kuyaangalia maandiko?
 
Up to now na Mimi sielewi ila wa Tanzania hupenda kuiga niliwahi kuona napoabudu Mimi walinzi wako kwenye mvua huku wamevaa suti .mvua iliwaishia mwilini hadi Leo sijapata jibu kwanini wachungaji wanajuwa nama bodyguard
 
Up to now na Mimi sielewi ila wa Tanzania hupenda kuiga niliwahi kuona napoabudu Mimi walinzi wako kwenye mvua huku wamevaa suti .mvua iliwaishia mwilini hadi Leo sijapata jibu kwanini wachungaji wanajuwa nama bodyguard
Gwajima huyo.
 
Baraaa wewe fuata neno usifuate vitendo utapotea pia imani nikitu hatari Sana wengi tumekuwa brain washed na madhehebu ya sasa ila tumtumai Mungu tu basi hatuna jinsi
 
ukweli ni kwamba mtindo wa maisha ndiyo unaowafanya wawe na mabodigadi.
 
Huu ulinzi utatufanya sisi waumini tuwaone ni binadamu wa kawaida wanaoishi bila Mungu na wamejawa na hofu nyingi kutokana na matendo yao.
 
Wanajifahamu wantumikia mungu yupi, ndio maana ni lazima wajilinde.
 
Wewe inaonekana kwanza huna adabu kwa watumishi wa Mungu, umetoa mandiko kutoka kwa yeremia,sikiliza km hujui uliza,kwanza inafaa kila MTUMISHI awe na bodyguard, soma maandiko vzr, mfalme Daudi alikuwa na mashuka wenye silaha wangapi?walio mlinda?sulemani? Daniel? Hata yesu mwenyewe alikuwaga nao, ndio maana ilifika mahari akawambia wabebe panga. Ngoja nikuache kwanza ukinijibu nitakupa misitali. Usie na adabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom