Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,142
Je Sheria ya nchi inasemaje ? soma hapo chini 👇
ASalam Alaykum,
Hongera nyingi sana kwa ndugu yetu wa imani ya kiislamu kwa jihad kubwa aliejitolea wa ujasiri mkubwa kuongea hayo bila oga na hatimaye natija yake ameamsha usingizi hisiya ya siyo ya viongozi na Mashekh wetu tuu bali hata viongozi wetu wa serikali kuwa kutukumbusha na nyaraka ilyotolewa mwaka 1999. na wizard ya elimu...hatuwezi kujua kiasi ya malipo yake kubwa atapewa na Mwenyeezi Mungu Subhana Wataala. Pia kuwa zindua viongozi wa dini na Mashekh wetu kuweza kutambua makosa yetu kotika kujua haki zetu nyingi tulizo nazo katika Serikali yetu ya Mungano wa Tanzania.
Alhamdulillah.. sasa wanafunzi wa kiislamu wengi watapewa haki yao ya kutimiza ibada sala ya ijuma na sasa itakuwa ni thawabu ja'ariyah kwa huyo bwana.. hata siyo kiongozi wala Sheikh. Bali alikerwa na kuchukua uamuzi binti zake wasiende shule ili waende kutimiza ibada ya salaa ya ijumaa.. kweli Mwenyeezi Mungu Subhana Wataala amempa malipo makubwa ya jitihada zake kupigania haki za wanafunzi wote wapate ruhusa ya kutimiza ibada ya salaa za ijumaa...Ameen
Kweli Alhamdulillah ametupa darasa kubwa sana...tusiogope kusema ukweli kunusuru Dini la
Mwenyeezi Mungu Subhana Wataala na yeye ndie atawalipa .. Ameen