Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,330
- 24,213
Katika taarifa ya habari saa saba mchana huu, msoma taarifa ya habari (dada) alisema Tanzania ina nia ya kuendeleza uhusiano kati ya Tanzania na India ulioanzishwa na Baba wa Taifa na waziri Mkuu wa India Mahatma Gandhi! Hili lilirudiwa mara mbili.
Kwa kushangaa nikijua kuwa Mahatma Gandhi alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Taifa la India (akishirikiana na kina Jawaharlal Nehru), Mahatma alifariki kitambo, 1948, na hakuwahi kuonana na Mwalimu.
Nikachoka, nikajua ITV/Radio One wameajiri mazuzu!
Joyce Mhavile, ajirini basi vijana waliopasi na wana uelewa wa kihistoria na mambo ya dunia.