WADAU. Nimekuwamsikilizaji wa kipindi cha asubuhi cha Clouds FM cha Power Breakfast, ambachoni maarufu sana siku hizi, siku za karibuni GERALD HANDO kupitia segment yakeya Jicho la Ngombe amedhihirisha dhamira yake hasi kwa taifa letu, dhamirailiyojaa unafiki mkubwa.
HakikaGerald amejivika kuwa mtetezi wa maovu ya serikali, hususan bajeti hii ambayohata serikali yenyewe imekiri kuwa ni mbovu ikifanya mkakati wa kuiboresha.Ndugu zangu wenye nia thabiti ya kuleta mabadiliko katika mfumo mbovu wa serikalihii, nawaomba tuungane kwa nguvu zetu zote kukataa propaganda chafu za GeraldHando (siamini kama ni msimamo wa Clouds Fm kama ndivyo wawathibitishiewananchi).
Leo asubuhiamewakejeli wabunge wetu wote wanaoikosoa bajeti hii, akidai wanatafutaattention kwa wananchi, tena akienda mbali kwa kudai ni watovu wa nidhamu kwababa yao (Rais), tena hawafanyi kilichowapeleka bungeni. Hivi yeye ni nanimpaka atoe kashfa zote hizo? Au kwa kuwa amepewa jukwaa la kubwabwaja. Hakikanimemshusha thamani kwa hoja zake dhaifu!
Wadau,naandika kwa urefu nikiwa very disappointed na hawa wana habari uchwara (kamaGerald Hando) ambao wanaweka maslahi yao badala ya umma. Sielewi kwa mtazamo waGerald Hando wabunge kazi yako bungeni ni ipi kama sio kuihoji na kuibanaserikali, yawezekana hawafahamu hata majukumu ya mbunge (inataka elimu ilikujua hilo sijui kama anayo), anataka waende kusinzia kama baadhiwalivyochukuliwa na picha?.
Iwapoameamua kuwa msemaji wa serikali ya CCM, basi tujulishwe kwani hatuna tatizo naRadio Uhuru amabyo ni propaganda machine ya CCM, kila mtu anajua hilo na hatuna tatizao nalo, ilawapigania ukombozi wa kweli tutaendelea kuibana serikali, tukiwatumia wabungewetu kama Mnyika kueleza umma uozo wa serikali hii, asitukatishe tama kwanihatofanikiwa kamwe. Hongera Mnyika tuko nyuma yako katika hili.
Aluta Kontinua mpakaserikali itambue haki ya wananchi. Ole wao wanafiki siku zao zinahesabika
Mkuu mimi naungana na wewe 100%, kuna watu waliopata nafasi ya kuwa kwenye vyombo vya habari na kuamua kutumia muda mwingi kufikiri mawazo yao tene yaliyojaa ubinafsi na ufisadi ndiyo mawazo yaliyo sahihi kuliko ya wenzao.
Kuna watangazaji wa radio hii ya clouds FM specificaly Kibonde, huyo geradl hando na wengine wanafikiri Taifa hili ni la CCM na wao. Hawa jamaa hata shule yenyewe ni ya kuunga unga sasa sijui wanakuwa wanaongea reference yao iko wapo.
Leo hii Madaktari wanataka kugoma eti kwa sababu serikali haitaki kurekebisha maslahi yao, waalimu wanataka kugoma kwa sababu serikali haitaki kurekebisha maslahi yao na kuwalipa malimbikizo yao halafu wanakuja wenda wazimu fulani eti bajeti ni Nzuri tena waonekane wanaoirekebisha kwa kupinga ni wendawazimu zaidi.
Leo hii ananakuja mtangazaji ambaye kimsingi anajua tu kusema maneno ya kiswahili anaanza kupingana na watalamu wa Uchumi, Sheria na mambo ya Mipamgo.
Hawa jamaa ni wapinza wa uhuru halali wa Watanzani na wapinzani wa wale wanaopinga matendo ya kifisadi... Mimi nashangaa sana wamekaa Maprofes UDSM, wanalalamika bajeti hii haina tija kwa watanzania kwani imeshindwa kutatua matatizo ya msingi ya watanzania, eti wanakuja hawa waliofeli na kuanza kufanya propaganda.
Kwa mimi mtu wa kawaida ninavyofahamu, mtangazaji anatakiwa kuwa neutral na kusikiliza wachangiaji wengi wanasema nini, sasa kwa hawa wao tu ndiyo wanaongea na kupiga kelele tangi asubuhi hadi jioni wakilazimisha eti mawazo yao ndiyo yako sahihi kumbe ni Pumba tu.
Haiwezeka watanzania wengi wakiwemo wataalamu wa Uchumi wanasema bajeti Mbaya kwa kutoa sababu na maelezo halafu wanakuja tu watu wawili from noware eti hakuna bajeti nzuri kama hii na kuwaponda wanaopinga kwa kutoa mawazo mbadala.
Kama alivyosema mchunga Peter mwesiga, Hawa ndiyo waliosababisha matatizo yaliyoko kwa makusudi kwa hiyo hawawezi kuwa solutions, watabaku kuwa matatizo tu.
Just imagine tokea lini mtu aliyepotea njia akawaelekeza wengine.
Problems cannot be solved by the same level of thinking that have created them, we need an alternative solution