MTAZAMO
Platinum Member
- Feb 8, 2011
- 19,990
- 34,838
Clouds tumeilalamikia mno lakini hawana hata nia ya kubadilika.Moja ya sababu ya wao kutotaka kubadilika ni namna wanavyonufaika na hali ilivyo na jinsi wanavyotumika kwa malengo ya watu fulani.Tahadhari ni kuwa wamewezeshwa kukua kwa kasi na kwa porojo zao wanao wasikilizaji wengi pia sababu Watanzania tunapenda porojo pia!
Upo umuhimu wa labda kwenda hatua mbele zaidi kuwapa funzo wale watangazaji wanaowapotosha kwa makusudi wananchi wa kawaida.Clouds hawawezi kubadilika fahamuni hivyo hata tupigeje kelele maana nao wanajua upepo unavyokwenda na wanauma na kupuliza.
Nasikitika Chadema hawajawahi kujibu rasmi tuhuma za kipuuzi za watangazaji wa Clouds ambazo si za kupuuza kwa namna zinavyowafikia wananchi.nafikiri Chadema wanaogopa mgogoro na vyombo vya habari lakini kwa hawa Clouds hata wanahabari wengine wamechoshwa nao na unafiki wao uliopitiliza.
TUMEAMUA KUWAPUUZA TUENDELEE HIVYO LAKINI HAWATAACHA KUENEZA CHUKI DHIDI YA UPINZANI.