Ujumbe kutoka kwa Prince aliyepita

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
JAMHURI: Wewe na Waziri Membe mna uhusiano gani?

RIDHIWANI: Membe mimi ni rafiki yangu, lakini pia Membe ni baba yangu, mentor (mlezi) wangu. Namwangalia kama mtu unayeweza ukamwiga kwa mawazo yake na utendaji wake. Nimemfahamu mara ya kwanza mwaka 1986. Tulikuwa tumetoka Arusha tumekuja Dar es Salaam na baba. Tukaenda nyumbani kwake Membe, tukaenda wote. Wakawa wanazungumza. Ni marafiki wa siku nyingi. Tukiwa Nachingwea alikuwa anafika kumsabahi baba. Kulikuwapo na ndege inatua pale Nachingwea kila akitoka airport anapitia kwetu.

Mambo makuu matatu yakiendekezwa taifa huingia matatani, udini, ukabila na upendeleo. Nimekuwa nikiichungulia serikali na kuonamo fitina ya ukanda na ukabila. Ni kana kwamba kanda ya kaskazi imetoswa nje japo kwa kulambishwa unaibu elimu. Nimechungulia huko jeshini, mikoani na wizarani ni kama kumejaa ukanda hivi.

Niliitafakari sana Kariakoo ya awamu ya tatu kwanini maduka mengi yaliyajaa watu wa kanda ya kaskazini. Ningali katika kuwaza hilo mmoja ambaye sikumfahamu vizuri alinizushia kwamba mwangalie first lady ujue ametoka wapi na ndipo uendelee kutafakari upate majibu. Jamani hivi first lady wa awamu ya tatu alitokea wapi?

Wakati mwingine tunawalaum sana wakurugenzi wa idara na waajiri kwa namna wanavyoonesha upendeleo. Lakini ukiitazama vizuri serikali kuu ni kama baba wa upendeleo halisi!

Kunako miaka ya 2005-2008 palikuwako kampuni moja ya mradi wa mbao mkoani Mwanza. Kampuni hiyo iliyomilikiwa na mhaya mmoja ambaye kwa baadaye machine yake ilimkata mkono, ilijaa wakurya tele!! Basi watu walijiuliza kwanini wakurya tu? Mbona mmiliki wake ni mhaya? Kumbe mkewe alikuwa mkurya!!

Ilifikia hatua watu wakaanza kunong'ona chini kwa chini kwanini kila taasisi kuna wahaya? Wengine walijibu eti walisoma mapema!! Jibu la namna hiyo liliwahi kutolewa na serikali ya Zanzibar. Ulifika wakati nafasi za kazi hususan kwenye Hotel management n.k, zilishikiliwa na eidha watu wa bara ama watu wa kutoka nchin Kenya. Wazanzibar walipozidisha minong'ono walijibiwa wasome wasikalie kujidanganya na madrasa zao kwa kuziita vyuo. Wazanzibar walitamani ajira ambazo hawakuwa na taaruma yake maana taaruma yao ilikuwa kusoma na kukariri aya za Koran kwenye mashindano ya kuisoma.

Hali haikuwa vile kwa mzee Kikwete. Urafiki ulifanya upendeleo wa kumteua rafiki yake wa siku nyingi Bernad Membe kuwa waziri wa mambo ya kigeni. Wengi husema Membe ni ndugu wa Kikwete mara mpwa wake! Sivyo! Ni urafiki! Wasemao ni nduguye bilashaka wanahadaika kwa kigezo cha mfanano wa rangi.

Wengi wamekuwa na maswali ya kwanini Membe anajimwambafy. Wengine hujijibu ni kwasababu Kikwete ni mjomba wake hivyo serikali haiwezi kumninihii. Kuzingirwa na sifa ama uwepo wa baba kuna aina fulani ya nguvu kama wengi wasemavyo kumhusu Fatma Karume. Si wengi tu bali hata Bashte Makonda aliwahi kumwambia mbashala!! Kumbe upinzani wa kweli utatoka kiunoni mwa wastaafu!

Tumtarajie Liziwani kuwa ACT Wazalendo, Abdallah Mwinyi(mtoto wa Hassan Mwinyi) kuwa CHADEMA, Makongoro Nyerere kuwa NCCR Mageuzi, Brasilia Wiliam Mkapa awe NLD, Salama Ali Hasan Mwinyi awe TLP, Jerry na Jesca John Magufuli wawe CUF!

Je watapigwa mabomu? Je watatekwa? Je watafunguliwa mashtaka ya hapa na pale? Je watazuiwa kufanya mikutano ya siasa? Je wataenguliwa kiserikali za mitaa?

Uwepo serikalini wa Makonda, Mabbeyo, Gambo, Kitwanga, Kalemani, Mabula, Mwijage n.k ni kama aina fulani ya siasa za ukanda as opposing to ukanda wa kaskazini.

Miaka michache iliyopita ililipotiwa uwepo wa upendeleo wa nafasi za juu BoT ambapo watoto wa vigogo walijirundika humo. Pia kwenye sekta ya afya jijini Dar es salaam palijaa watoto wa vigogo akiwemo binti wa Kawawa na kijana Lowassa pamoja na Sumaye n.k. Palikuwepo na watu wengi wenye sifa kama hizo lakini eidha walikoswa ajira ama kutupwa vijijini.

Upendeleo huu tuliuona pia kwa binti Magufuli "Jesca" kwenye zamani za vilaza ambapo alifeli mtihani wa kidato cha nne kwa kupata daraja la nne 30 katika sekondary ya Mtakatifu Mathew. Wakati vilaza wakitimuliwa vyuoni, Jesca alikuwepo UDOM akidundadunda!! Lakini pia kilichowaumiza wananchi ni hivi: Jesca alipataje kujiunga na kisomo cha elimu ya chuo kikuu kusomea shahada ya biashara akiwa hana sifa? Yaani mtu alipata "F" ya commerce form four iweje asome bachala yake? Kumbuka alimaliza form four 2011.

Aliwezaje kusoma kidato cha sita tena kwa miaka miwili akajiunga na chuo 2014? Aliwezaje kujiunga na kisomo cha kidato cha sita na wingi huo wa miswaki kwenye cheti chake? Je alisoma certiticate kwa mwaka mmoja kisha ikampa kusoma diploma kwa mwaka mmoja? N' nchi ya mabwege? Nafuatilia kujua hatima yake! Ukiwa na kilaza nyumbani kumbe ni aibu! Ni nongwa!! Huyu hapa:- http://196.44.162.33/necta2011/CSEE 2011/s1071.htm

Wenye akili zao na division 4 ya 27 wanabaki nyumbani. Wenye serikali yao mfukoni wana-join universities na kupata mi-scholarship kibao!!

Wakipanda kwenye majukwaa ya siasa wanatangaza amani, umoja na mshikamano! Kama walifaulu ukilaza kuuingiza vyuoni watashindwa nini kuliingiza liccm serikalini?

Niwakumbushe kauli moja ya rais mstaafu wa hapa East Africa. Alisema, "chama tawala kitashindwaje? Kikishindwa ni uzembe kwa maana jeshi ni lake na mabunduki ni yake". Unamkumbuka huyo n'nani alisema na akimwambia nani?

Marehemu Nyerere anasema, "ukila nyama ya mtu utataka uile tena". Mimi mtakatifu wa Bwana ninasema siasa zikianza na upendeleo kifamilia, kirafiki, kikanda, kielimu, kimatibabu, kiajira hatimaye zitajipendelea zenyewe kuishi madarakani kwa namna yoyote iwayo iwe kwa amani ama kwa shari, damu itamwagika mpaka wamekweya serikalini.
 
Kumbe ndio maana watu wanaamini kwamba Membe na Kikwete ni ndugu hawajakutana leo awa washikaji!

Akili ya mwanasiasa uja pale tu anapokuwa nje ya mfumo wa wizi na upigaji kuna siku ata Makonda atakuwa anaongea lugha izi.

Kama ni kweli Riz kaongea haya namkaribisha kwenye ulimwengu mpya wa kuongea ukweli na kutetea watanzania.
 
Ridhiwani hawezi nena hayaa
1575307027569.jpeg

Huyu ndiye msemaji.
 
Kama huyo ndio RIDHIWANI na hayo ndiyo majibu yake basi yeye na wafuasi wake ni booonge la Mapopoma


Maneno meeengi dhamira ni kutaka WACHAGGA ndani ya serikali kuu.

Mh.MBOWE anawaongoza watu na degree zao yeye ana phd ngapi?
 
Back
Top Bottom