MSITUTUKANE, MSITUDHARAU, MSITUBEZE!
Wapo watu wanatuita waoga! Wanasema tunazungumza sana mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuliko kuchukua hatua za kivitendo.
Jibu langu binafsi kwao ni kuwa; kujitoa kwetu peke yake na kuwaeleza watawala madhambi yao, vinywa na mikono yao kujaa damu za raia, uhuni wao, udhalimu wao, ubabe wao, udikteta wao, uzandiki wao, chuki zao, tamaa zao za madaraka ya damu.... ni jambo kubwa mno.
Barani Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara, mtawala huwa anajiona ni Mungu Mtu. Mtu anayemkosoa mtawala waziwazi huwa amekwishatia saini hati ya kifo chake. Tundulissu hajawahi kuchukua ACTION yoyote zaidi ya kuzungumza ukweli, mitandaoni, bungeni na kwenye vyombo vya habari, wamejaribu kumuua kwa silaha za kivita.
Hata sisi tunaowasema watawala bila woga, tukiwaonya, tukiwanasihi, tukiwakosoa na kuwaeleza madhambi yao, tunafuatwa kila tuendako na roho zetu zinatafutwa usiku na mchana. Pamoja na mazonge yote tuliyonayo, hatuja-give up, tuko imara sana, walio-give up mmewasikia wako CCM, wanalinda roho zao, maisha yao na familia zao.
Sisi wengine tumekataa kusaliti ukweli halisi, kwamba Rais wetu John Pombe Magufuli analipeleka taifa letu shimoni, na lazima abadilike, atubu, arejeshe utengamano wa taifa, umoja na mshikamano, ailinde katiba kwa vitendo, asishikilie uhuru wa bunge, asiikalie mahakama, asivifunge mdomo vyombo vya habari, asichukue uhuru wa maoni wa raia, asijaribu kuviua vyama vya upinzani na taasisi za harakati hapa nchini.
Haya tunayomweleza Magufuli, watangulizi wake (Mwinyi, Mkapa, Kikwete) hawawezi kumweleza, wazee wanaoheshimika kwenye taifa hili hawawezi kumweleza (kina Warioba, Butiku na wengine), Maprofesa na wasomi wakubwa hawawezi kusimama hadharani wakamweleza.
Walau kwa sasa, kwa sababu tunaweza kumweleza bila kujali maisha na uhai wetu, tuacheni tumweleze. Ni Nyerere tu ndiye angekuwa hai na leo angelisimama hadharani na kumkanya Magufuli. Ni Mzee Kingunge peke yake ndiye amesimama hadharani na kumkanya, wengine wote wanatetea pensheni zao, mishahara yao, matumbo yao na raha za familia zao.
Sisi mnaotubeza pia tuna familia, tunapenda pensheni, tunataka mishahara, tunataka raha - lakini tumeamua kuvipata vitu hivyo kwa njia halali binafsi nje ya mifungamano na kuitumikia dola dhalimu. Kwa hiyo walau mtutie moyo, walau mseme "wapo viongozi imara, msitubeze".
Kama tumeweza kulinda utu na heshima ya taifa letu mpaka sasa, tumetishiwa, tumefuatwa, tumezongwa, tumefilisiwa na kila ukatili tumefanyiwa, na bado tuna misimamo - kumbe basi, kama ikibidi "hatutakua na hofu tena na mambo mengine ya kupita, tutasimamia ukweli mpaka mwisho wa maisha yetu, kumbe basi tutakuwa tayari kufa vifo walivyovipanga watawala juu yetu, kumbe basi tutakuwa tayari kufia magerezani - lakini tutakufa huku tukiongoza mapambano ya kudai haki na uhuru kwenye nchi yetu."
If need be that we die fighting for justice and freedom in our country, many of us will be ready to die, no body should underestimate us, as the cause we are fighting for is innerly sponsored, it is a cause of protecting the dignity and well being of our people.
If need be that we will not be available should the JUSTICE and FREEDOM will showup, then we are ready for that to happen, we are ready that our blood irrigates the victory to our next generetion.
And whoever think that, fighting for justice, democracy and freedom in this country will be stopped by bullets, and bombs, and killings, and kidnapping and propaganda, that person is very wrong.
As long as we are not ready to betray our people; justice and democracy and freedom shall prevail. We understand that horrible things shall happen to us, we know that the worst are yet to come; smilingly and comfortably, we shall receive whatever bitterness and hurtings and destructions and consequences.
It is the law of the nature that, the payment of fighting for justice is always painful, and whoever is not ready to receive the pain won't sustain the struggle.
[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J