Halafu Hapo Sioni Suala Lolote La Ufisadi Unalidhalilisha Jeshi Letu La Polisi Unavyojaribu Kuliweka Katika Mazingira Haya Bwana
pole sana kwa yote yaliokukuta why usimpigie kamanda wa kandaa maaluumu ukamwelezea jinsi vijana wake wanavyofanya kazi kizembe awaajipishe, namba yake ni Kamanda Seleman Kova 0754094224
Wee shy wewe, wanasema hivi ukiwa muongo ni vizuri uwe na kumbukumbu. Usinone ni junior member, nimeanza kusoma JF Kama guest zaidi ya mwaka. N akumbuka sana story zako za kukamatwa na laptop na polisi ukalazwa ndani na uongo mwingine mwingi, kumbe pale ulikuwa unalisifu jeshi la polisi au ulikuwa unalidhalilisha au ulikuwa unatuletea story zako ili tukuhurumie au ni uongo tu. Sijui nikuewke group gani ila kwa mwanaume kubehave the way you do ni aibu. we ni mnafiki sana shy, either uanafanya makusudi kuwaudhi watu au uko kwenye payroll ya watu. I should know better tangu scandal ya JF hadi watu fulani wakashikwa. Behave like a man atleast for once. Siyo muhimu kuchangia kama huna ch kusema, no wonder your status says you are alone in the dark! From what i see thats very true.
Yani nimesumbuliwa wiki mbili ili nilipie tu sh 500 QUOTE]
Mkubwa unakua kama ndo umekuja leo Bongo.....!! ungewapa hao manjagu buku jero tu walaa hata usingezuka hivo!!!
penye udhia......mkubwa penyeza..... Ndio Bongo yetu hiyo tufanyeje!!! tehe tehe
mkuu Watu Kama Akina Shy Wasikupotezee Mda..hapa Tumeshawazoea..wapo Tuu Kwa Sababu Mungu Aliwaumba Wawepo! The Guy Is Just A Joke Whenever You Read His/her Arguments! He Thinks Kutetea Maovu Ya Serikali Ndo Uzalendo...anyway Ukiona Post Kama Hizo Ignore. Maana Watu Kama Haop Wanataka Attention. Infact Hapa Jf Watu Walishamgundua, Ndo Maana Post Zake Watu Wanaziignore Kwa Sababu Hazina Substance.....jaribu Kuchek Na Kova Kwenye Simu Yake Ya Kiganjani...
ila Aise Pole Sana, Na By The Way Jaribu Uende Benki Uombe Atleast Temporary Blockage Ya Account Yako..maana Wezi Wanaweza Kuwa Wanapita Pita Hata Hapa Jf..wewe Kawaambie Kwamba Incase Of Anything..you Will Proceed Against Them. Utaprove Ownership Ya Account Kama Ukipata Hiyo Barua. Lakini Pesa Yako Ikiibiwa Kwauzembe Wao..then Hawana Pa Kukimbilia.
Huu ni ugonjwa wa polisi wa mlimani tangu zamani. Mimi miaka ya nyuma niliwahi kupoteza ATM yangu nikaenda wakaniambia hivyo hivyo. Fikiria gharama ya kutoka Mlimani hadi Oysterbay na muda kwa ajili ya kulipa sh. 500. Sasa hao polisi hapo kazi yao ni nini? Wangeenda hukohuko Oysterbay ijulikane hakuna kituo hapo. Wht happened ni kwamba nilitoa 1000 nikawama mara wakachomoa form wakaniandikia kila kitu na mhuri juu. It was painful but that is what I had to do otherwise I would incur unbearable cost. Na hili libenki hapo lina protokal ya ajabu. Maafisa wanaboa as if sio professionals. Wana kawaida ya kutoweka hela kwenye ATM siku za weekend na sikukuu. Huwa wanaweka Jm mosi wakiwepo, ila wakishaondoka hakuna kitu.
Thank you for the number, nimepiga sasa hivi na landline imeita halafu ghafla answermachine inasema simu haiwezi kupokelewa nitafute namba nyingine kama inawekana. Mnaona sasa ilivyo ngumu, huyu kova au rwambow ofisi zao ziko wapi? niko tayari kuwafata na kuwakilisha malalamiko yangu.
Kijana Wewe Ni Fisadi Namba Moja Kwa Sababu Unasema Vitu Bila Kuwa Na Vidhibitisho Vyovyote Vile Hata Hiyo Mada Yako Nina Wasi Wasi Nayo Sana Ndio Maana Nikakuuliza Yote Hayo Juu Nakuone Huruma Sana Kwa Kusukumwa Na Hulka Kwamba Mfanyakazo Wowote Wa Serikali Ni Fisadi Hata Hao Wanaolinda Mali Na Usalama Wako Una Wadhalilisha
Mfano Katika Maelezo Yako Ungetaja Bank Gani Pale Kituo Cha Polisi Uliwasiliana Na Nani Manake Wale Wanamajina Na Namba Zao Kwanini Hukuzinote Hizo ? Sasa Unatufanya Sisi Wote Ni Wahuni Humu ?
Mimi Sina Mengi Nafikiri Umenielewa Wewe Endelea Kuongopa Tu Mbele Ya Ummha Utaona Faida Zake
Sisi watanzania tumezoea vitu viwili:
1) kununua haki yetu. Kiasi cha kwamba hatuoni taabu kukata kitu kidogo ili tuipate.
2) Kuogopa authority. Tunakubali kuendeshwa na madesk officers, receptionists hata mesenja! Kwa nini huyu bwana baada ya kuona upuuzi hu hakudai kuwaona wakubwa zaidi? Huko polisi angepanda ngazi hadi kwa Mwema. Hapo ndipo jamaa watakapo shika adabu. Hauwezi kuzungushwa vituo vyote hivyo kwa ajili ya risiti!
Nashauri lolote litakalotokea aandike barua ya kulalamika kwa Kova, nakala Mwema na Katibu Mkuu, Mambo ya Ndani. Akiona wanapuuzia aitie kwenye magazeti na mlolongo mzima wa ishu. Aandike nyingine kwa meneja wa benki yake, nakala kwa CEO, akitoa sababu za KUFUNGA akaunti yake.
Upuuzi huu ni kama ule wa PF3. Inabidi wabadilike na kuwajali wateja.