Ujio wa Yesu na Dini

Ujio wa Yesu na Dini

Mleta post mmoja juu alikupa mfano wa watu kushinda makanisani sasa waweza kujiuliza muda wa kufanya kazi wanatoa wapi? Wapo wengi ambao maisha yakiwapiga hukimbilia kanisani kuombewa wakiamini ndo msaadawa maendeleo uliobaki badala ya kutafuta vyanzo vingine vya mapato
Mbona hoja nyepesi mkuu,mbona pia kuna watu wapo vijiweni tu hawafanyi kazi yawezakuwa kwa kutotaka kufanya kazi ama kukataa kazi zenye malipo kidogo kisa yeye msomi..je nao pia utasema dini ndiyo imesababisha hivyo? ama ni watu wenyewe tu?

Halafu tuache kukariri usione mtu anashinda tu sehemu ukadhani hana kitu cha kumuingizia kipato.
 
Dini ni kama taasisi iliyotengenezwa kuwa subject watu haswa waafrica kukubali utawala wa wazungu na kuwafanya kuwa tegemezi maisha yao yote..Tafsiri yangu..
Wazungu hawa hawa ambao wanataka tukubali ndoa za jinsia moja? kama ndio hawa hebu eleza ni vp wazungu wanatumia hizi dini ili tukubali utawala wao.
 
Mbona hoja nyepesi mkuu,mbona pia kuna watu wapo vijiweni tu hawafanyi kazi yawezakuwa kwa kutotaka kufanya kazi ama kukataa kazi zenye malipo kidogo kisa yeye msomi..je nao pia utasema dini ndiyo imesababisha hivyo? ama ni watu wenyewe tu?

Halafu tuache kukariri usione mtu anashinda tu sehemu ukadhani hana kitu cha kumuingizia kipato.

Usiame sana Mkuu, dhana ni imani ya dini. wapo wasioamini katika dini na wapo wanaoamini. Kwa sensa ya harakaharaka maskini wengi wanaamini katika dini na kuona ndo njia ya kumfikia Mungu kupata mahitaji yao tofauti na ilivyo kwa matajiri wengi..
 
Uliwahi kufa mkuu hayo mambo wewe umeyajuaje?

scientific proof.. achanana mambo ya dhahania kutokana navitabu vya mzungu. Mfano ni kwamba ukifa na tukaja kukuangalia baada ya miaka minne ni udongo tu sasa utafufuka huku ushafutika katika sura ya dunia!!
 
Maneno ya Marehemu Remmy Ongala katika wimbo wa Kilio ukiyasikiliza kwa makini yanaleta hoja nzuri nzuri juu ya mapokeo ya dini, ujio wa Yesu na namna wakoloni walivyotuchota na kutulisha matango pori yao hadi leo tunayatumia.

Vitabu vingi vya dini vimeanza kuandikwa na wao, Hatuna mtu, tulikuwa na dini zetu wakatuambukiza za kwao kwamba zetu hazifai, ujio wa Yesu hadi leo hatokeii vitabu vya dini vinaandika anakuja yu karibu kuanzia miaka mingi iliyopita vizazi na vizazi vimepita tunazaliwa, tunakua na kuzeeka, tunakufa lakini haji. Sasa hii ya anakuja yuko karibu ni nini! Au ndo njia wazungu walizotumia kututuliza ili watutawale vizuri.

Kwa njia hizi naamini wazungu ndo wamechangia asilimia 100 kuturudisha nyuma wenyewe wanaendelea na mpaka leo wanatutawala kutumia vitu mbalimbali wanavyotuletea na misaada. Hivi tumerogwa au tumejiroga! Hatuwezi kurudi kwenye dini za babu zetu.

Wazungu tu ndo walibarikiwa kuonana na Mungu na kuwapa maneno ya kutuandikia sisi. Njia nyingine za kututawala bana!Mababu zetu walikuwa wepesi kiasi hiki kununulika na maneno ya matumaini.

Ngoja tuendelee kumsubiri Yesu bana dah!
Song: Remmy-Kilio
Sasa Rafiki Prof. Nanii karogwa na nani?
 
kwanza nikuweke sawa,ancient egypt(kemet) ilikuwa ya watu weusi,mafarao waliojenga mapiramidi ya kwanza(step pyramid by imhotep,great pyramids at giza)...misri ilivamiwa na wagiriki,wakafata warumi na mwisho waarabu ambao wapo hadi sasa(story yake hapa ni ndefu kidogo).

nasema walitokea afrika mashariki confidently...this is what they said.."We came from the beginning of the Nile where God Hapi dwells, at the foothills of The Mountains of the Moon." "We," meaning the Egyptians, as stated, came from the beginning of the Nile.This proof is housed in the London Museum that is holding artifacts of Egypt. In that museum you will find a document called the Papyrus of Hunifer.Kwa kukufahamisha tu "the mountains of the moon" ni mlima kilimanjaro.
Kwa hio ni nini kiliwaondoa wale weusi katika misri?? Ni intermarriage,,waliuliwa (genocide) au walihamishwa? Hadi wagiriki na waarabu wakatakeover,,,mimi kulingana na biblia Mwanzo10:6~20 Utaona Misri akiwa Mtoto wa Hamu alizaa wafilisti ambao ni kabila la waarabu.Hivyo lazima alikuwa na gene za kiarabu.Na zaidi misri ni jina la mtu aliewazaa Wamisri wote kama ilivyo kwa Yakobo kwa wana wa Israel..Na Wamisri walikuwa ni taifa kubwa kama Marekani hapo zamani na elimu yao haimtegemei mgiriki labda uniambie mgiriki alikopi na kupesti kwa mmisri.Na pia kwangu mimi kushi sio waafrika,,kushi ana mtoto alieitwa Nimrodi na ndie alienzisha ufalme katika babeli kwenye nchi ya Shinari(iraq) mpaka Syria na ndie mjenzi wa mji wa Ninawi,,,na mpaka leo kuna sanamu ya Nimrodi ninawi.Kwa hio watu walipoanza kuwa wengi Iraq ndio wakaanza kuhama kwenda maeneo mengine...Na wanubi(weusi)Wameanza maisha yao Sudan..Misri ina fungamana na waarabu..na ni mojawapo ya chimbuko(shrine) la waarabu.
 
Usiame sana Mkuu, dhana ni imani ya dini. wapo wasioamini katika dini na wapo wanaoamini. Kwa sensa ya harakaharaka maskini wengi wanaamini katika dini na kuona ndo njia ya kumfikia Mungu kupata mahitaji yao tofauti na ilivyo kwa matajiri wengi..
Nimekuuliza kuna watu hawafanyi kazi wapo ndani wakimtegemea mungu? au wote wenye kuamini na wasio amini dini wanafanya kazi pamoja?
 
Huwa najiuliza kilitokea nini hadi watu wakapokwa historia yao.
Wakauziwa huu utapeli unaoitwa dini pamoja na Miungu yake kwa gharama kubwa hata ya maisha yao.

Sasa hivi watu wengi hasa wa nchi masikini ndio wamebaki kuabudu huu utapeli.Hata public figures wasioamini kwenye hayo mambo huwa wanaigiza kuamini ili waonekane wapo pamoja na wafia dini mradi wapate wanachokitaka kutoka kwao.
Yesu hakuwa na uungu kwa namna yoyote ile, alikuwa mtu wa kawaida na alishajifia zamani na kuozea kaburini[possibly aliuawa kwa makosa ya uhaini].
Wanaomsubiri sijui wanasubiri atoke wapi.
Kabla ya kifo chake Yesu alisema angerudi kabla ya kufa kwa watu waliokuwa wakimsikiliza.Cha kushangaza leo ni miaka 2017 hajaonekana popote.Kama kuna mtu anayemsubiri Yesu arudi au anayesubiri siku ya kiama ifike, huyo ni wa kumtibu.
Ww ni mtu wa ajabu sana
 
scientific proof.. achanana mambo ya dhahania kutokana navitabu vya mzungu. Mfano ni kwamba ukifa na tukaja kukuangalia baada ya miaka minne ni udongo tu sasa utafufuka huku ushafutika katika sura ya dunia!!
Sasa hapo ushahidi wa kuwa hakuna kinachoendelea ni upi?

Halafu vitu vingine ni vya ajabu,leo hatushangai habari ya ya manii kwa sababu tunajua taratibu zake hadi anapokuja kupatikana kiumbe na hadi kuzaliwa ila unasema haiwezekani binadamu huyo huyo aliyepatikana kwa manii kuwa hawezi kufufuka!!!
 
Islamic state japo wako nje ya uhalisia wa ukweli lakini wameyaendesha mambo yao kwa weledi mkubwa,,Umewahi kufikiri chochote juu ya Ninawi au Dabiq?? Umewahi kuwaza juu ya kauli ya Abu Musab al zarqaw""A torch has been lit here on dabiq which will rise until it burnt all the crusaders"" Hawa jamaa walikuwa na plan na walifikiria maeneo Mojawapo ambayo maisha yalianzia na wakajua wanaweza kuanzisha sera mpya ya maisha na Utawala kwa kupitia yale maeneo sensitive..Na kingine ile Armageddon kambi zao hazitakuwa mbali na maeneo haya maana circle humalizikia ilipoanzia..Africa wangekuwa wakushi wasingeamini mizimu maana Nimrodi mtoto wa kushi alikuwa rafiki wa MUNGU.
 
Mzungu ana akili sana, ila nacho shukuru binafsi namzidi mzungu kwa kufata misingi ya Afrika.

Moja sitambui Biblia maana Biblia ina ujinga mwingi wa kumpa Mzungu thamani.

Pili nafata Vitu vyenye ushaidi kama Mwl Nyerere na Bob Marley najua walikuwepo sifati history ya matango pori.
Mkuu toa ushahidi kwamba Bob Marley alikuwepo bila kutumia historia.Ungejua hata huyo Bob aliamini Mungu yupo na alikuwa msomaji mzuri wa Biblia otherwise asingejua habari ya Shadrach Meshach na Abednego na hata kuwaimba katika moja ya nyimbo zake.
 
Back
Top Bottom