Ujio wa Yesu na Dini

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
686
589
Maneno ya Marehemu Remmy Ongala katika wimbo wa Kilio ukiyasikiliza kwa makini yanaleta hoja nzuri nzuri juu ya mapokeo ya dini, ujio wa Yesu na namna wakoloni walivyotuchota na kutulisha matango pori yao hadi leo tunayatumia.

Vitabu vingi vya dini vimeanza kuandikwa na wao, Hatuna mtu, tulikuwa na dini zetu wakatuambukiza za kwao kwamba zetu hazifai, ujio wa Yesu hadi leo hatokeii vitabu vya dini vinaandika anakuja yu karibu kuanzia miaka mingi iliyopita vizazi na vizazi vimepita tunazaliwa, tunakua na kuzeeka, tunakufa lakini haji. Sasa hii ya anakuja yuko karibu ni nini! Au ndo njia wazungu walizotumia kututuliza ili watutawale vizuri.

Kwa njia hizi naamini wazungu ndo wamechangia asilimia 100 kuturudisha nyuma wenyewe wanaendelea na mpaka leo wanatutawala kutumia vitu mbalimbali wanavyotuletea na misaada. Hivi tumerogwa au tumejiroga! Hatuwezi kurudi kwenye dini za babu zetu.

Wazungu tu ndo walibarikiwa kuonana na Mungu na kuwapa maneno ya kutuandikia sisi. Njia nyingine za kututawala bana!Mababu zetu walikuwa wepesi kiasi hiki kununulika na maneno ya matumaini.

Ngoja tuendelee kumsubiri Yesu bana dah!
Song: Remmy-Kilio
 
Wewe ni Imani gani? Ni nini legacy ya babu zetu?? Kisayansi labda!! Ni nini tunachoweza kujisifia kwa babu zetu!## ni uchawi,,uganga,,uvivu na kuoa na kuchunga mifugo?? Je hata sasa hivi unahisi tutawaachia nini kizazi kijacho?? Bora hata ungechagua imani tu uwaachie urithi watoto wako la sivyo utakuwa kama babu zako...Yesu sio mtu hata aeleweke kwa akili ya kawaida.
 
Huwa najiuliza kilitokea nini hadi watu wakapokwa historia yao.
Wakauziwa huu utapeli unaoitwa dini pamoja na Miungu yake kwa gharama kubwa hata ya maisha yao.

Sasa hivi watu wengi hasa wa nchi masikini ndio wamebaki kuabudu huu utapeli.Hata public figures wasioamini kwenye hayo mambo huwa wanaigiza kuamini ili waonekane wapo pamoja na wafia dini mradi wapate wanachokitaka kutoka kwao.
Yesu hakuwa na uungu kwa namna yoyote ile, alikuwa mtu wa kawaida na alishajifia zamani na kuozea kaburini[possibly aliuawa kwa makosa ya uhaini].
Wanaomsubiri sijui wanasubiri atoke wapi.
Kabla ya kifo chake Yesu alisema angerudi kabla ya kufa kwa watu waliokuwa wakimsikiliza.Cha kushangaza leo ni miaka 2017 hajaonekana popote.Kama kuna mtu anayemsubiri Yesu arudi au anayesubiri siku ya kiama ifike, huyo ni wa kumtibu.
 
Badonkwa Huruma Anasema "Baba wasamehe hawajui watendalo. "

USHUKIE MASIHA, KUWAOKOA WATUMWAO
MKOMBOZI MASIHA, NJOO NJOO NJOO
SHUKA KWETU SIKAWIEE
 
We jifariji hata nafsi yako inakushuhudia kwamba Kristo atarudi ndio maana ukaandika,heri uokoke mapema maana atakaye kosa mwaliko ule itakuwa kilio na kusaga meno
 
Wewe ni Imani gani? Ni nini legacy ya babu zetu?? Kisayansi labda!! Ni nini tunachoweza kujisifia kwa babu zetu!## ni uchawi,,uganga,,uvivu na kuoa na kuchunga mifugo?? Je hata sasa hivi unahisi tutawaachia nini kizazi kijacho?? Bora hata ungechagua imani tu uwaachie urithi watoto wako la sivyo utakuwa kama babu zako...Yesu sio mtu hata aeleweke kwa akili ya kawaida.
Wewe ni Imani gani? Ni nini legacy ya babu zetu?? Kisayansi labda!! Ni nini tunachoweza kujisifia kwa babu zetu!## ni uchawi,,uganga,,uvivu na kuoa na kuchunga mifugo?? Je hata sasa hivi unahisi tutawaachia nini kizazi kijacho?? Bora hata ungechagua imani tu uwaachie urithi watoto wako la sivyo utakuwa kama babu zako...Yesu sio mtu hata aeleweke kwa akili ya kawaida.
endelea kujidanganya hivo hivo
 
Mzungu ana akili sana, ila nacho shukuru binafsi namzidi mzungu kwa kufata misingi ya Afrika.

Moja sitambui Biblia maana Biblia ina ujinga mwingi wa kumpa Mzungu thamani.

Pili nafata Vitu vyenye ushaidi kama Mwl Nyerere na Bob Marley najua walikuwepo sifati history ya matango pori.
 
Wewe ni Imani gani? Ni nini legacy ya babu zetu?? Kisayansi labda!! Ni nini tunachoweza kujisifia kwa babu zetu!## ni uchawi,,uganga,,uvivu na kuoa na kuchunga mifugo?? Je hata sasa hivi unahisi tutawaachia nini kizazi kijacho?? Bora hata ungechagua imani tu uwaachie urithi watoto wako la sivyo utakuwa kama babu zako...Yesu sio mtu hata aeleweke kwa akili ya kawaida.

Imani ni suala la kuamini tu, wapo watu wengi katika sehemu tofauti wanaendelea kuamini vitu mbali mbali na wanaamini pia vinawasaidia tofauti na hizi dini za mzungu ambazo zinatuaminisha kuendelea kuwanyenyekea. Vitabu walivyoviandika wakatuletea vinatuonesha kuwa hakuna mtu mweusi aliyetumiwa kupewa neno. Ni vizuri kuendelea kuamini walichokuwa wakiamini watu wa zamani (mababu zetu) ambacho kiliwajenga na kufanya waishi kwa amani zaidi tofauti na dini ya mzungu.
 
We jifariji hata nafsi yako inakushuhudia kwamba Kristo atarudi ndio maana ukaandika,heri uokoke mapema maana atakaye kosa mwaliko ule itakuwa kilio na kusaga meno

Lini sasa!! Hivi wazungu wasingeleta hizi dini wangeliweza kututawala kirahisi!! si wangeua watu wengi sana. Walileta dini ili kutu subject tuwe chini yao wanyenyekevu.
 
Huwa najiuliza kilitokea nini hadi watu wakapokwa historia yao.
Wakauziwa huu utapeli unaoitwa dini pamoja na Miungu yake kwa gharama kubwa hata ya maisha yao.

Sasa hivi watu wengi hasa wa nchi masikini ndio wamebaki kuabudu huu utapeli.Hata public figures wasioamini kwenye hayo mambo huwa wanaigiza kuamini ili waonekane wapo pamoja na wafia dini mradi wapate wanachokitaka kutoka kwao.
Yesu hakuwa na uungu kwa namna yoyote ile, alikuwa mtu wa kawaida na alishajifia zamani na kuozea kaburini[possibly aliuawa kwa makosa ya uhaini].
Wanaomsubiri sijui wanasubiri atoke wapi.
Kabla ya kifo chake Yesu alisema angerudi kabla ya kufa kwa watu waliokuwa wakimsikiliza.Cha kushangaza leo ni miaka 2017 hajaonekana popote.Kama kuna mtu anayemsubiri Yesu arudi au anayesubiri siku ya kiama ifike, huyo ni wa kumtibu.

Wameleta dini lakini wengi wao sasa hivi hawaamini katika dini bali wanaamini katika science, wanatumia akili nyingi kuvumbua na kutuacha tukilia shida kuamini shetani ndo kaileta na ili kutoka katika hiyo shida tunapaswa kukesha tukiomba msaada kwa Mungu badala ya kufanya kazi kwa bidiii....
 
Mtu nyumba za ibada anashinda kama kaajiliwa humo..! Siku ya kusali akienda mpaka mnamsahau..! Utindiga huo sifanyi kabisa. Nilifanya wakati nafunga ndoa ndio nilikubali huo upwenku.

Toka niwe kundi la Mchungaji wangu Bob nawaza pesa tu kama Wachina. Mapunziko ya akili 300 tu nakuwa fresh full Upendo kwa Raia.
 
Nashindwa kuelewa kuwa wazungu ndio waliyoanzisha dini au nao pia waliletewa dini kama waafrika hali ya kuwa nao wazungu walikuwa na imani zao mbalimbali? maana naona lawama za hizi dini zinaenda kwa wazungu kuwa ndiyo waliyoanzisha hizi dini.

Halafu ikiwa kweli wazungu ndiyo waliyoanzisha hizi dini na wamefanikiwa kwa kiasi hiki je,hatuoni kuwa na mambo mengine watakuwa wameyabuni pia kwa manufaa yao na wamefanikiwa kutuchota akili kama walivyofanya kwenye dini?
 
Mtu nyumba za ibada anashinda kama kaajiliwa humo..! Siku ya kusali akienda mpaka mnamsahau..! Utindiga huo sifanyi kabisa. Nilifanya wakati nafunga ndoa ndio nilikubali huo upwenku.

Toka niwe kundi la Mchungaji wangu Bob nawaza pesa tu kama Wachina. Mapunziko ya akili 300 tu nakuwa fresh full Upendo kwa Raia.
Ukikuta mtu anaamini dini kwa 60% na kuendelea, huyo ana matatizo ya kihisia ama ya kisaikolojia.
 
Wameleta dini lakini wengi wao sasa hivi hawaamini katika dini bali wanaamini katika science, wanatumia akili nyingi kuvumbua na kutuacha tukilia shida kuamini shetani ndo kaileta na ili kutoka katika hiyo shida tunapaswa kukesha tukiomba msaada kwa Mungu badala ya kufanya kazi kwa bidiii....
Mkuu kuacha kuamini katika dini na kuamini katika sayansi ndiyo kupi huko? unamaanisha wazungu mwanzo walikuwa wakiumwa wanaenda kwenye nyumba za ibada badala ya hospitali kwa sababu walikuwa wanaamini dini ama VP?
 
Dini iliundwa kwa ajili ya mtu mweusi na maskini, wao wengi hawaamini. kiwango cha maendeleo kimewafanya waamini zaidi katika uvumbuzi na jitihada na kuona kwamba hawana cha kuomba kama kila kitu kinaweza kupatikana. Kwa mtu mweusi asilimia kubwa ya watu wanakimbilia kwenye hayo makanisa kupata msaada wa maombi bila kufikiria namna ya kutatua tatizo hilo kwa njia nyingine.
 
Mtu nyumba za ibada anashinda kama kaajiliwa humo..! Siku ya kusali akienda mpaka mnamsahau..! Utindiga huo sifanyi kabisa. Nilifanya wakati nafunga ndoa ndio nilikubali huo upwenku.

Toka niwe kundi la Mchungaji wangu Bob nawaza pesa tu kama Wachina. Mapunziko ya akili 300 tu nakuwa fresh full Upendo kwa Raia.
Io pia ni dini tu cema hujijui
 
Dini iliundwa kwa ajili ya mtu mweusi na maskini, wao wengi hawaamini. kiwango cha maendeleo kimewafanya waamini zaidi katika uvumbuzi na jitihada na kuona kwamba hawana cha kuomba kama kila kitu kinaweza kupatikana. Kwa mtu mweusi asilimia kubwa ya watu wanakimbilia kwenye hayo makanisa kupata msaada wa maombi bila kufikiria namna ya kutatua tatizo hilo kwa njia nyingine.
Hujajibu swali mkuu ndiyo kwanza unazidi kunichanganya kwa kuniambia dini zimeundwa kwa ajiri ya watu weusi na masikini maana utanifanya nianze kuuliza maswali mengi mengine ili nipate uhalisia usemacho.

Nimeuliza kuacha kuamini katika dini na kuamini katika sayansi ndiyo nini? ina maana mwanzoni wazungu walikuwa wakiumwa wanaenda kwenye nyumba za ibada na si hospitali kwa sababu hawakuamini sayansi?
 
Back
Top Bottom