Ujio wa Tundu Lissu utawaunganisha CCM

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,034
50,956
UJIO WA TUNDU LISU UTAWAUNGANISHA CCM.

Anaandika Robert HERIEL.

Kheri ya Mwaka MPYA Ndugu zangu. Nimesikiliza Hotuba zote mbili za viongozi wetu. Hotuba ya Rais wetu Mama Samia Suluhu, kisha nikamsikiliza Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Tundu Lisu.
Sio lengo langu kuelezea hotuba zao lakini nitagusia Kwa uchache Kauli ya Lisu katika hotuba yake kuhusu kurudi hapa nchini.

Kurudi Kwa Tundu Lisu Tanzania kutainufaisha zaidi CCM kuliko CHADEMA.

Kwa Hali ilivyo Kwa sasa hapa nchini, Vyama vya Kisiasa hasa vya upinzani nguvu yake ni hafifu na ipo dhoofu kuliko wakati wowote ule. Nafikiri awamu ya tano imechangia Kwa kiasi kikubwa kudhoofisha Vyama hivi.

Kitu pekee ambacho ninakiona mara Kwa mara kikijitokeza ni kuwa CCM hakiruhusu Vyama vingine kuweka mifumo imara na kujiimarisha. Hii ni kusema Vyama vya upinzani hapa nchini havina mifumo imara yakueleweka Jambo ambalo linaathiri malengo Yao ya kushika Dola.

CCM ndio chama kilichojidhatiti Kwa kuweka mifumo imara, na hii ndio nguzo Yao muhimu inayowafanya waendelee kushika Dola na Kama hatua za akili za makusudi hazitafanyika basi ni wazi CCM bado inamuda mrefu kuitawala nchi hii.

Kila Vyama vya upinzani vinapokaribia kuweka mifumo imara, CCM huibomoa upesi kabla havijaimarika.

Moja ya mbinu za CCM kubomoa mifumo tishio ya upinzani ni kuhakikisha Wale watu wenye ushawishi na wenye madhara ndani ya Vyama vya upinzani hawapatani. Na Kama wapo chama kimoja basi huwagombanisha ikiwezekana kumnunua mmoja wao ili Kupunguza nguvu ya upande wa pili.

Kwa Hali ilivyo hapa nchini Tundu Lisu hata angeruhusiwa aje Leo hii itamuwia vigumu ku-perform na kupata matokeo chanya kwa upande wa chama chake.

Kisiasa huwezi kifuta chama kinzani Kwa sababu Kwa kufanya hivyo utakuwa unajitengenezea mazingira mabaya Kwa chama chako na kutengeneza upinzani ndani ya chama chako mwenyewe.
Unachoweza kufanya ni kukata Ile mizizi mikuu ya Vyama vya upinzani na kuacha mizizi legelege tuu.

Migogoro ya CCM wenyewe Kwa wenyewe ni matokeo ya kuishi pasipo tishio kubwa kutoka nje ya chama Chao. Kama Hali itaendelea kuwa hivi inaweza kuwa hatari Kwa CCM kuliko upinzani.

CCM Kwa sasa ili irudi kuwa na umoja itahitaji tishio kutoka nje ya chama Chao ambalo litawaunganisha na kuwaleta Pamoja.

Ujio wa Tundu Lisu ni kete muhimu Sana Kwa upande wa CCM kujiimarisha ingawaje CCM wenyewe hawalioni Jambo hili.
Ujio wa Lisu utaondoa mivutano na migongano isiyo na ulazima ndani ya CCM.

Kwani Lisu akija Kama mlivyomsikia kwenye Hotuba yake yeye anakawaida ya kushambulia pande zote za makundi ya CCM kuanzia Kundi la Sukuma Gang Kwa kumshambulia Hayatti Magufuli, na pia kumshambulia Mama Samia moja Kwa moja.

Wafuasi wa Magufuli wataungana na kundi lililopo Utawalani sasa hivi ikiwezekana Kwa dharura kwani wote wanajua Kama CCM ikianguka wote hawatasalimika. Hivyo Suluhu ni kuondoa Kwanza tofauti zao na kupambana na tishio kutoka nje.

Kuungana kwao ndio manufaa zaidi ya CCM wakati upande wa Upinzani wakiambulia patupu.

Nature ya Watanzania hupenda kutetewa lakini baada ya mambo kukaa Sawa hawaungani na Wale waliowatetea.

Watanzania wengi ni Sawa na Mwanamke aliyepo kwenye ndoa ambaye ameolewa alafu anapata kero za mume wake, alafu anatokea mwanaume mwingine(mchepuko) ambaye humtetea mwanamke huyo Kwa kupigania haki zake na kumpa Baadhi ya Huduma. Mchepuko akitegemea mwanamke huyo atamuacha mume wake na kuhamia kwake.
Lakini kumbe mwanamke huyo Hana mpango wa kumuacha mume wake isipokuwa anamtumia mchepuko Kama mwamvuli wa kumkinga na jua na mvua(madhila ya Mumewe), na jua na mvua zikiisha hutupa mwamvuli na kuendelea na mume wake.

Hivyo ndivyo Watanzania walivyo kwenye Siasa za TANZANIA.

Wanakusakazia uwatetee Kwa gharama zako Kwa ajili Yao, unapatwa na madhila wao wala hawako huko. Wakipata uliowatetea ama hawajapata bado hawataachana na mume wao CCM.

Upinzani wanajua moja ya Mfumo na mzizi wanaotakiwa kuukata unaoishikilia CCM ni pamoja na Katiba ndio maana wanadai Katiba mpya ili Baadhi ya vipengele viondoshwe na vingine viongezwe ili pawe na mizani Sawa katika mapambano ya kushika Dola.

Lakini Jambo moja la hakika ni kuwa Watanzania wengi ni Kama mfano nilioutoa hapo juu. Wengi wanaogopa kutoa talaka Kwa CCM. Hata hivyo kutoa Talaka Kwa mume au mke uliyemzoea sio Jambo rahisi Kwa wazoefu wa mambo watakuambia.

Lisu aje, lakini sioni Kama kuna Vijana werevu wenye msimamo Kama yeye. Wengi nawaona hawawezi kuhimili miliki mikiki. Wengi wao ni rahisi kununuliwa tena Kwa bei Sawa na bure. Wengi wao ni wachumia tumbo ambao Siasa kwao ni Ajira. Wengi wao ni watu wasio na dhamiri ya kweli ya uzalendo kulikomboa taifa hili isipokuwa wanaongozwa na uchu na wivu Kwa kuwaona wenzao wakiwa kwenye mifumo ya kuila keki ya taifa alafu wao wakigeuka Paka wa nyumbani wanaojikomba Kwa wenye Nyumba.

Lisu ni mzizi Mkubwa ambao utahitaji mizizi mingine isiyopungua mitano ili kuweka kukamilisha malengo Yao ya kushika Dola. CCM nao hawakubali mizizi mikubwa iimarishe upande wa pili.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Andiko reefu kuisiffia CCM, ungeandika kuwa CCM hairuhusu vyama vya upinzani kujiimarisha kwasababu 1. Inaogopa kung'olewa madarakani hivyo inatumia dola kudhoofisha vyama vya upinzani 2. CCM ni chama dola wanategemea vyombo vya ulinzi na usalama ili waendelee kukaa madarakani na ndiyo maana hawakubali mabadiliko ya sheria haswa sheria mama (Katiba)
 
Andiko reefu kuisiffia CCM, ungeandika kuwa CCM hairuhusu vyama vya upinzani kujiimarisha kwasababu 1. Inaogopa kung'olewa madarakani hivyo inatumia dola kudhoofisha vyama vya upinzani 2. CCM ni chama dola wanategemea vyombo vya ulinzi na usalama ili waendelee kukaa madarakani na ndiyo maana hawakubali mabadiliko ya sheria haswa sheria mama (Katiba)
Umesoma kwa hisia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi, Lissu si rafiki wa Watanzania wengi.

Tutampinga huyu kibaraka wa mabeberu.

#kataawahuni
 
Rais Samia aruhusu siasa za ushindani, na awaambie wabunge wa ccm wa mbeleko ya magufuli watapambana na upinzani bila kubebwa na wakurugenzi uone ka huko ccm wataanza kumshambulia Rais, maana kauli ya Ndugai ingetakiwa itolewe na upinzani, ccm hubugi kutaka kufuta upinzani wakati upinzani ukiwa busy kila mwana ccm huwaza kutetea ubunge jimboni, Jk alikuwaga mjanja alijua ccm ni hatari kwa makundi so akaruhusu upinzani wapambane na ccm, na ndani ya ccm wakawa busy na upinzani na kusahau makundi na wakaungana
 
Sipingani na ww mtoa mada kwa kuongezea watanzania sawa na mwanamke malaya/ barmed hawaaminik hata umpe gar atagooo out tu na mwingine leo hiyi lisu lisu lisu lakini wamesahau huyo huyo lisu aliwataka waandamane kupinga matokeo ya upigaji kura nani aliandamana?? Kama sio wanafiki hawa kelele tu mitandaon matendo ziloo Hili taifa watu wake wana laana kubwa
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom