ujinga wa wazazi wengi tanzania

Kiboko Yenu

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
311
65
wanazaa watoto wengi na hovyo hovyo ambao wanashindwa mpaka kuwahudumia matokeo yake wanakaa kulaumu hovyo oh maisha magumu nashindwa somesha familia kama wangekuwa wachache wasingelaumu
 
i kweli hata mimi hua nashangaa sana mtu hana kazi ila ana watoto nane na wake wawili
 
This is from Etic point of view. Ukiwapa nafasi ya kukuelezea kwa nini wanayafanya hayo utashangaa how shallow you are. Kumbuka human being is always a rational animal............. whether from the eye you are eyeing it or not. Wape nafasi
 
i kweli hata mimi hua nashangaa sana mtu hana kazi ila ana watoto nane na wake wawili

...huwezi jua, kati ya hao nane mmoja aweza "watoa" kimasomaso wazazi wake...
tajiri na mali zake, maskini na watoto--- aliimba Remmy Ongala (R.I.P)
 
wanazaa watoto wengi na hovyo hovyo ambao wanashindwa mpaka kuwahudumia matokeo yake wanakaa kulaumu hovyo oh maisha magumu nashindwa somesha familia kama wangekuwa wachache wasingelaumu

Mkuu hueleweki, nikionacho hapa ni wewe kutokwa na mapovu mdomoni! Hakuna mzazi anaezaa hovyo hovyo, Acha ubaguzi usio na msingi. Maisha ni Magumu kweli.
 
...huwezi jua, kati ya hao nane mmoja aweza "watoa" kimasomaso wazazi wake...
tajiri na mali zake, maskini na watoto--- aliimba Remmy Ongala (R.I.P)

Mbu umenifanya nicheke :lol:

wanasema kila mtoto anazaliwa na bahati yake hivoo!!!
 
kama huwezi kuwapa msaada waache watajua wenyewe.

mchungaji mmoja alisema kwao walikuwa 10 bahati mbaya mmoja keshatwaliwa (R.I.P)
na wote wana kazi nzuri na maisha yanasonga.
 
wanazaa watoto wengi na hovyo hovyo ambao wanashindwa mpaka kuwahudumia matokeo yake wanakaa kulaumu hovyo oh maisha magumu nashindwa somesha familia kama wangekuwa wachache wasingelaumu

Wengine wana wachache alafu bado wanakaumu
 
...huwezi jua, kati ya hao nane mmoja aweza "watoa" kimasomaso wazazi wake...
tajiri na mali zake, maskini na watoto--- aliimba Remmy Ongala (R.I.P)

Ndo wanachoamini japo hakina ukweli ndani yake
 
Mkuu hueleweki, nikionacho hapa ni wewe kutokwa na mapovu mdomoni! Hakuna mzazi anaezaa hovyo hovyo, Acha ubaguzi usio na msingi. Maisha ni Magumu kweli.

Nadhani wengine wanakuja kuwapiga vijembe majirani zao humu jf kitu ambacho hakitawasaidia labda wangewaendea na kuwaambia ukweli
 
Ndo wanachoamini japo hakina ukweli ndani yake

Faith and hopes are linked! ...wanaamini na inakuwa kweli...
fikiria kwa wigo mpana zaidi, kuna wataoolewa hapo, na wataozaa...
hata ikibidi kusubiri 30yrs, faida itapatikana tu...kama kilimo cha mitike!
 
rasilimali za Taifa mbona zipo za kumwaga. tatizo letu ni ujinga wa kuzitumia.tukizutumia vizuri naamini Tanzania kila mtoto anayezaliwa angekuwa analipwa posho!
 
Kuna mwengi behind pazia jamani do not just starting blaming them.
Kuna gender issues - forced sex or rape kwa wanana na waume zao. Kumbukeni katika familia nyingi habari ya uzazi wa mpango bado ni ndoto za alinacha, Mzee amerudi ana 'hitaji" we mama unakimbilia kumsomesha kalenda anaelewa? unamletea mipira anakuelewa? yeye yuko high anachotaka ni kutimiziwa- inakubamba.
Wamama tunafundwa ukiolewa huna amri na mwili wako, huruhusiwi kulala na nguo ya ndani, mzee anarudi na mbili baridi moja moto kichwani, utamwelewesha?? ukimgomea kesi!
Wengine wanaingiliwa hata wakiwa ndo wametoka kujifungua, wakilalamika kuwa wana vidonda wanaambiwa watoe mlango mwingine, wakisema wako MPs wanaambiwa kuna lango mwingine.
Above all abortion ni dhambi, imenasa unafanyaje?? Jamani tambueni kuwa wanawake wenye say ni wachache sana tena kati ya hao wanaojiita wasomi ambao kwa bahati mbaya katika hili wanaonekana hawana maadili. Nenda NBS tizama TDHS ya mwaka 2010 bado inaonyesha watu wenye watoto wengi ni wale ambao wake hawana elimu kubwa.
So kabla hujaanza kuwanyooshea vidole na kuwakaripia kwa sauti ya ukali, wape nafasi wajieleze yanayowasibu.
 
..............................neendeni mkaijaze dunia......................
 
Back
Top Bottom