"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

WOS, asante kwa hii.
Leo nimefanikiwa kufika msibani na kuzungumza 3rd witness at the scene, kiukweli kinachoripotiwa kumhusu huyu binti, sicho kilichotokea!. Rest assured hicho nilichosikia kama sio uwongo mwingine, then huyu binti ni innocent victim wa male aggression na Kanumba ameanguka mwenyewe!. Lets wait and see!.
 
Kwa sababu imejaa speculation na ambayo haiwezi kuthibitika mkuu. Ulivyoisema is as if una uhakika nayo wa 100% wakati ni kitu ambacho umekiwaza tu kwenye akili yako.
Nadhani kwa mtu muelewa huwezi kuleta jukwaani analysis ambazo zimekua influenced na individual subjectvism/ guess. Katika hali halisi hiyo namba moja ndivyo ilivyo unless uniambie una uthibitisho kwamba Kanumba alikua anambaka huyu binti.

lulu alipohojiwa kwenye show ya mkasi kuhusiana na maswala ya mapenzi alikataa kuwa yeye ana mpenzi.
Hii inaweza kutafsiriwa kwamba
1.ni kweli hakuwa na mpenzi bali ni porojo za mtaani,kwanza yeye ni mdogo wa kufanya mambo hayo, na alijitahidi kuonyesha hivyo kulingana na reaction mbele ya kamera ya Eatv.
2.aliamua kukanusha jambo hili lakini kuna nafsi ilimkumbusha kuwa 'yuko kanumba ambaye labda kila siku anamlazimisha kufanya tendo la ndoa bila maridhiano' na hivyo wakati umefika wa kumzuia kwa njia yoyote ile.ni wakati wa kuachana na maswali yanayoumiza nafsi!

Ni kweli kabisa siwezi kuwa na uhakika wa 100% .ninachojaribu ni kupanua uwigo wa fikra tu.
I hope utanielewa.
 
WOS, asante kwa hii.
Leo nimefanikiwa kufika msibani na kuzungumza 3rd witness at the scene, kiukweli kinachoripotiwa kumhusu huyu binti, sicho kilichotokea!. Rest assured hicho nilichosikia kama sio uwongo mwingine, then huyu binti ni innocent victim wa male aggression na Kanumba ameanguka mwenyewe!. Lets wait and see!.

Hicho hata mimi ndicho ninachohisi. Kama kweli jamaa alikuwa amegida "Jacky Daniel" basi kuna uwezekano mkubwa balance yake ilikuwa impaired na hivyo katika purukushani kusababisha kuanguka.

Haingii akilini kabisa eti Lulu awe na miguvu ya kumsukuma Kanumba (who most likely weighs twice as much as she does and who is much bigger - almost six feet tall - when Lulu more than likely she's not even 5'1.)
 
WOS, asante kwa hii.
Leo nimefanikiwa kufika msibani na kuzungumza 3rd witness at the scene, kiukweli kinachoripotiwa kumhusu huyu binti, sicho kilichotokea!. Rest assured hicho nilichosikia kama sio uwongo mwingine, then huyu binti ni innocent victim wa male aggression na Kanumba ameanguka mwenyewe!. Lets wait and see!.
Pasco nisaidie kaka, hivi lulu alifikaje Oysterbay polisi?
nisamehewe bure jamani kama hili limeonyeshwa mahali...
 
WOS hongera kwa thread ya kisheria zaidi
huku ukiwa makini kuweka points bila 'kuanzisha vita dhidi ya mfumo dume au abusive partners'

wasiwasi wangu ni kuwa hii kesi inaweza kuwagawa watu......badala ya kutazama incompetence ya polisi
watu wakaanza kugawanyika kijinsia...zaidi...na sio kutazama facts..

hii thread iko deep...hongera....
 
Hili tukio lina maswali Mengi yenye kuhitaji majibu ya kina, lakini mpaka sasa inaonekana hata police hawajuhi waanzie wapi na waishie wapi, maana hata uchunguzi haujakamilika police wameshaweka nusu ya report

1: Lulu alipokuja kumwambia seth kuwa kanumba ameanguka, alikuja na ngeu ama alikuwa mzima? (jibu kutoka kwa seth)
2: Lulu alipoondoka hapo aliekea wapi na kwa usafiri gani? (Jibu kutoka kwa LUlu)
3: Lulu alikamatwa kwa kutafutwa na polisi ama alienda mwenyewe? (Police)
4: Lulu alikuwa chini ya polisi baada ya muda gani tangu kifo cha Kanumba? (Police/Lulu/Seth)
5: alipokuwa chini ya police alikuwa bado anableed ama alikuwa na ngeu tu bila damu? (Police)
6: Record yake ya simu inaonyesha Lulu aliongea na watu gani, kabla ya kuja kwa Kanumba, na wakati yupo kwa Kanumba (simu iliyoleta ugomvi) na baada ya kutoka kwa Kanumba? (Lulu/Kampuni ya simu husika/Police)
7: Kanumba alishakiri hivi karibuni kuwa hawaelewani na Ray (Mikasi na Salama), na Ray alikuwa ni Mshirika mkubwa wa Lulu je kuna connection yoyote kati ya LUlu/Ray na kifo cha Kanumba? (Lulu/Ray/Police)
8: Inavyosemekana Lulu alikamatwa Bila nguo, sasa hizo nguo zilipotelea wapi?, maana alikuja na nguo na akakimbia getini ili atoke nje akiwa na nguo na alipoingia ndani tu ndio kanumba akadondoka, sasa iweje akutwe uchi? (Lulu/Seth/police)
9: Hao police wametumia kipimo gani kujua kuwa Kanumba amekunywa Jack Daniel na wala sio Captain Morgan , maana unaweza kuzitofautisha hizi pombe kwa type zake (Lager, Ciders, Whisky, Gin, Wine, nk) (Police/Seth/Lulu/Mkemia)
 
WOS hongera kwa thread ya kisheria zaidi
huku ukiwa makini kuweka points bila 'kuanzisha vita dhidi ya mfumo dume au abusive partners'

wasiwasi wangu ni kuwa hii kesi inaweza kuwagawa watu......badala ya kutazama incompetence ya polisi
watu wakaanza kugawanyika kijinsia...zaidi...na sio kutazama facts..

hii thread iko deep...hongera....

Incompetence iliyoonyeshwa na polisi ni ya aina yake. Ile kauli ya yule kamanda mimi ndiyo imenichosha kabisa.
 
Mnaweza gungua muuaji wa kanumba ni aliyepiga simu iliyoleta ugomvi. Kwa sababu mmeamua kuisaidia polisi basi nami nachangia. Kama kanumba alifanikiwa kunyang'anya cm, aliambiwa nini? Hakushinikizwa kumshughulikia lulu? Hakuambiwa maneno ya kumfanya alegee. Kwa mfumo dume wetu, lulu hana ubavu wa kumuua kanumba.
 
Incompetence iliyoonyeshwa na polisi ni ya aina yake. Ile kauli ya yule kamanda mimi ndiyo imenichosha kabisa.

na ukichanganya na mfumo wetu wa watu kubeba 'mwili wa marehemu' anaeshukiwa kuuwawa
wenyewe bila hata polisi wala ambulance za viwango kuja kwenye tukio..
ukichanganya hapo unapata one big circus....
 
WOS, asante kwa hii.
Leo nimefanikiwa kufika msibani na kuzungumza 3rd witness at the scene, kiukweli kinachoripotiwa kumhusu huyu binti, sicho kilichotokea!. Rest assured hicho nilichosikia kama sio uwongo mwingine, then huyu binti ni innocent victim wa male aggression na Kanumba ameanguka mwenyewe!. Lets wait and see!.
Asante Pasco!
Tutasikia mengi hasa baada ya msiba na situation kurudia normalcy.
 
na ukichanganya na mfumo wetu wa watu kubeba 'mwili wa marehemu' anaeshukiwa kuuwawa
wenyewe bila hata polisi wala ambulance za viwango kuja kwenye tukio..
ukichanganya hapo unapata one big circus....

Si ndo hapo!

Ingekuwa kwingine hao nao wangeshitakiwa kwa interference with official acts lol.
 
Incompetence iliyoonyeshwa na polisi ni ya aina yake. Ile kauli ya yule kamanda mimi ndiyo imenichosha kabisa.
Na hao ndo Law enforcers sasa...

Hivi niulize, mara kadhaa nimesoma kuwa polisi wamesema marehemu alikunywa 'jack daniel's'...wao walijuaje?
 
Incompetence iliyoonyeshwa na polisi ni ya aina yake. Ile kauli ya yule kamanda mimi ndiyo imenichosha kabisa.

I wanted to comment on the same thing, its highly unlikely and very unproffesional for a senior police official to issue passing,suggesting remarks which are really layman's thinking....

If I were lulu, knowing that am a prime suspect and all, I will insist for a proper autopsy(sp) before that body is laid to rest,we don't have exhume(sp) cases in TZ ...

Further to that, there is too much effort on burying Kanumba in style...am just thinking loudly...all these costs, stages and all, pamoja na posho za wanakamati..the whole thing might cost 50M....sasa mama yake atabaki na nini maana kufa kufaana hapa...

And jack ur observation is spot on, doctor wa Kanumba should also give his medical history....

Simu ya lulu pamoja na ya marehemu pia zichunguzwe, nyendo zake kabla na mawasiliano yake kabla hajakata roho, simu ya Seth pia iwe seized, maana polisi inabidi wawe extremely impartial on this
 
Umegusa penyewe kabisa!
Ukiangalia mazingira ya tukio, sijaona kiwango cha kuridhisha kutosha kukusanya ushahidi forensically.Eneo la tukio limeingiliwa na watu wa kila aina kiasi ambacho sijui kama kweli inawezekana kupata forensic evidence.Pia Kanumba alipofikishwa Muhimbili alipelekwa motuary moja kwa moja......

Na inasemekana uchunguzi uliofanyika katika mwili wake ni wa ku-scan kichwa kama kina majeraha!! Wakati kuna narration toka kwa Seth kwamba marehemu alikuwa anatokwa na mapovu mdomoni!! Sasa kama ndivyo, hapo autopsy ilikua haiepukiki; sasa sijui kama walimfanyia autopsy, au kama wamechukua sampuli za damu au sehemu za mwili wake (kama ini n.k.) kwa ajili ya uchungunzi zaidi!

Hapo kuna kuhitaji weledi wa forensic pathologist katika kuweza kutoa majibu kamili.
 
Anayejua kilichotokea chumbani lulu na kanumba, bahati mbaya mmoja kaondoka, seth siyo shuhuda wa tikio lilitokea chumbani ila ni ni shuhuda wa matokeo ya kilichofanyika kati ya lulu na kanumba. Hii kesi ni ngumu sana kumcovict lulu!
 
na ukichanganya na mfumo wetu wa watu kubeba 'mwili wa marehemu' anaeshukiwa kuuwawa
wenyewe bila hata polisi wala ambulance za viwango kuja kwenye tukio..
ukichanganya hapo unapata one big circus....

Kifo cha Rais wa Malawi, Bwana Bingu wa Mutharika na Msanii wa filamu wa Tanzania Bawa Kanumba (The great) vinaonyesha jinsi gani Afrika tunavyokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Huduma za Magonjwa ya Dharura. Mifano hiyo miwili inaonyesha jinsi gani, tatizo hili lilivyokuwa kubwa Afrika, kwa mfano baada ya Rais Bingu wa Mutharika kupatwa na tatizo la moyo wake kusisimama (Cardiac Arrest) alikimbizwa hospitali ya Lilongwe na gari ya kawaida, si Ambulance kisha alionekana akiingizwa hospitalini kwa kutumia baiskeli ya matairi mawili (Wheelchair), mgonjwa wa ''Cardiac Arrest'' anakimbizwa hospitali na Gari ya kawaida kisha anaingizwa hospitali na ''Wheelchair'''??.

Aidha, kifo cha msaanii wa filamu Tanzania, Bwana Kanumba kilichotokea jana saa 9 usiku nacho kimetokea katika mazingira hayo hayo, alianguka nyumbani kwake, hakuna huduma yeyote ya dharura aliyopewa wakati alipokuwa anakimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kufia njia, hakukuwa na ''Ambulance'' iliyomkimbiza Muhimbili??. Hii ni mifano tu ya vifo vilivyotokea Afrika vilivyosababishwa na magonjwa ya dharura, kwa mawazo yangu ni vifo vilivyoweza kuzuilika kama kungekuwa na huduma bora za magonjwa ya dharura katika nchi hizo. Viongozi wengi wa nchini za Kiafrika, Tanzania ikiwemo hazitilii mkazo kabisa, kuimarisha huduma za magonjwa ya dharura katika nchi zao, na pindi wanapopatwa na magonjwa ya dharura watu wao, huwa na mawazo ya kuwakimbiza nchi za nje kama South Africa, Israel au India, lakini wanasahau kuwa magonjwa ya dharura yanapotokea kunakuwa hakunaga muda wa kupoteza (time is critical), ukishazipoteza dakika za mwanzo, hakuna utakachoweza kufanya kumuokoa mgonjwa hata kama mgonjwa atakimbizwa kwenye hospitali iliyobora kiasi gani.

Huduma za magonjwa ya dharura zinaanza mara moja katika eneo la tukio, Wataalam wa magonjwa ya dharura (Emergency Medicine Specialists) wanaitwa eneo la tukio maramoja na kufika kwenye eneo la tukio na gari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) haraka huku wakiwa na vifaa tiba vya huduma ya kwanza tayari kuokoa maisha ya wagonjwa. Katika nchi zilizoendelea huduma za magonjwa ya dharura ni za hali ya juu, huduma hizo zinafaamika kwa wananchi wote, elimu ya magonjwa ya dharura zinatolewa kwa wanchi wote na wanafahamishwa nini cha kufanya pindi inapotokea dharura, kuna namba maaluum ambazo unapiga na watoa huduma hufika katika eneo la tukio haraka, lakini katika nchi za Afika ni kinyume chake. Hali ni mbaya, kinachosikitisha ni watawala wa nchi za Kiafrika kutotilia mkazo huduma hii, ikiwa wao ni watu ambao wapo kwenye hatari na kupatwa na magonjwa ya mstuko kutokana na mazingira ya kazi zao za siasa ambazo zina ''stress'' kubwa na kama wataendelea na dharau zao za kutoimarisha huduma hii wataendelea kuangamia maana watakapopatwa na magonjwa ya dharura majukwaani hakutakuwa na mtu wa kuwasaidia ''and their life will be at stake''

USHAURI

Viongozi wa Afrika haraka imarisheni huduma za magonjwa ya dharura kwa kuwajengea uwezo wataalam wao wa ndani kwa

1. Kusomesha wataalam wengi wa magonjwa ya dharura (Emergency Medicine Specialists), kuanzia ngazi ya vyeti (Certificate), stashahada (Diploma), Astashahada (Advanced Diploma), Shahada (Degree) na Udhamili (Master), wakiwemo paramedics.

2. Kununua vifaa tiba vya kisasa vya magonjwa ya dharura na kuviweka katika hospitali za Wilaya, Mkoa na ngazi ya Taifa, pamoja na kuweka na vifaa vya msingi katika Zahanati zote na Vituo vya Afya.

3. Kununua magari ya wagonjwa (Ambulance) yenye vifaa tiba ndani yake na kufanya gari hilo kutoa tiba ya dharura kuanzia kwenye eneo la tukio na katika safari nzima kuelekea hospitali au kituo cha Afya. Magari haya ya wagonjwa yasambazwe katika hospitali na vituo vya afya vyote.

4. Maslahi ya watoa huduma za dharura yaboreshwe ili wapende kufanya kazi yao muhimu ya kuokoa maisha ya watu

5. Kutoa elimu ya umma endelevu kuhusu huduma za magonjwa ya dharura ikiwemo huduma ya kwanza na jinsi gani ya kutoa huduma hiyo kwa watu walipatwa na magonjwa ya dharura majumbani, maofisini, kwenye viwanja na kumbi za starehe n.k.. Elimu hiyo ianzie mashuleni.

6. Mawasiliano ya kati ya wataka huduma na watoa huduma yaboreshwe, kwa mfano kuwe na namba maalum ambayo itatumika kuombea huduma za dharura kama ''Ambulance'' ambazo wananchi watapiga bure (free call) kwa mfano 911. Wanachi wote waelimishwe uwepo wa namba hizo za dharura na jinsi ya kuzipiga.

7. Kuwe na Sera ya Afya ya huduma ya magonjwa ya dharura.

Kama yote hayo hapo juu yatakelezwa na Viongozi wa Kiafrika, maisha ya watu wasio na hatia yataokolewa wakiwemo wanasiasa wenyewe. Vifo vya kina Kanumba na Bingu wa Mutharika vingeepukika. Kwa mfano Kanumba kaanguka nyumbani kwake saa 6 usiku na kapelekwa hospitali ya Muhimbili saa kumi na moja alfajiri, imechukua zaidi ya masaa 5 kumfikisha Muhimbili huku akiwa amekosa kabisa huduma ya dharura ya msingi kuanzia nyumbani kwake.

Tutafakari Waafrika kisha tuchukue hatua.
 
  • Thanks
Reactions: Aza
je baba wa kanumba anamjua lulu?wamewahi kuwasiliana nae?this case is very open.
 
Na inasemekana uchunguzi uliofanyika katika mwili wake ni wa ku-scan kichwa kama kina majeraha!! Wakati kuna narration toka kwa Seth kwamba marehemu alikuwa anatokwa na mapovu mdomoni!! Sasa kama ndivyo, hapo autopsy ilikua haiepukiki; sasa sijui kama walimfanyia autopsy, au kama wamechukua sampuli za damu au sehemu za mwili wake (kama ini n.k.) kwa ajili ya uchungunzi zaidi!

Hapo kuna kuhitaji weledi wa forensic pathologist katika kuweza kutoa majibu kamili.
Kaka hapa ndo uwezo wa jeshi la polisi unapopimwa, kama kzi yao ni kufyatua mabomu ya machozi tu au wanaweza kutafuta haki iliyofichika pia!
 
Kifo cha Rais wa Malawi, Bwana Bingu wa Mutharika na Msanii wa filamu wa Tanzania Bawa Kanumba (The great) vinaonyesha jinsi gani Afrika tunavyokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Huduma za Magonjwa ya Dharura. Mifano hiyo miwili inaonyesha jinsi gani, tatizo hili lilivyokuwa kubwa Afrika, kwa mfano baada ya Rais Bingu wa Mutharika kupatwa na tatizo la moyo wake kusisimama (Cardiac Arrest) alikimbizwa hospitali ya Lilongwe na gari ya kawaida, si Ambulance kisha alionekana akiingizwa hospitalini kwa kutumia baiskeli ya matairi mawili (Wheelchair), mgonjwa wa ''Cardiac Arrest'' anakimbizwa hospitali na Gari ya kawaida kisha anaingizwa hospitali na ''Wheelchair'''??.

Aidha, kifo cha msaanii wa filamu Tanzania, Bwana Kanumba kilichotokea jana saa 9 usiku nacho kimetokea katika mazingira hayo hayo, alianguka nyumbani kwake, hakuna huduma yeyote ya dharura aliyopewa wakati alipokuwa anakimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kufia njia, hakukuwa na ''Ambulance'' iliyomkimbiza Muhimbili??. Hii ni mifano tu ya vifo vilivyotokea Afrika vilivyosababishwa na magonjwa ya dharura, kwa mawazo yangu ni vifo vilivyoweza kuzuilika kama kungekuwa na huduma bora za magonjwa ya dharura katika nchi hizo. Viongozi wengi wa nchini za Kiafrika, Tanzania ikiwemo hazitilii mkazo kabisa, kuimarisha huduma za magonjwa ya dharura katika nchi zao, na pindi wanapopatwa na magonjwa ya dharura watu wao, huwa na mawazo ya kuwakimbiza nchi za nje kama South Africa, Israel au India, lakini wanasahau kuwa magonjwa ya dharura yanapotokea kunakuwa hakunaga muda wa kupoteza (time is critical), ukishazipoteza dakika za mwanzo, hakuna utakachoweza kufanya kumuokoa mgonjwa hata kama mgonjwa atakimbizwa kwenye hospitali iliyobora kiasi gani.

Huduma za magonjwa ya dharura zinaanza mara moja katika eneo la tukio, Wataalam wa magonjwa ya dharura (Emergency Medicine Specialists) wanaitwa eneo la tukio maramoja na kufika kwenye eneo la tukio na gari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) haraka huku wakiwa na vifaa tiba vya huduma ya kwanza tayari kuokoa maisha ya wagonjwa. Katika nchi zilizoendelea huduma za magonjwa ya dharura ni za hali ya juu, huduma hizo zinafaamika kwa wananchi wote, elimu ya magonjwa ya dharura zinatolewa kwa wanchi wote na wanafahamishwa nini cha kufanya pindi inapotokea dharura, kuna namba maaluum ambazo unapiga na watoa huduma hufika katika eneo la tukio haraka, lakini katika nchi za Afika ni kinyume chake. Hali ni mbaya, kinachosikitisha ni watawala wa nchi za Kiafrika kutotilia mkazo huduma hii, ikiwa wao ni watu ambao wapo kwenye hatari na kupatwa na magonjwa ya mstuko kutokana na mazingira ya kazi zao za siasa ambazo zina ''stress'' kubwa na kama wataendelea na dharau zao za kutoimarisha huduma hii wataendelea kuangamia maana watakapopatwa na magonjwa ya dharura majukwaani hakutakuwa na mtu wa kuwasaidia ''and their life will be at stake''

USHAURI

Viongozi wa Afrika haraka imarisheni huduma za magonjwa ya dharura kwa kuwajengea uwezo wataalam wao wa ndani kwa

1. Kusomesha wataalam wengi wa magonjwa ya dharura (Emergency Medicine Specialists), kuanzia ngazi ya vyeti (Certificate), stashahada (Diploma), Astashahada (Advanced Diploma), Shahada (Degree) na Udhamili (Master), wakiwemo paramedics.

2. Kununua vifaa tiba vya kisasa vya magonjwa ya dharura na kuviweka katika hospitali za Wilaya, Mkoa na ngazi ya Taifa, pamoja na kuweka na vifaa vya msingi katika Zahanati zote na Vituo vya Afya.

3. Kununua magari ya wagonjwa (Ambulance) yenye vifaa tiba ndani yake na kufanya gari hilo kutoa tiba ya dharura kuanzia kwenye eneo la tukio na katika safari nzima kuelekea hospitali au kituo cha Afya. Magari haya ya wagonjwa yasambazwe katika hospitali na vituo vya afya vyote.

4. Maslahi ya watoa huduma za dharura yaboreshwe ili wapende kufanya kazi yao muhimu ya kuokoa maisha ya watu

5. Kutoa elimu ya umma endelevu kuhusu huduma za magonjwa ya dharura ikiwemo huduma ya kwanza na jinsi gani ya kutoa huduma hiyo kwa watu walipatwa na magonjwa ya dharura majumbani, maofisini, kwenye viwanja na kumbi za starehe n.k.. Elimu hiyo ianzie mashuleni.

6. Mawasiliano ya kati ya wataka huduma na watoa huduma yaboreshwe, kwa mfano kuwe na namba maalum ambayo itatumika kuombea huduma za dharura kama ''Ambulance'' ambazo wananchi watapiga bure (free call) kwa mfano 911. Wanachi wote waelimishwe uwepo wa namba hizo za dharura na jinsi ya kuzipiga.

7. Kuwe na Sera ya Afya ya huduma ya magonjwa ya dharura.

Kama yote hayo hapo juu yatakelezwa na Viongozi wa Kiafrika, maisha ya watu wasio na hatia yataokolewa wakiwemo wanasiasa wenyewe. Vifo vya kina Kanumba na Bingu wa Mutharika vingeepukika. Kwa mfano Kanumba kaanguka nyumbani kwake saa 6 usiku na kapelekwa hospitali ya Muhimbili saa kumi na moja alfajiri, imechukua zaidi ya masaa 5 kumfikisha Muhimbili huku akiwa amekosa kabisa huduma ya dharura ya msingi kuanzia nyumbani kwake.

Tutafakari Waafrika kisha tuchukue hatua.

Karata,
Hili ulilosema ni zito linahitaj kufanyiwa kazi asap.

Afrika kwa ujumla majuto ni mjukuu...hatuhangaiki na pro-active thinking wala prevention ya kitu chochote labda uje mradi wa wafadhili lol!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom